Huyu mchumba vipi?

Mchumba wangu wa kike anauza duka maeneo flani hapa mjini.
Ni wiki mbili tu tangu nilipomtambulisha kwa wazazi.
Jana saa saba na dakika 10 mchana nikamtumia meseji ya kawaida, hakujibu.

Ilipofika saa saba na dakika 33 nikawa na wasi wasi ikabidi nimpigie simu.
Nikapiga mara ya kwanza kimya. Nikatulia dakika 3 zikapita nikapiga tena kimya.

Baada ya dakika kama 5 akanipigia. Kwa hasira sikupokea simu. Akatuma meseji eti sory mpenzi nilienda kununua chakula.
Mmh sikuridhika na sababu yake hiyo maana sikutegemea kama ataacha duka aende kununua chakula zaidi ya dakika 20.
Akaendelea kunitext na kupiga nikakaa kimya. Usiku ikabidi nipokee simu yake, tuliiashia kulaumiana bila muafaka.

Hadi muda huu napoandika hajanitumia SMS wala kupiga tangu jana usiku. Na mimi nimeamua kukaa kimya.

Sasa najiuliza, huyu mchumba vipi? Anafaa kweli? Na nshamtambulisha sasa. Najiuliza nimchukulie hatua gani bila majibu.

haupo tayari kwa ndoa wewe....still need some growing up.
 
we jamaa naona una hamu ya kufungua thread tuu,,,,,
kama uko serious, honestly... You are Pathetic!! and i wish she leaves yo stupid ass...
 
Kwanza mkuu unaonekana bado una akili ya kitoto, kila walio kwenye mahusiano wangekuwa wanasusiana kama ulivuofanya ww bac ndoa zisingekuwepo. Unapaswa kuwa na utulivu wa akili, muelewa, mvumilivu, mwenye kusamehe na mwenye kujenga hoja sio kukurupuka tu eti hajapokea simu. Sasa hapo kwa mawaz yako yalivyo finyu unahisi alikuwa na mwanaume mwingine? Be matured bhana
 
Mimi ni Me mkuu
Kwanza kabisa mkuu punguza wivu,pia usimuhukum mtu kwa jambo ambalo halina ushahidi,Anza kumchunguza kwa taratibu nyendo zake jifanye mjinga kwa mda utamkamata tu,ndipo utachukua hatua mwisho kabisa kama ulikua na nia ya kumuoa hivi karibun ongeza miezi.halafu kuhusu mawasiliano mpe mda jifanye kumpigia hata kutwa 3 mda mwingne potezea uone kama nae anakukumbuka,
 
Asante mkuu. Nitafanyia kazi ushauri wako
 
Pole baba yeyoo, mama yeyoo anahitaji muda wa kufanya mambo yake sio customer care wa emergency hata awe pembeni ya simu Kila sekunde.
 
Mchumba wangu wa kike anauza duka maeneo flani hapa mjini.
Ni wiki mbili tu tangu nilipomtambulisha kwa wazazi.
Jana saa saba na dakika 10 mchana nikamtumia meseji ya kawaida, hakujibu.

Ilipofika saa saba na dakika 33 nikawa na wasi wasi ikabidi nimpigie simu.
Nikapiga mara ya kwanza kimya. Nikatulia dakika 3 zikapita nikapiga tena kimya.

Baada ya dakika kama 5 akanipigia. Kwa hasira sikupokea simu. Akatuma meseji eti sory mpenzi nilienda kununua chakula.
Mmh sikuridhika na sababu yake hiyo maana sikutegemea kama ataacha duka aende kununua chakula zaidi ya dakika 20.
Akaendelea kunitext na kupiga nikakaa kimya. Usiku ikabidi nipokee simu yake, tuliiashia kulaumiana bila muafaka.

Hadi muda huu napoandika hajanitumia SMS wala kupiga tangu jana usiku. Na mimi nimeamua kukaa kimya.

Sasa najiuliza, huyu mchumba vipi? Anafaa kweli? Na nshamtambulisha sasa. Najiuliza nimchukulie hatua gani bila majibu.
Tatizo lako una hasira za papo kwa hapo, usitoe hukumu bila ya uchunguzi mkuu
 
"Love is The Seventh Sense , Which Destroys All other 6 Senses leading to creation of eighth sense called NON SENSE.
 
Mbona tabia zako sio za kiume!!!!!!?

Huyo mwanamke ulitongozewa na nani?!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom