Huyu mpenzi wangu anafaa kuwa mke?

Huyu mpenzi wangu anafaa kuwa mke?

authentic05

Member
Joined
Aug 15, 2016
Posts
89
Reaction score
83
Habari za wakati wana jf.
Naomba ushauri wenu tafadhari.

Mimi ni kijana wa miaka 28, kwa sasa ninaishi dar, elimu yangu ni chuo kikuu, Nina kazi na kipato changu ni cha wastani.

Katika maisha yangu, nilimpenda msichana mmoja wakati nipo kidato cha tano,
Yeye wakati huo alikuwa kidato cha nne,
Kwa ufupi, ni msichana mweupe, msafi, mrefu wa wastani , ana staha, ni mzuri, ana shape nzuri kiasi kwamba wanaume wengi huvutiwa kuwa nae.
Ni msichana ambaye tumetoka kijiji kimoja, kwa umri nimemzidi mwaka mmoja, amemaliza chuo mwaka huu maana alisoma diploma kwanza, (another story though..)

nilianza kumtaka kimapenzi huyu binti tangu wakati huo, Mimi nilikuwa nasoma shule ya Wavulana na yeye alikuwa shule ya mchanganyiko..
Nilitamani sana kuwa nae, kuna wakati alinikubali, lakini haikudumu kwa muda aliniambia haoni nafasi yangu moyoni mwake,
Nilijitahidi sana kuubadilisha moyo wake, nilijitoa kwake Mara nyingi na kwa mengi sana, lakini haikufaa, japo alikuwa akinifariji kuwa kama imepangwa awe wangu atakuwa tu..
Ni Mara mbili alinikubalia na mwenyewe akaniacha
Wakati huo Mimi pia nilibahatika kupendwa na wasichana wengine, nikatoka nao japo bado sikuamini kama naweza kuishi bila yeye.
Na pia yeye kuna wakati nilishuhudia akiwa na mahusiano na vijana wengine , iliniuma kweli na nilipojaribu kuachana nae haikuwa rahisi kabisa kwangu.
Nilipokuwa chuo nilikuwa namtembelea Mara kwa Mara(tulikuwa vuo tofauti vilivyopo mji mmoja) , japo yeye kunitembelea ilikuwa hadi nimlazimishe, au awe na shida binafsi.
Baada ya Kumaliza chuo niliondoka nikamuacha yeye bado yupo chuo na kwa hapo mawasiliano baina yetu yalififia,
Japo sikumsahau ila nilijisemea moyoni kuwa sio lazima niwe na yeye maana huku mtaani wanawake ni wengi sana na wengine wananitaka tena kwa kunitongoza.
Nilijichanganya na wanawake wengine japo nilijitahidi kuwa makini kulinda Afya na heshima yangu kwa ujumla.

Baada ya siku na miaka kadhaa kuenda hatimaye nilipata binti mwingine aliyenipenda sana, kuna wakati alikuwa hadi ananikera, maana haishi kunisumbua kwa simu na meseji hata nikiwa kazini au kanisani..
Kwakweli nilijiaminisha kuwa huyu ndiye niweke malengo nae, kwa pamoja tulifurahia sana mahusiano yetu..

Lakini wakati wote huo sikuweza kumsahau X wangu pamoja na kuwa na huyu binti mpya.
Ilikuwa tunakumbukana japo Mara moja kwa mwezi.

Sasa ilifika wakati huyu X niliyemtafuta kwa miaka bila success akaniuliza kama bado nampenda;
Kwakweli nilifikiria sana ila nikaja na jibu moja kuwa 'NDIO' (stupid udhaifu wa wanaume tulio wengi)
Akanitumia picha moja tuliyopiga pamoja zamani sana akaniambia niiweke profile ya Whatsap..
Ilikuwa ni vigumu sana, lakini nikajikuta nimeiweka. (Mpenz niliekuwanae hakuwa Whatsap) kwaiyo hapo miundombinu haikuwa migumu kwa upande wa pili.

baada ya kuona maswali na majibu yanachukua umaarufu katika conversations na ma-ex na marafiki na ndugu na jamaa, niliamua kuitoa ile picha..
Huku nikiamini nimemridhisha huyu mwanamke.,

Siku kadhaa baadae aliniambia anataka kuja dar kutafuta laptop hivyo angependa afikie kwangu na akataka nimjibu kama hilo linawezekana..
Hahahahaha..
Kwakweli lilikuwa ni swali rahisi sana zaidi ya swali la factors for rise and fall of mali empire kwenye history au lile swali la kuprove kama acceleration due to gravity = 9.8ms-1 kwenye simple harmonic motion..)
Ili kuhakikisha habadilishi mpango wake nilimwambia anitumie hiyo budget ya PC nimtafutie mwenyewe ili akija asipate shida ya kwenda kariakoo au mlimani city kabisa,

Kwakuwa binti ananiamini katika mambo mengi ya maisha alinitumia ile pesa huku nikimkoleza kwa kumuahidi kumtafutia PC adhimu..hatimae kama ndoto hivi nilimpokea binti ubungo, nikaenda nae hadi geto kwangu sinza,
Nilikaa nae kwa siku 4 ndani, yaani siku zote hizo ilikuwa ni kama ndoto kwangu aisee, nilimtafuna mtoto wa watu hadi akawa anashindwa kufumbua macho,
Yaani nilienjoy hatari, sikuwahi enjoy sex kiasi kile.
Wakati mahaba yamenoga, nikaamua kumwambia kuwa Nina mpenzi mwingine na ananitegemea na kuniamini sana,
Hakuonesha kustuka,
Akafikiria kwa muda, akaangalia picha ya mpenz wangu, akaonekana kumhurumia, akaniambia niendelee nae tu nisimuache maana yeye hawezi kuolewa na Mimi maana umri wetu ni tumekaribiana sana na amenipa penzi lake kama shukrani ya kumpenda na kumjali kwa miaka mingi.
Moyoni sikuridhika na hayo majibu yake mepesi kabisa maana aliniambia hana mtu na yupo absolutely single at the moment. (Just like a free radical)
Baada ya Siku 4 za uvunjifu wa amri ya sita nikamkatia tiketi akarudi chuo.
Baada ya hapo mawasiliano kati yetu yalishika kasi huku mwenyewe nikianza mchakato wa kuachana na huyu binti mwingine taratibu , nilitaka nimuache kwa njia nzuri ili nisimuumize kwa kuwa umri wake ulikuwa ni mdogo .

Baadae nilifanikiwa kumuacha mpenz niliekuwa nae, nikawa na huyu kwa 100% na nikaacha kila aina ya mchepuko.
Hadi sasa nipo nae yeye tu na huwa anakuja kwangu na kukaa kwa Uhuru na kuondoka Mara kwa mara, ameshahamishia nguo na baadhi ya vitu vyake kwangu.

Tatizo ni Hili,
Amekuwa na watu kadhaa kabla yangu ,
Ingawa hilo sio tatizo sana,
Kuna wakati nimemuona akichati na mwanaume mwingine wakisifiana sana na anaenda mbali zaidi akidai bado anamkumbuka sana , nilipomuuliza akaniambia huyo ndiye alikuwa boyfriend wake wa kwanza,
OMG, nikikereheka na nikampa adhabu Kali ya kisaikolojia iliyomfanya alie mbele yangu hadi nikajikuta nimemsamehe..

Tatizo lingine huyu mwanamke,
she isn't proud of me yet, hanitambulishi kwa rafiki zake freely kama mimi ninavyomtambulisha yeye,
na huwa haoneshi kuumia, hata nikimwambia Leo tuachane yupo tayari..
Nilijaribu kuzungumza nae kuhusu hili akaniambia niwe huru tu kutafuta mwanamke mwingine ikiwa naona yeye hanifai,
Je ni kweli wanawake humuacha mwanaume kirahisi hivyo?

Mara zote ananiambia ananipenda sana but hana wivu na Mimi kabisa,
Ikiwa anawafahamu baadhi ya wasichana na ma -ex wangu wanaonitaka, mmoja tupo nae group moja la Whatsap na huwa haipiti siku asinikumbuke kwa msg za mahaba , na yeye anaona hayo yote maana pia ni mamber ,ila hata haoneshi kujali..
Nimelileta hili humu jf ikiwa tunafikiria kuanza hatua za awali za ndoa mwakani Mungu akipenda.,

Naombeni ushauri wenu wapendwa, nikiwa nafahamu ni bora zaidi kuumia kwa kumpoteza mchumba kuliko kuumia katika ndoa .
Nina nafasi ya kubadilisha maamuzi for betterment of my future.
Je , Huyu mwanamke ananifaa?
 
Kwanini usirudi chuo ukasome tena?...Naona umesoma chuo but hujaelimika kabisa kiasi cha kushindwa kutumia hesabu nyepesi kama za kutafuta namba inayofuata?...

Sioni ushauri wowote unaohitaji kwetu ila tambua hili..."Sio kila mwanamke ameumbwa kuwa mke wa ndoa...Wengine wameumbwa kuwasaidia wenzao walio kwenye ndoa.....Michepukoooooooo"

Yuleeee girlfriend uliyemuacha ndio "Mke wa ndoa " na huyu mtu mzima uliyenaye ndio "Mchevukooooooo"....Umeelewa wewe mtoto wa shule?...Miaka 28 unaoa unawahi nini?.....Videmu vyemnyewe ulivyoisha gonga hujazi hata basi moja la mwendo kasi...Kiherehere chako kuwahi ndoani wakati shughuli za ujana hujamaliza...Mwishowe uwasababishie watu wakose appetite ya ndoa kwa kukutazama wewe utavyokuwa unazagaa na malaya mitaani wakati una mkeo mzuri na watoto nyumbani....

By the way unaoa ushajenga?....Au unataka kuwatesa wakwe wakija kukusalimia dar uwalaze sebuleni kwenye makochi na madumu ya maji uliyojaza ndani mwako?

Elimu....Elimu....Elimuuuuu.
 
Hapana mkuu, huyo ni Mimi na hiyo ni habari ya maisha yangu..

KUBALI NI HADITHI TUKUSAIDIE JINSI YA KUTUNGA HADITHI ZENYE KUVUTIA NA KUUZA SOKO LA MAGAZETI YA UDAKU NA UMBEA KAMA KWA SHIGONGO....dogo janjaroooooo. KASOME CHUO BANA
 
KWANINI USIRUDI CHUO UKASOME TENA?...NAONA UMESOMA CHUO BUT HUJAELIMIKA KABISA KIASI CHA KUSHINDWA KUTUMIA HESABU NYEPESI KAMA ZA KUTAFUTA NAMBA INAYOFUATA?...

SIONI USHAURI WOWOTE UNAOHITAJI KWETU ILA TAMBUA HILI..."SIO KILA MWANAMKE AMEUMBWA KUWA MKE WA NDOA...WENGINE WAMEUMBWA KUWASAIDIA WENZAO WALIO KWENYE NDOA.....michepukoooooooo"

YULEEEE GIRLFRIEND ULIYEMUACHA NDIO "MKE WA NDOA " NA HUYU MTU MZIMA ULIYENAYE NDIO "MCHEVUKOOOOOOO"....UMEELEWA WEWE MTOTO WA SHULE?...miaka 28 unaoa unawahi nini?.....videmu vyemnyewe ulivyoisha gonga hujazi hata basi moja la mwendo kasi...kiherehere chako kuwahi ndoani wakati shughuli za ujana hujamaliza...MWISHOWE UWASABABISHIE WATU WAKOSE APPETITE YA NDOA KWA KUKUTAZAMA WEWE UTAVYOKUWA UNAZAGAA NA MALAYA MITAANI WAKATI UNA MKEO MZURI NA WATOTO NYUMBANI....

BY THE WAY UNAOA USHAJENGA?....AU UNATAKA KUWATESA WAKWE WAKIJA KUKUSALIMIA DAR UWALAZE SEBULENI KWENYE MAKOCHI NA MADUMU YA MAJI ULIYOJAZA NDANI MWAKO?

ELIMU....ELIMU....ELIMUUUUU.
Hahahaha.. Duh, mkuu taratibu aisee, I agree with you kwa baadhi ya mambo anyway.
Nashukuru kwa ushauri.
 
KUBALI NI HADITHI TUKUSAIDIE JINSI YA KUTUNGA HADITHI ZENYE KUVUTIA NA KUUZA SOKO LA MAGAZETI YA UDAKU NA UMBEA KAMA KWA SHIGONGO....dogo janjaroooooo. KASOME CHUO BANA
Sipo huko bwana, na masuala ya uandishi si fani ya kila mtu,
Wengine tunajali kufikisha ujumbe tu,
Kama umenielewa you are free to advise, but usitumie hisia zako binafsi kufanya justification ya usiyoyajua.
Thanks pia.
 
[QUOTE="Who Cares?, post: 17236924, member: 11290" "Sio kila mwanamke ameumbwa kuwa mke wa ndoa...Wengine wameumbwa kuwasaidia wenzao walio kwenye ndoa.....Michepukoooooooo"




Jamii forum raha sanaaaaa
 
Mwe kuna watu mapenzi yana wanyanyasa, uvumilivu ulionao unahitaji nishani ya kimataifa, na kujitunza kwako miaka yote siku ulipozawadiwa hukukumbuka angaza. Mkuu, hata kama huelewi thamani ya maisha yako, wazazi na ndugu zako wanailewa.
 
Kwanini usirudi chuo ukasome tena?...Naona umesoma chuo but hujaelimika kabisa kiasi cha kushindwa kutumia hesabu nyepesi kama za kutafuta namba inayofuata?...

Sioni ushauri wowote unaohitaji kwetu ila tambua hili..."Sio kila mwanamke ameumbwa kuwa mke wa ndoa...Wengine wameumbwa kuwasaidia wenzao walio kwenye ndoa.....Michepukoooooooo"

Yuleeee girlfriend uliyemuacha ndio "Mke wa ndoa " na huyu mtu mzima uliyenaye ndio "Mchevukooooooo"....Umeelewa wewe mtoto wa shule?...Miaka 28 unaoa unawahi nini?.....Videmu vyemnyewe ulivyoisha gonga hujazi hata basi moja la mwendo kasi...Kiherehere chako kuwahi ndoani wakati shughuli za ujana hujamaliza...Mwishowe uwasababishie watu wakose appetite ya ndoa kwa kukutazama wewe utavyokuwa unazagaa na malaya mitaani wakati una mkeo mzuri na watoto nyumbani....

By the way unaoa ushajenga?....Au unataka kuwatesa wakwe wakija kukusalimia dar uwalaze sebuleni kwenye makochi na madumu ya maji uliyojaza ndani mwako?

Elimu....Elimu....Elimuuuuu.
Hahahah..

Na Mie bado kama siti nne nijaze basi la mwendo Kasi mkuu,dah nimecheka sana
 
Mwe kuna watu mapenzi yana wanyanyasa, uvumilivu ulionao unahitaji nishani ya kimataifa, na kujitunza kwako miaka yote siku ulipozawadiwa hukukumbuka angaza. Mkuu, hata kama huelewi thamani ya maisha yako, wazazi na ndugu zako wanailewa.
Hahahaha, hapana madam, nipo makini katika hilo.
Nashukuru nimekuelewa anyway.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom