greater G
JF-Expert Member
- Nov 12, 2016
- 308
- 215
Mwaka juzi katikati nilianza mawasiliano na dada mmoja. dada huyu ambaye ni mwajiriwa Serikalini mara baada ya kuonana Dar akitokea kwake tulikubaliana kuanza mahusiano baada ya kuafikiana.
Urafiki wetu na huyo dada uliosababisha tufahamiane ulichagizwa na rafiki yangu mmoja anayetoka mitaa ya huko aliyenipatia namba zake huku akimsifia kuwa ananifaa,nami bila ajizi nikaanza kumwaga Sera zangu kwake na Mungu si Athumani tukaafikiana.
Baada ya muda nilimtumia nauli akaja hapa Dar ambapo tulionana kwa mara ya kwanza na kupanga mipango yetu kisha nikamuwezesha tena nauli ya kurudi kwao.
Miezi michache alikuja tena Dar tukapiga show kadhaa za kula tunda na baada ya siku chache akarejea kwao akiwa ameburudika sana tu.
Sasa siku baada ya siku mawasiliano yalianza kushuka baada ya yeye kutaka tukafunge ndoa kwao haraka sana kitu ambacho mimi sikukiafiki kwani nilitaka nimsome zaidi.
Baada ya muda kupita akanijulisha amepata bwana mwingine na sasa anaujauzito, ila kwa kuwa mimi nilimpenda Daaah! Aisee niliumia sana.
Siku hazigandi bana! Kutokana na ukweli huo kuwa nilikuwa nampenda niliendelea kumsalimia tu huku akiniomba nisimvunjie ndoa yake japo alidai atanirudishia pesa zangu.
Baada ya hapo akiwa ni mjamzito akikaribia kujifungua mtoto alifia tumboni kutokana na tatizo alilokuwa nalo ambalo tangu awali nilimwambia atibiwe.
Dada huyo anasema jamaa baada ya kumtia mimba kulianza kutokea kutoelewana kati yao hadi mapenzi yao kufa.
Sasa anadai turudiane, hivi huyu anafaa kweli kuwa mke?