Huyu Housegirl anafaa sana ila sitaki aendelee kufanya kazi hapa home. Mke wangu ni tufani

Komeo Lachuma

JF-Expert Member
Oct 31, 2014
5,364
11,520
Nimeandika uzi huu kutokana na uchungu mkubwa niliokuwa nao.. Mimi si mwandishi mzuri.Natamani kama kisa hiki ningemsimulia mtu kama gudume aandike yeye.

Roho yangu inanisuta sana. Toka nimeoa ni muda sasa. Tulifanikiwa kupata mtoto mmoja na hivyo tukaleta house girl atusaidie kazi mbalimbali. Huyu dada anatoka mkoa flani..Kiukweli ni mpole,mstaarabu anajali sana. Anamwangalia mtoto vizuri.Mtoto akilia huyu dada atambembeleza kwa upendo sana na kumnyamazisha.Wife mtoto akilia huwa hataki hata kuhangaika kujua analia nini utasikia tu " bupee..... Njoo umchukue mtoto mi nataka kupumzika" yule dada atamchukua mtoto na kumuuliza tatizo nini n.K

Kiukweli huwa inaniuma sana.Maana mtoto amemzoea na kumpenda housegirl kuliko hata mama yake. Hana habari na mama yake kama mama yake asivyo na habari naye.Nikiwepo mimi tutacheza vizuri n.K akiumwa anayejua kuwa mtoto anaumwa ni dada ndo atasema "Kaka leo xxx naona joto lipo juu" au leo anakohoa au ana mafua n.K. Nikisema twende hospital wife ananambia nimbebe mimi au twende na dada ndo awe anambeba.Yeye kucha ndefu hataki zikatike na amepaka rangi ya thamani sana.

Lakini kwa unafiki huyu mke wangu ndo kwake."Facebook na instagram zimejaa picha zake na mtoto akimwandika kwa majina mazuri ya kupendeza. Yaani utasema ana mapenzi sana kwa mtoto. Nikirudi toka kazini dada atanifungulia geti atakuja kunisubiria kama nina mizigo anipokee na kunambia pole na kazi. Wife hata akiwa likizo muda huo atakuwa sebuleni anacheck movie,anachat au yupo insta.

Dada ndo anajua tule nini,mtoto anakula nini,chakula kimeisha n.K niliumwa sana kipindi flani nakumbuka siku hiyo wote tupo sebuleni.Mimi na mke wangu.Nikatapika... Wife alichofanya ni kunambia nisitapikie kwenye sofa... Dada alikuja akaniletea ndoo na pale chini akaanza kupiga deki.Matapishi yangu.Haraka akaingia jikoni na kuanza kutengeneza uji wa limao.Baada ya dk chache nililetewa uji wa limao ninywe.Sikumwambia.Wife ameweka miguu juu busy na simu.Sikujua nimwambie nini.

Housegirl amelata uji ila anaambia ameniweka maji ya uvugu vugu bafuni nioge kwanza then nije ninywe uji nipate nguvu. Dawa alishazileta kaziweka mezani.Hali hii iliniuma sana....Maana haya ni mambo ambayo alipaswa ayafanye mke wangu.Nlijaribu sana kipindi flani kumwambia wajibu wake..Akanambia kwa dunia ya sasa wote tunafanya kazi so ni ngumu naye anarudi amechoka..Ningetaka mwanamke wa hivyo ningeoa ambaye ni mama wa nyumbani.

Kuna mengi ambayo sitaki yaelezea. Na niwe mkweli huyu dada hajaonesha hali yoyote ya kunitega. Anafanya from the heart. Na malezi ya mtoto naona hata mtoto mwenyewe anampenda sana dada kuliko mama yake. Na mama yake proudly kabisa nimemsikia akizungumza mbele ya wenzie "Yaani xxx mimi nikiwepo wala hajali ye kila wakati tu ni aunt aunt... Kama vile mimi sipo... Mi namwachia aunt yake si namlipa? Ndo amwangalie mtoto wangu vizuri sasa" nliumia sana.

But nimewaza haya baada ya kuona huyu dada anaingia moyoni mwangu.Aliishia form 2 ila she is so smart.Ana akili na anajua kuishi na watu. Nimejikuta naanza kumpenda.Napomtizamana najikuta mapenzi yanabubujika. Mara kadhaa namtizama najikuta moyo unashtuka.Nawaza why sikumwoa yeye? Mwaka wa pili naishi naye mtoto anakua mikononi mwake akiwa na afya njema kabisa. Ana mapenzi kwa watoto, ananijali ananiheshimu. Mke wangu ana sura na umbo zuri.Ila ni mjeuri,mkaidi mwenye majivuno na dharau kwa watu.

Nataka nimwondoe house girl maana mapenzi yananizidi kwake. Nami sitaki kufanya kosa la kutembea na house girl.Sitaki nimwaribie na yeye..Ila nawaza nikimwondoa ntamwondoa kwa sababu gani.Hajanikosea kitu? Then mtoto atakuwa katika hali gani?Maana mtoto anampenda sana aunt yake. Sana kiasi kwamba napata shida ataishi vipi na je ataathika kiasi gani?Nitamwambia mke wangu kwa nini tumwondoe?
 
huna hata kapicha ka house girl?

Ingekuwa mimi ndio wewe.
Kwanza.
1.ningetapikia sofa
2ningetapikia TV
3.ningetapikia hata simu yake
4.ningemwambia hausi girl akalale.

Ila kwa upande mwingine mwanaume mzima upo sebuleni tena nyumbani kwako. Unasikia kutapika si uinuke ukatapikie bafuni?au nje?
Yani umekaa kabisa kitako unajitapikia hadi hausigel anakuletea ndoo?
Una matatizo gani? Mwili mzito ama?

Pambana na hali yako. Na ushauri wangu kwako.


Usije ukajaribu kutembea na huyo house girl.

Kwanza ni dhambi. Kama ulifunga ndoa hasa ya kanisani maana yake unaichezea madhabahu. Utakuja kupata laana ya maana.

Upo kwenye ndoa tulia. Ndoa ni ndoano.

Na mimi kama mwanaume mwenzako nakushauri tu kuvumilia na kubaliana na hali halisi.
Kila mtu akikupa matatizo ya ndoa yake hapa utajiona kuwa wewe huna shida wana huna tatizo. Utajiona wewe ni malaika.

Kuna wengine kwenye ndoa zao mkewe anataka dushe kubwa ila yeye ana kibamia.

Afanyeje?
Anatulia tu na kuvumilia ya dunia.

Au mwingine ni hanithi..

Ila atafanyaje? Ili kutunza heshima kwenye jamii?

Hujasikia kisa kimoja jamaa alimlipa mshkaji wake alale na mkewe ili angalau apate mimba. Mke akaomba na likizo kabisa. Alilipa mil3. Ila mke hakupata mimba. Kumbe mshkaji wake nao ana matatizo na ana watoto watatu ambao sio wa kwake.

Upo hapo brother?

Sitaki kukupa visa vingi vya kwenye ndoa ila..

Shukuru Mungu uko fit na una mtoto na upo able kuilea familia yako na mke wako hachepuki nje .

Tumia akili kama mwanaume. Mwanamke haweZi kukushinda.. Inawezekana mke wako anapenda sana kusifiwa..

Hata akipika chai anataka uisifie.. Akivaa kapendeza anataka umuone na umsifie .. Akiongea kitu mpe attention..

Na mpe misifa kede kede.

Utaona mabadiliko.
Hilo ni wazo moja nimekupa..

Mengine jiongeze kama kidume acha kulia lia.

Ndo kama nilivyosema ndoa zina mambo mengi sana..

Ila kati ya yote muweke Mungu mbele.

Ngoja niachie hapa manake nishaanza kujiona mangekimambi
 
Kupanga ni kuchagua kwa sauti ya mfalme ji.w.e. hapo mkuu futa hisia zote za mapenzi kichwani mwako mchukulie tuu kama msichana wa kazi usijaribu kumwondoa wengine tunawasichana wa kazi mizigo sana . Unakuta mke mzigo msichana wa kazi nae mzigo.
Hadi mtoto inabidi uwe unamwangalia mwenyewe
 
Usilie wewe ni mwanaume kabisa kulia sio suluhu ya changamoto yako

Kikubwa kaa na wife zungumza naye mweleze wajibu wake na anavyopaswa kukuhudumia lkn na wewe umuhudumie vyema

Jiangalie kama unapenda kupiga naye story jifanye nawe mbeya huko insta na facie ili umfanye apende kupiga story nawe harafu atabadilika ikishindikana kubadilika muoe hause girl licha naye anaweza kuwa anabembeleza kazi tu
 
nimeandika uzi huu kutokana na uchungu mkubwa niliokuwa nao.. mimi si mwandishi mzuri.natamani kama kisa hiki ningemsimulia mtu kama GuDume aandike yeye.

roho yangu inanisuta sana. toka nimeoa ni muda sasa. tulifanikiwa kupata mtoto mmoja na hivyo tukaleta house girl atusaidie kazi mbalimbali. huyu dada anatoka mkoa flani..kiukweli ni mpole,mstaarabu anajali sana. anamwangalia mtoto vizuri.mtoto akilia huyu dada atambembeleza kwa upendo sana na kumnyamazisha.wife mtoto akilia huwa hataki hata kuhangaika kujua analia nini utasikia tu " bupee..... njoo umchukue mtoto mi nataka kupumzika" yule dada atamchukua mtoto na kumuuliza tatizo nini n.k

kiukweli huwa inaniuma sana.maana mtoto amemzoea na kumpenda housegirl kuliko hata mama yake. hana habari na mama yake kama mama yake asivyo na habari naye.nikiwepo mimi tutacheza vizuri n.k akiumwa anayejua kuwa mtoto anaumwa ni dada ndo atasema "kaka leo xxx naona joto lipo juu" au leo anakohoa au ana mafua n.k. nikisema twende hospital wife ananambia nimbebe mimi au twende na dada ndo awe anambeba.yeye kucha ndefu hataki zikatike na amepaka rangi ya thamani sana.

lakini kwa unafiki huyu mke wangu ndo kwake."facebook na instagram zimejaa picha zake na mtoto akimwandika kwa majina mazuri ya kupendeza. yaani utasema ana mapenzi sana kwa mtoto. nikirudi toka kazini dada atanifungulia geti atakuja kunisubiria kama nina mizigo anipokee na kunambia pole na kazi. wife hata akiwa likizo muda huo atakuwa sebuleni anacheck movie,anachat au yupo insta.

dada ndo anajua tule nini,mtoto anakula nini,chakula kimeisha n.k niliumwa sana kipindi flani nakumbuka siku hiyo wote tupo sebuleni.mimi na mke wangu.nikatapika... wife alichofanya ni kunambia nisitapikie kwenye sofa... dada alikuja akaniletea ndoo na pale chini akaanza kupiga deki.matapishi yangu.haraka akaingia jikoni na kuanza kutengeneza uji wa limao.baada ya dk chache nililetewa uji wa limao ninywe.sikumwambia.wife ameweka miguu juu busy na simu.sikujua nimwambie nini.

housegirl amelata uji ila anaambia ameniweka maji ya uvugu vugu bafuni nioge kwanza then nije ninywe uji nipate nguvu. dawa alishazileta kaziweka mezani.hali hii iliniuma sana....maana haya ni mambo ambayo alipaswa ayafanye mke wangu.nlijaribu sana kipindi flani kumwambia wajibu wake..akanambia kwa dunia ya sasa wote tunafanya kazi so ni ngumu naye anarudi amechoka..ningetaka mwanamke wa hivyo ningeoa ambaye ni mama wa nyumbani.

kuna mengi ambayo sitaki yaelezea. na niwe mkweli huyu dada hajaonesha hali yoyote ya kunitega. anafanya from the heart. na malezi ya mtoto naona hata mtoto mwenyewe anampenda sana dada kuliko mama yake. na mama yake proudly kabisa nimemsikia akizungumza mbele ya wenzie "yaani xxx mimi nikiwepo wala hajali ye kila wakati tu ni aunt aunt... kama vile mimi sipo... mi namwachia aunt yake si namlipa? ndo amwangalie mtoto wangu vizuri sasa" nliumia sana.

but nimewaza haya baada ya kuona huyu dada anaingia moyoni mwangu.aliishia form 2 ila she is so smart.ana akili na anajua kuishi na watu. nimejikuta naanza kumpenda.napomtizamana najikuta mapenzi yanabubujika. mara kadhaa namtizama najikuta moyo unashtuka.nawaza why sikumwoa yeye? mwaka wa pili naishi naye mtoto anakua mikononi mwake akiwa na afya njema kabisa. ana mapenzi kwa watoto, ananijali ananiheshimu. mke wangu ana sura na umbo zuri.ila ni mjeuri,mkaidi mwenye majivuno na dharau kwa watu.

nataka nimwondoe house girl maana mapenzi yananizidi kwake. nami sitaki kufanya kosa la kutembea na house girl.sitaki nimwaribie na yeye..ila nawaza nikimwondoa ntamwondoa kwa sababu gani.hajanikosea kitu? then mtoto atakuwa katika hali gani?maana mtoto anampenda sana aunt yake. sana kiasi kwamba napata shida ataishi vipi na je ataathika kiasi gani?nitamwambia mke wangu kwa nini tumwondoe?
Kama kweli unampenda kiasi hicho... Mpeleke shule.. Ongea nae pembeni akuelewe.... Aombe kuondoka umlipie shule hata evening class amalize form 4
 
mkuu uko kwenye chumba cha mtihani, hapo ni maombi tu yaweza kukukwamua hapo!
ushauri wangu ;- 1. zidi kuzungumza na mkeo mkumbushe wajibu na majukumu yake, mkumbushe na muoneshe vitu unavyovikosa kwake, uone matokeo yake.
2. Huyo dada wa kazi kakutendea mengi mema msaidie kitu fulani katika maisha yake mfano ufundi wa kudarizi, n.k kitu kitakacho msaidia katika maisha yake, kuendelekea kukaa na huyo dada chances za kushiriki naye ngono ni kubwa kwa kweli, ingawa kuna changamoto ya kutompata dada wa kazi mwema kama yeye, iokoe ndoa yako, kila la heri!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom