Technologiest
JF-Expert Member
- Feb 8, 2017
- 3,712
- 4,026
Habari za blue Monday wanajamvi!
Naenda kwenye mada, nikiwa kama mwanafunzi wa kawaida kabisa katika shule yetu iliyopo huku kijijini nashangazwa sana na huyu kiongozi wetu wa shule; amekua sio mtu wa kuwaacha aliowagawia madaraka watekeleze wajibu wao kama ilivyo kwa shule nyingine nilizowahi kusoma kwakua hapa nimehamia kutoka shule nyingine.
Kiukweli nakuta kama mkuu wa shule hii anatufanya tumzoee mno kiasi kwamba tunakua hatuna hamu nae ya kuweka umakini mkubwa siku akitaka kuzungumza ili tutake kujua ana mpya gani leo! Binafsi sioni kama ni sahihi kwake kufanya hivo,tunatakiwa tummic bhana sasa wanafunzi wakipiga kelele anakuja kutuliza yeye, vitabu vipya vikiletwa anaenda kupokea yeye,wachelewaji anakamata yeye na adhabu zote anataka atoe yeye jamaniii...
Naombeni kuuliza labda nawaza vibaya,au huu ndo uwajibikaji unaotakiwa? Nadhani tunamzoea mno kiasi kwamba akitaka kutupa ujumbe hata kama ni muhimu tutachukulia poa tu na kumwona wa kawaida sana.
Nakumbuka baadhi ya shule nilizowahi kusoma mkuu wa shule kumwona ni nadra,kwanza sijui uwe na ishu nzito kiasi gani mpaka ufike kwake yaani inamaana hawa wengine wote wameshindwa kutekeleza ni ngumu mno! Hadi inapofikia siku anataka kuongea wanafunzi wote tulikua tunaweka attention kubwa kutaka kujua leo kuna jambo gani zito.
Daaah! Naomba niishie hapa,natamani kama ujumbe wangu ungemfikia walau awe anajichimbia kidogo awaache walimu wengine wawajibike yeye awafuatilie kwa karibu hao na kwetu aje baada ya muda fulani walau tupate kamuda kakummic.
Wasaalam,
Mhembejr.