Huyu Mtangazaji wa michezo wa Clouds tv na fm huku kuongea kwa kubana pua ni maumbile au mapozi tu?

Prognosticator

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
40,125
2,000
Mkuu, wewe ni mtu mzima na unayeheshimika humu JF. Unapoandika vimada vya kitoto kama hivi unajidhalilisha. Tafadhali linda heshima yako.

#1. Ninachojua tu ni kwamba humu Jamvini hakuna mada ya Kitoto, Kizee wala Kiutu uzima na kama ingekuwa ni hivyo basi tungewekewa Vigezo vya jinsi ya Kuanzisha mada na vinavyoendana na Umri wetu ila bahati nzuri tu ni kwamba hili ni Jamvi huru linaloratibu mawazo huru.

#2. GENTAMYCINE nina aina yangu ya kuanzisha uzi na hata Kuichokoza hiyo threads ili iweze kuleta maana akisi ili idadavuliwe na mbinu kubwa katika threads zangu zote huwa naongozwa na kitu Kiuandishi kinaitwa ' anecdote ' na ndiyo maana pamoja na Wewe kusema huo upuuzi / upupu wako wote hapo juu bado GENTAMYCINE anabaki kuwa ni Mtu anayefuatiliwa na wengi humu Jamvini kila uchao hata kama nitaanzisha uzi ambao Wewe utaona si wa hadhi yangu.

#3. Sikujiunga humu JamiiForums ili nilinde au sijui nipate hadhi kwani nimeanza kuwa na hadhi tena kubwa tu hata kabla sijajiunga rasmi humu Jamvini mwaka 2013 ila ninachoshangaa tu ni kwamba japo Wewe ulinitangulia kuwepo humu JF lakini Mimi niliyejiunga mwaka mmoja baadae nimekuzidi kwa kuwa maarufu na kukubalika sasa sijui hiko Kigezo chako kuwa hadhi yangu inashuka umekitoa katika Sayari gani labda iwe ni Sayari ya Wajinga / Mangumbaru wenzako.

#4. Nakupa tu assignment ndogo anza kufuatilia threads zangu zote ambazo nimekuwa nikiwaanzishia hasa Watangazaji wa Electronic Media kisha waangalie wale ' Characters ' wote niliokuwa nikiwasema kwamba wamebadilika au wapo vile vile? Mmoja wapo wa hapa juzi tu alikuwa ni Mtangazaji wa BBC Swahili Salim Kikeke ambapo kuna vitu nilimkosoa japo kuna ' Wapuuzi ' wenzio humu walinishangaa na hadi kunishambulia ila nikuhakikishie tu kuwa katika yale mapungufu yake ( Salim Kikeke ) niliyomtajia 75% ameachana nayo na nadhani hata leo usiku Saa 3 Kamili hadi na Nusu atakuwa zamu akisoma News Bulletin mfuatilie ndipo utajua vyema impact ya GENTAMYCINE ambayo kama ukiwa na IQ ya punje ya mchele kamwe huwezi kuiona.

#5. Kamwe na tena ukome kutaka kunibadilisha Mimi GENTAMYCINE hasa juu ya maandiko yangu humu Jamvini na labda tu nichukue fursa hii adhimu kukuhakikishia kuwa sitokuja kubadilika kwa aina yangu yangu ya Uandishi na Uchangiaji humu halafu huwa siwalazimishi muwe mnazifungua threads zangu au hata kuzisoma posts zangu bali nadhani huwa ni ' Viherehere ' vyenu tu vinawapanda.

#6. Katika Uandishi kuna ' technique ' moja muhimu mno ambayo inatumika nayo huwa ni ' Teaser ' na ndiyo maana kama una akili sawa sawa ungeweza tu kuelewa mapema kwamba kwanini nimekuja na Headline ya aina hiyo kisha katika ' Content ' ya uzi nikachombeza na hiyo Sentensi ya ' Sisi Watu wa Pwani ya Bahari ya Hindi '. Kuna Hoja kubwa hapo ya Kihisia nimeianzisha ambayo sidhani kama kwa upeo wako utaielewa.

#7. Na mwisho labda nikusaidie tu kukuambia kwamba huwa sianzishi humu threads kama kwa ' chuki ' dhidi ya hao niwaowataja na wapo ambao hunifuata hadi katika PM kusema kuwa nimeona mbali na nimesaidia kitu fulani cha kuwabadilisha Walengwa. Na laiti ungejua kwamba hivi ninavyowasema ndiyo nawasaidia na kuwajenga wala usingekurupuka kama vile umebanwa na haja kubwa ya Uharo kuja na takataka yako hii.

Kumbuka ya kwamba GENTAMYCINE ni ' Purely Talented, Charismatic Fella and a Game Changer '.

Nimemaliza.
 

Prognosticator

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
40,125
2,000
Mada ya kitoto wakati na wewe wakili msomi unaogelea humo humo?!!......ndomana Mtikila aliwapuuza sana mawakili wa kibongo bongo!

Achana naye huyo Mpuuzi Mkuu tayari nimeshampa ' dozi ' yaka na nadhani sasa anaisoma na pengine inaweza ikambadilisha Kifikra, Kimawazo na hata Kiupeo. Anadhani Watu humu huwa tunakurupuka tu wakati kumbe tunajua tunalolifanya.
 

Black jew

Member
Sep 4, 2017
50
125
Kuna mtu mtu atakua ame hack acount ya getamycin mana hii sio yeye , with all due respect GETA wew ni legend hum so hiz mada za kigrobal news tuachie sisi amature.
 

fasiliteta

JF-Expert Member
Jul 2, 2014
1,383
2,000
Wakili msomi kaeleza kweli lakini Mkuu,hua una madharau na utoto mwingi lakini
Achana naye huyo Mpuuzi Mkuu tayari nimeshampa ' dozi ' yaka na nadhani sasa anaisoma na pengine inaweza ikambadilisha Kifikra, Kimawazo na hata Kiupeo. Anadhani Watu humu huwa tunakurupuka tu wakati kumbe tunajua tunalolifanya.
msomi ka
 

Ngai Moko

JF-Expert Member
Mar 21, 2016
877
1,000
Kwa utangazaji ule huwa napata wasiwasi sana yaani inaonesha ni jinsi gani alivyo rojorojo katika matamshi, Kotinyo Nicasius wa sasa sio yule wa mwanzon
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom