Huyu mganga wa kienyeji amenipa masharti magumu sana kuyatekeleza

Hivi punde

JF-Expert Member
Apr 1, 2017
2,554
8,581
Salaam wanaJF.

Ugumu wa maisha hupelekea kufanya kila linalowezekana (ukiacha kuua) ili mkono uingie kinywani. Na sasa kuna hawa wataalamu wetu a.k.a waganga wa kienyeji ambao wao wamejaaliwa katika kufanya sayansi ya asili ,sayansi ya kumsaidia mtu utajili ilihali wao wakiwa na maisha magumu, maisha ya kukaa machakani au mapangoni.

Katika pitapita yangu Wilayani Lushoto Mkoani Tanga, nikafika kijiji fulani kinaitwa Soni.Hapa kuna mganga wa kienyeji matata sana.Jamaa yangu mmoja akashauri tumwone bwana huyu ili tujue kama kuna fursa toka kwake.Basi asubuhi na mapema ya May 19, 2017 tukajongea kwake porini.

Agenda yangu kichwani ikawa ni kupata mapesa mengi ghafla bila kuvuja jasho au kuua binadamu. Tukakubaliana "Terms and conditions". Masharti aliyonipatia ni kama yafuatayo:-

1. Nikitaka kulala, nilale nikiwa nimekaa, kwa miezi 6 mfululizo.

2. Nguo ya ndani (chupi) niliyokuwa nayo ndo niitumie hiyohiyo na haitakiwi ifuliwe kwa miezi 6 mfululizo

3. Popote ninapopishana na mtu, nipite upande wa kushoto kwa miezi 6.

4. Nisifanye mapenzi, kunywa beer wala kuvuta sigara kwa miezi 6.

5. Kila wiki niwe namtumia elfu 20 kwa mpesa

6. Sitakiwi kumwambia mtu siri zote physically.

Ndo haya tu masharti yake.Chaa

Nimejaribu kuyatekeleza ndani ya siku 2 toka aliponoambia, nimeshindwa kabisa. Yaani ni kama aliwasiliana na watu wangu tunaokunywaga nao pombe na kwenda club.Wananipigia simu nijoin toka ile siku amenipa hayo masharti.

Inakuwaje waganga wa kienyeji wanakuwa na masharti magumu sana ile hali wakijua hayatekelezeki? Mbona wao pia wana maisha mbuzi tu?

Karibuni
 
Achana na madhabahu ya kuzimu ndugu, hiyo sadaka unayotuma inakuunganisha na roho za kuzimu.
 
  • Thanks
Reactions: PNC
Utateseka sana kwa muda mrefu haswa na mwishowe utajikuta umetumia nguvu nyingi kuliko ambavyo ungefanya kazi kumtegemea Bwana Yesu.

Mrudie Kristo, jenga tabia ya kutoa 10% ya unachopata kama sadaka, na hakika Mungu atakujazia bila masharti yoyote
 
  • Thanks
Reactions: PNC
Yaani Mkuu una hela na kundi la watu mnakunywa bia halafu unasema maisha magumu? Na siye wa "leo afadhali ya jana" tusemeje?. Waganga wana akili sana ndo maana kasema uwe unamtunia pesa kila mwezi. Ungekuwa kapuku angesema kakamate kuku wako mweusi umletee amle maana angejuwa huna hela.
Hayo ndiyo maajabu ya watanzania
 
Muongezee dau kila wiki mtumie zaidi atalegeza masharti Kiongozi.
 
Back
Top Bottom