Huyu Demu nimwambie nini ili anielewe?

kabila01

JF-Expert Member
Apr 21, 2009
4,235
4,949
Kuna demu mmoja nilikua na mahusiano naye zamani sana ilikua mwaka 2003, mahusiano yetu yalikaa kama miezi mitatu then akaondoka kurudi kwao Ngara. Katika kipindi cha mahusiano yetu hatukuwahi kufanya tendo la ndoa, lakin kwa jinsi tulivyokua tunapendana kila mtu alijua pale mtaani hadi wazazi wangu na ndugu zake pia. By that time yeye alikua amemaliza form six na mimi nikifanya kazi ya ualimu kijijini. Alipoenda kwao Ngara tuliendelea kuwasiliana kama miezi sita baada ya hapo mawasiliano yakafifia baadae tukapoteana kabisa. Baadae nikiwa chuo kikuu akanitafuta kwenye cm ingawa nilikua nimebadili line na akaniambia kua yupo chuo kikuu Mwanza Sauti. Hapo mawasiliano yakawa kwa mbali sana labda mie ndo nimpigie simu. akiwa mwaka wa mwisho chuoni akafunga ndoa na alinipa taarifa nikamtumia hela ya mchango kupitia a/c yake. Ingawa niliumia lakin baadae nikaamua kuchukulia kawaida na kuanzisha maisha mapya mwenyewe. alipomaliza chuo na mimi pia nikawa namaliza chuo nikabahatika kupata kazi yeye akawa bado yupo nyumbani kwa mumewe. akiwa kwa mumewe alikua akiniomba nimsaidie kumtafutia kazi nami nikawa nikiziona nafasi za kazi nampatia ajaribu, mawasiliano yakawa kama kaka na dada. Sasa hivi baada ya yeye kupata kazi na mimi nikawa nimehamishiwa jirani na mkoa alipo yeye. Sasa kasheshe ikaja siku niliyomwambia kua nimehamishwa tena kikazi nahamia Dar. Hapo ndo akaaanza kuniambia kua mimi nipo Moyoni mwake na anapata sana mateso juu yangu. usiku akilala na mumewe anahisi kama amelala na mimi, hata akiwa anafanya tendo la ndoa na mumewe bado anahisi kama yupo na mimi. imefikia kipindi hata akikaa na mumewe sebulen basi anatoroka anaenda nje ili anipigie tu simu tuongee.
Nimejitahidi kwa kila hali kumkwepa na kumwambia kua mie saizi nina mchumba ninayempenda na nataka kumuoa hivi karibuni bado anaendelea kua king'ang'anizi. nimejaribu kubadilisha line ya simu sijui wapi kaipata no yangu nashangaa ananipigia simu.
Naelewa kua mke wa mtu ni sumu na ni noma kutembea na mke wa mtu na hasa akijua bwana wake. najaribu kutopokea hata simu zake akipiga na akiandika sms sijibu lakin wapi. amesema ataamua kukimbia kwenye ndoa yake na kuja kwangu kitu ambacho ni hatari sana
sielewi wana JF huyu demu nimwambie nini anielewe maana ataniharibia future yangu ya maisha
 
Pole sana! mpotezee, kwanini sa hizi baada ya kuolewa ndo akukumbuke? ndoa yake imemshinda anatafuta sehemu ya kupata releif.
 
Kabila01 sometimes haijalishi ni nini unaongea, ila jinsi unavyoongea inaweza fanya asikuelewe ...
 
Kwa anavyokufanyia kweli atakuharibia. Wewe cha kufanya ni kumtishia kuhusu kumtaarifu mume wake (jifanye kama unayo no. ya mume wake). Then sikilizia hali itakuwaje. Pia jua kuwa mchumba wako akija akibaini mwenyewe kuhusu hilo, utakuwa umemkosesha amani. Hivyo siyo vibaya kumjuilisha mchumba wako ikiwa tu mnaishi pamoja au muda mkubwa mko pamoja. Pia acha kumpa msaada katika shida zake.
 
sio kumtishia kuwa utamwambia mume wake kuhusu king'anga'nizi chake, wewe ni kufanya kweli, mtafute mume wake alipo mtembelee na uso kwa uso mpatie michapo ya mkewe. purukushani atakayoipata kutoka kwa mumewe ndiyo labda inaweza kumfanya akuachie LOL
 
My brother,mwambie tu mumewe kama una contacts zake,na kama kuna watoto wanahusika katika kinyang'anyiro hiki,nakuomba ukae nae mbali kwani na sisi wanaume tuna weakness zetu na anaweza kukutaim siku ambayo uko lonely or just plain horny...mwambie na mchumba wako situation unayoiface! Good luck bro!
 
Mweleze ukweli na hakikisha mazungumzo hayapo kabisa kwa kipindi kirefu! Unaweza kumwambia mume wake! Lkn je akigeuza kibao ya kuwa ww ndio unamtaka amekukataa ndio ukamueleza mume wake! Mpaka mumewe amuelewe/akuelewe itachukua muda
 
Mwambie wewe na mimi kuwa pamoja tena haitawezekana kwa sababu:
  1. Una mume
  2. Nina mchumba
  3. Awali hukuwa na subira
  4. Moyoni haupo tena
  5. .........................
 
Tatizo kupenda usipopendwa...

Usema ukweli hutaweza kuukataza moyo wa
mtu kupenda... cha kufanya we timua bila hata kumuuaga.. usiseme unaenda wapi.. Ila na we kuwa na uhakika humpendi .. isija kuwa na we Una chembe fulani juu yake..
 
5. Hata ukioa huna mpango wa kuchakachua
6. Misaada uliyokuwa ukimpa ni kama kaka na dada tu pia ni kumuonesha kuwa hukuwa na kinyongo naye na umeridhika yeye kuolewa
7. Mchumba wako wa sasa ni "Tyson" akimgundua atamharibu sura
8. ..............................................................
Mwambie wewe na mimi kuwa pamoja tena haitawezekana kwa sababu:
  1. Una mume
  2. Nina mchumba
  3. Awali hukuwa na subira
  4. Moyoni haupo tena
  5. .........................
 
Samahani kama nitakuwa off topic Mkuu; Ila kwa kweli kabisa huwa sipendi kabisa kumuita mwanamke demu nahisi kama anakosewa heshima na hatendewi haki. Natambua kuwa katika lugha ta ki-dutch mwanamke huitwa dame lakini matumizi ya neno demu katika lugha yetu ya kiswahili huwa naona kama vile yanamdhalilisha mwanamke wa kitanzania. I am proud of Tanzanian women
 
sio kumtishia kuwa utamwambia mume wake kuhusu king'anga'nizi chake, wewe ni kufanya kweli, mtafute mume wake alipo mtembelee na uso kwa uso mpatie michapo ya mkewe. purukushani atakayoipata kutoka kwa mumewe ndiyo labda inaweza kumfanya akuachie LOL

Ukitaka kuchukua uamuzi wa mambo haya ni vyema kwenda hatua kwa hatua coz lengo siyo kuharibiana bali ni kujenga. Hivyo kumtishia ni hatua ya mwanzo ambayo inaweza kufuatiwa na kumuenform mume wake au kwa wazazi wake (coz ndiyo anaowafahamu).
 
Samahani kama nitakuwa off topic Mkuu; Ila kwa kweli kabisa huwa sipendi kabisa kumuita mwanamke demu nahisi kama anakosewa heshima na hatendewi haki. Natambua kuwa katika lugha ta ki-dutch mwanamke huitwa dame lakini matumizi ya neno demu katika lugha yetu ya kiswahili huwa naona kama vile yanamdhalilisha mwanamke wa kitanzania. I am proud of Tanzanian women

mi natumia lakini naangalia mazingira na huyo ninayemuongelea yukoje. Kwangu siyo kila mwanamke kuwa ni demu ila kila demu ni mwanamke. Katika mtandao (sehemu kama hii) au media nyengine haipendezi kutumia neno kama demu na mengine yanayomuwakilisha mwanamke (siyataji).
Ni dakika chache tu kabla ya thread hii mtu alitumia neno hili katika kipindi cha "Ladha laini" na muendesha kipindi hakukaa kimya ila alimuambia kuwa siyo vizuri.
 
Mawazo ya Mkwaruzo, Kobelo, Futota na Maria roza yote nayaunga mkono kwa 450%. Usipoangalia na kwako yatakuharibikia. nakupa mfano live: Mimi kulikuwa na mtu kama huyo ambaye alifikia hata kuniapia kuwa jamaa yake ayuko nae tena na hamtaki kabisa, kumbe alikuwa anatanua ujasiriamali tu, na kuongeza slots za ATM.
Bahati nzuri nilifanikiwa kupata namba ya bwanake, na yeye akawa amenitumia meseji yakutaka mahela kutoka kwangu. What I did, Niliforward ile meseji kwa bwana wake na koments kuwa yawezekana meseji hii imekosewa kuja kwangu ila ilikuwa intended kuwa yako, samahani kwa usumbufu.
jamaa aliniomba nimueleze ni wakati gani nimetumiwa meseji hiyo? Nikamwambia sasa hivi. Kumbe by then yule jamaa alikuwa yuko nae hospitali anagharamia matibabu yake. From that date yule mwanamke hajarudia tena, na yeye ndiye aliyeniomba niifute namba yake kwangu, na usumbufu umeisha. Jaribu hiyo dawa itakuwa tiba kamili kama kikombe cha babu:A S 103::A S 103::smow::smow::dance::dance::dance::biggrin1:
 
Back
Top Bottom