Huyu kiongozi wa mwendokasi anastahili kubaki ofisini? Analalamika abiria kuongezeka badala ya kuona kama fursa. Watumishi wa umma duu

Resilience

JF-Expert Member
Jan 4, 2023
877
4,106
Uongozi wa mwendokasi umekiri kwamba wameshindwa kuendesha miradi husika na hivyo wanasubiri hadi serikali inunue mfumo wa Artificial Intelligence wakuongoza magari. Hayo yamesemwa leo katika mahojiano baina ya waandishi wa habari na viongozi wa mradi husika.

Baada ya viongozi hawa kusema wamekwama, nimejaribu kuangalia umri wa kiongozi huyu, uwezo wake wa kuchakata issue nikabaini tuna watu wasio sahihi kwenye miradi yetu.

Kibiashara kuongezeka kwa abiria ni opportunity lakini kwa huyu kiongozi anatamani abiria wapungue. Kama huyu mtu yupo ofisini na analipwa salary tunategemea miradi hii iwe na ufanisi?
 
Ukipita kwenye vituo vyao vikubwa mabasi hayo yapo kibao yamepark kwa ubovu. Nashangaa wanasubiri nini kuyatengeneza, ndiomana wamezidiwa na idadi ya watu. Sikuizi kupanda mwendokasi unakuwa kama upo kwenye ugomvi, unaweza ukavunjwa mguu hasa likija lile tupu. Aibu naona mimi wenye shirika lao wao sijui wanawaza kwa kutumia kiungo gani cha mwili.
 
Wenzio wameona opportunity hapo, watapiga mabilioni mengi kwenye kununua huo mfumo na usiwe na tija tena. Hiyo statement iliyotolewa imepangwa hajatolewa kwa bahati mbaya au umri wa alietoa. Kuna watu nyuma yake, kalaghabaho.
Inasikitisha sana wasomi na wale walioaminiwa kugeuza wezi na vibaka dhidi ya watanzania wengi wanaotegemea utumishi wao.

Mambo yamebadilika sana na kuna kila dalili yataanza kutupa changamoto ambazo wala hazina sababu yakuja.
Kila mbuzi ale kwa urefu wa kamba yake, je polisi atakula wapi? Magereza atakula wapi? daktari atakula wapi? It was a mistake to come up with that statement in the first place!!!

Bora daladala tunajua watampiga ngumi ya chembe mwenye mali yake!!!
 
Hapo bado route ya mbagala hali iko hivi wa ruhusu sekta binafsi wafanye hiyo biashara.Tuna ona mtu kams Aboud anao uwezo wa kuingiza magari zaidi ya 20 mapya kwa wakati mmoja.
 
Uongozi wa mwendokasi umekiri kwamba wameshindwa kuendesha miradi husika na hivyo wanasubiri hadi serikali inunue mfumo wa Artificial Intelligence wakuongoza magari. Hayo yamesemwa leo katika mahojiano baina ya waandishi wa habari na viongozi wa mradi husika.

Baada ya viongozi hawa kusema wamekwama, nimejaribu kuangalia umri wa kiongozi huyu, uwezo wake wa kuchakata issue nikabaini tuna watu wasio sahihi kwenye miradi yetu.

Kibiashara kuongezeka kwa abiria ni opportunity lakini kwa huyu kiongozi anatamani abiria wapungue. Kama huyu mtu yupo ofisini na analipwa salary tunategemea miradi hii iwe na ufanisi?
Mwendokasi angepewa mtu binafsi angefanya kazi 24Hrs na pesa ingeonekana, watu wa umma wengi ni wajinga sn
 
Inasikitisha sana wasomi na wale walioaminiwa kugeuza wezi na vibaka dhidi ya watanzania wengi wanaotegemea utumishi wao.

Mambo yamebadilika sana na kuna kila dalili yataanza kutupa changamoto ambazo wala hazina sababu yakuja.
Kila mbuzi ale kwa urefu wa kamba yake, je polisi atakula wapi? Magereza atakula wapi? daktari atakula wapi? It was a mistake to come up with that statement in the first place!!!

Bora daladala tunajua watampiga ngumi ya chembe mwenye mali yake!!!
Kila mtu anakula kwa urefu wa kamba yake
 
Watumishi wengi wa umma wamepata nafasi hizo kwa njia zisizohalali na kuwaacha wenye uwezo wanasaga lami mitaani! Connection, rushwa, undugunization, ukabila.
Dah unateseka ukiwa wap? Ume generalize labda kwa vile wewe umekosa. Hapo umekaa mpka unacheua maharage raha mstarehe ni kwamba muda huo watumish wanahakikisha mipaka ipo sawa, umeme upo sawa,ukiumwa utaenda utawakuta na utapata huduma sawa,hela zako benk mifumo ipo sawa kot huko watumish.sasa wewe mbona huna shukran
 
Uongozi wa mwendokasi umekiri kwamba wameshindwa kuendesha miradi husika na hivyo wanasubiri hadi serikali inunue mfumo wa Artificial Intelligence wakuongoza magari. Hayo yamesemwa leo katika mahojiano baina ya waandishi wa habari na viongozi wa mradi husika.

Baada ya viongozi hawa kusema wamekwama, nimejaribu kuangalia umri wa kiongozi huyu, uwezo wake wa kuchakata issue nikabaini tuna watu wasio sahihi kwenye miradi yetu.

Kibiashara kuongezeka kwa abiria ni opportunity lakini kwa huyu kiongozi anatamani abiria wapungue. Kama huyu mtu yupo ofisini na analipwa salary tunategemea miradi hii iwe na ufanisi?
Kama ningekuwa na mamlaka ningeweka mwekezaji kwenye huu mradi chap kuwaachia watendaji wa serikali asiliamia 100 ni kujikaanga wenyewe maana kama hali ikiendelea hivi miaka 2 mbele yakmtabaki mabasi matatu tu..

Mabadi yote yanakufa hakuna kukarabati wala nini..
 
Hiyo mbinu ya Mwendokasi hapa kwangu imeshapitwa na wakati, ninachowashauri huko, chimbeni barabara hizo za mwendokasi ziwe trench nyembamba sana saizi ya kufit minbus mtengeneze railway za mjini, hapo mtakuwa wote mnaingia ndani ya jiji mkiwa mmekaa, mnacheka, mnapiga stori na wengine wanalala, wengine wanafanya kazi online, na wengine wanapata wapenzi wapya!!
Take that!
 
Huyu bwege sijui huu utumbo aliokuwa anaongea kama aliwaza!
Hali ni mbaya sana na kwa muda mrefu, nahisi anakaa tu ofisi na kunywa kahawa!
Nashauri wizara ya uchukuzi iondokane na huyu mtu pamoja na bodi yote ya DART.
 
Yaani ulitakiwa ushangae kama huo mradi wa DART ungekuwa unafanya kazi vizuri, rekodi zinaonyesha kwamba HAKUNA hata mradi mmoja ambao umeleta TIJA chini ya serikali hii dhalimu ya CCM;
Miradi ya UMEME -Zero
Miradi ya Maji-Zero
Shirika la Ndege- Zero
TTCL- Zero
Vivuko,Kigamboni et al - Zero
DART - Big Zero
Tatizo uharibify unafanywa na CCM wenyewe kwa;
Wizi wa fedha hizo za miradi
Mikataba mibovu (iliyojaa ubinafsi ili wale wao)
Undugunization bila kujali taaluma (kada mwenzetu)
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom