Huyu mbona simuelewi!!

M.E.M.A

JF-Expert Member
Joined
Jul 27, 2013
Posts
1,373
Reaction score
472
Habari za wakati huu wana MMU.

Kuna bibie mmoja nilimtokea kama wiki mbili hivi zilizopita. Kwa kweli ni mzuri sana..wa umbo (mengineyo sijui). Nilitaka kuona kama lile jini MAKATALIWA bado linanisumbua. Bahati nzuri akakubali...(nilishangilia sana moyoni).

Tatizo na habari iliyonileta hapa ni kwamba simuelewi. Nikimuita tupange mambo yetu anakuja ndani ya dakika mbili anasema anawahi nyumbani kupika (nimechunguza sio house girl). Nyumbani kwangu ameshafika mara mbili. Angalau weekend hii alikaa kwa lisaa limoja na hata kuondoka kwake ilikuwa hoja ile ile (nawahi kupika). Nikimpigia simu na kumbusu zile za kisimu simu harudishi..anasema kuna watu. Ukimtumia ujumbe wa maneno anajibu short short tu (k, poa, sawa, asante, hahaha)... basi nikaona isiwe tabu na mimi niache kujifanya nilielewa sana somo la kutunga sentensi, na mimi nikaanza kujibu hivyo hivyo...tena nikayafupisha zaidi (k, asnt, mh,). Baada ya hayo kaanza kunilalamikia simjali, namjibu kifupi kifupi kama vile sitaki, simbusu kwenye simu...😕

Kwa kweli sielewi nifanyeje. Na sio mtoto huyu miaka 25 sasa.
 
kizur ni kile apendacho mwenziwako ila nawewe mwambie aache kujibu kufupi kuhusu kula mzigo naona huna tekinik za kuomba
 
Mwambie unampenda sana na endeleza libeneke lile la kufupisha maneno,tena wakati mwingine usiwe unamjibu,ukionyesha ume mfeel sana atakupeleka puta vibaya sana,take care,Tena almost muda mwingi jifanye uko bize na maisha,hatakusumbua kama unavyodhani.
 
Yani usiruhusu mtu akupelekeshe,ukiona mtu unampa attention kubwa af yeye anakupotezea,vumilia af endelea kujfanya unajpendekeza...,af gafla acha kumtext,kama umezoea kumpgia acha,text akikutumia tano jbu moja tena baada ya lisaa limoja...wee ona atakavyojileta mwenyewe!
Hiyo ndo dawa usiruhusu mtu acheze na akil yako
 
Bint ankpnd ila analeta mbwe mbwe that y analalamika bt mwambie ajilekebishe
 
Kama anakusumbua si achana nae, au mpaka kieleweke ndio itakua basi?
 
Pamoja na yooooote ulosema hapo haiondoi ukwlei kuwa mnapenda, tafuta njia nzuri ya kuwekana sana sasa na ww km utaanza kumjibu shotcut mwisho wake nini?? faida gani utapata, kwenye mapenzi jihadharini na jeuri, kiburi n.k
 
Hahahahaaa!
Ukiskia penzi la uchoyo ndio kama hilo!!!!
Generaly inawezekana watu kupendana kwa asilimia 100, but haiwezekani kuoneshana upendo kwa asilimia 100!!!
...Mh! Juzi nimeona msemo m1 ktk siredi ya Hmdn, unasema hivi:
'Mwanke ni kama kivuli, ukikikimbia kinakufata na ukikifata kinakukimbia!!!
...
Ili umech na huyo ke, na wewe kuwa mchoyo!!! Yap! Akitext 'thnx' wewe 'tx'!!!!!!
 
ila usikariri saaana wakati mwingine inaweza kukuumiza wewe
 
Bado nashindwa kuelewa vijana wa siku hizi, mwanaume wa miaka ishirini na ushee bado anakuwa na akili kama za mvulana ambaye ndio kwanza kabalehe.
 


Hii imekaa vizuri kweli. Ndio mkakati niliouanza hivi sasa. Nimeweza kuacha kupokea simu tano alizopiga leo. Na jana kaniuliza mbona simbusu..namimi nikajibu "hapa kuna watu"
 
Bint ankpnd ila analeta mbwe mbwe that y analalamika bt mwambie ajilekebishe

Pamoja na yooooote ulosema hapo haiondoi ukwlei kuwa mnapenda, tafuta njia nzuri ya kuwekana sana sasa na ww km utaanza kumjibu shotcut mwisho wake nini?? faida gani utapata, kwenye mapenzi jihadharini na jeuri, kiburi n.k

Inawezekana ananipenda kweli. Jana kaniletea nyanya za kutosha bajeti ya nusu mwezi..
 

Mkuu hili nalo neno. Huo mkakati wa uchoyo unaendelea hivi sasa. Msg yenye kurasa tatu yaani character 480 mimi najibu 'ok'
 

Hayatuhusus. This is your private business.
 
mkuu fisi hashindwi mfupa we ww mjibu vzuri ila ukisharamba sukari we sepa
 
Hii imekaa vizuri kweli. Ndio mkakati niliouanza hivi sasa. Nimeweza kuacha kupokea simu tano alizopiga leo. Na jana kaniuliza mbona simbusu..namimi nikajibu "hapa kuna watu"

Then umefaidika nini? After all wewe ndo mwenye shida then unajifafanya jeuri kiburi, grow up bhana men are not like that
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…