Wadau,
Mwezi wa Februari nikiwa naendesha pikipiki nilikatiza uchochoro kwa kasi ya about 80KMP, kufumba na kufumbua kundi la kuku na wanae walikatiza mbele yangu, nilipiga breki kali huku naserereka kuwakwepa. Pikipiki ilinishinda na kunitupa kichakani. Thanks God kuku niliwakwepa ila niliumia miguuni na pikipiki iliharibika kiasi.
Bibi anatokea
Nikiwa najizoa zoa, mara alitokea bibi nyumba ya jirani akaja kuniinua huku akinishukuru kwa lugha nisiyoijua kwa kuokoa kuku wake. Nilijikaza na kuinua pikipiki mara yule bibi aliniletea kuku mdogo mweusi. Nilikataa ila aliinsist na nikamfunga kwa pikipiki, nikawasha nikaondoka japo pikipiki ilikuwa vibaya.
Maajabu yaanza
Yule kuku alikua na alitaga mayai 31, na akayatotoa yote. Baada ya kuwaacha watoto wajitegemee (walikua wote) akataga tena safari hii mayai 41 na katotoa yote....
Sasa najiwaza, huyu kuku ni wa aina gani? Je, next atataga mayai 51?Naogopa kula products zake wala kuuza. Now nina kuku 73, na nawaogopa japo nawatunza vyema.