Huyu Mtangazaji wa michezo wa Clouds tv na fm huku kuongea kwa kubana pua ni maumbile au mapozi tu?

Kama unamuheshimu huyu bwege basi na mimi heshima yangu kwako nitaitoa. Huyu nilimuweka ignore list kitambo sana. Utoto mwingi akidhani anapamba kumbe anajibamba

Hivi Mtu unayemuweka katika Ignore List bado unaweza tena kupoteza muda wako Kumfuatilia au Kuzifuatilia threads na posts zake?
 
Katika kuwagentaminized hao usimsahau na yule mtangazaji wa Ea radio kwenye kipind cha michezo hajui wapi ikae herufi L na wapi ikae herufi R, na mbaya zaid hadi kwenye lugha ya mkoloni anachanganya hizo herufi, ni kichefuchefu aisee

Nitawaweka tu sawa Mkuu wote wala usijali. Kesho Mwenyezi Mungu akipenda nimeahidi nitamuanika Mtangazaji mmoja hivi tena wa Kike wa Radio One na ITV. Hana matatizo mengi kivile ila kikubwa nitamchambua tu ' Kitaalam ' na kumshauri asiwe anatangaza Taarifa za Habari za ITV bali abakie tu sana katika Redio kwani huko ndiko kunampendeza na ni imani yangu kubwa sana kuwa atausikiliza ushauri wangu kama ambavyo Wenzake wengi niliokwishawaanika humu wamenisikiliza na kubadilika.
 
mimi mwenyewe nilishagajiuliza sanaa, huyu jamaa anakisauti kinaboa sanaaaaaaa, halafu kiufupi clouds kipindi cha michezo hakuna lolote , kinachonifurahisha mimi ni kimoja tu, ngumu kumeza basi
 
Ni Nicatius Agwanda a.k.a yake anajiita Coutinho ( Kotinyo )

Anatupa sana tabu Sisi tuliozaliwa na kukulia hasa hii Mikoa ya Pwani ya Bahari ya Hindi.

Nawasilisha.
Wewe jamaa unapenda sana kuwachunguza wanaume ni jinsia gani?
 
Ewe Mtangazaji Nicatius Agwanda a.k.a Coutinho ( Kotinyo ) akhsante sana kwa kuweza kubadilika kwani baada ya kukusema katika uzi huu nimekusikiliza katika Kipindi chenu cha Michezo cha Clouds fm kilichomaliza hivi punde tu na umejirekebisha kwani muda wote uliokuwa unaongea umekuwa ukikaza Sauti yako vyema na Kuongea Kiume na si kama vile ambayo nimeukuzoe ukibana pua na kama nilivyokuona pia leo asubuhi ukiwa katika 360 Clouds tv ambapo kama kawaida yako ulitubania tena pua yako.

Safi sana Kijana na huyu ndiyo GENTAMYCINE Mzee wa Kurekebisha. Kesho tena namuanzishia Uzi Mtangazaji mmoja wa Redio One na ITV ambapo nitamshauri tu aachane na Kutangaza katika Runinga ( Television ) hasa Taarifa ya Habari ( News Bulletin ) na badala yake abakie tu katika Redio kwakuwa anafanya mno makosa ya Kitaaluma na Kiuweledi na nimemchunguza kwa muda mrefu nikidhani atabadilika ila nimegundua ndivyo alivyo.

Mliokuwa na mnaonidhihaki endeleeni hivyo hivyo ila nashukuru wote ninaowasema ( Watangazaji ) wanabadilika na kwa mliokisikiliza Kipindi cha Michezo cha Clouds fm cha leo ( usiku huu ) na kumsikiliza vizuri huyu Kijana nadhani nanyi mmemsikia jinsi alivyobadilika.

Akhsante Mwenyezi Mungu.
We kijana unapenda sifa za kijinga, sasa kotinyo kabadilika nini sasa mbona kaongea vilevile halafu unakimbilia huku kuja kujisifia ujinga......
 
Wewe mkimbizi uwe unapumzika. Mimi si wa kupiga porojo na kuanzisha vimada vya kitoto kama vyako ili nipate wachangiaji. HAPA KAZI TU!
watanzania watu wazuri ila munaubaguzi saana kwa watu tusokua na asili ya kitanzania izo habar za ukimbizi vip tena!!?acheni hivo sio poa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom