SASA TUENDELEEEEE
Baada ya kutoka kuzungumza na uyo binti nilikua km plug azichomi ivi maana nilihisi moyo tu ndio unafanya kazi viungo vyote na akili vimesimama kwa kutokuamin yanayo tokea katika maisha yang ukumbuke tang tufahamiane na G ni miezi8 ilikua imepita ayo ndio yanaanza kutokea iyo siku ndio siku ya kwanza natumia pombe Kali konyagi maana sikutaka kukumbuka kitu usiku nakumbuka nililewa Sana na sikuweza kwenda nyumbani nilijikuata Niko kwenye chumba cha lodge Niko peke yang na kila kitu chang kiko salama na ni SAA4 asubuh wafanya usafi ndio wananiamsha nilijimwagia maji nikaenda home Ku change nikaenda shop nikafungua kisha nikaenda kwa G Niki taka kupata uthibitisho wa yale nilio yasikia kutoka kwa ndugu yake ,
Alinikaribisha huku km ajiamin ivi nilamsalimu baada ya salaam nikamuuliza kwanin? Amebadilika ukumbuke kipindi icho na simu na text zimepungua Mara apokee Mara asipokee ndivyo ilivyo kua basi tuendelee akasema amuna kitu ni u busy tu namimi sikumficha nikamueleza kila kitu nilicho elezwa kuhusu yeye mpka tarehe ya mahar na kunithibitishia alinyamaza kimya akanambia aliona Mimi nampotezea mda na sikua na mpango nae na tayar tulikua tushapanga mwaka unaofuata yaan 2017 ndio ndoa yetu akuwa na cha kusema ni aibu tu kwa hasira nikaondoka huku kichwa kikiwa na msongo mwingi wa mawazo nikiwaza nishamtbulisha kwa watu Wang wa karbu watanielewaje na alimanusura nmpeleke nyumbani nishaanza kuingia kwenye kamati za harusi mbali mbali nikijua yangu aiko mbali ivyo nianze kuchanga maana nitahtaji kuchangiwa na mimi ayo mambo yote yalinivuruga kichwa nikaona bora nilewe tu pengine Niko ndotoni nitazindika kutoka usingizini lakini aikua ivyo ,
Mipango ya harus iliendelea na wakafunga ndoa ya kihalali kanisa katoliki huku Mimi familia na jamaa wasijue kitu gan kimenipata duka nilimuachia yule dogo walevi ndio wakawa rafiki zang nakumbuka Mara kadhaa nilipelekwa na mama kuombewa kwa watumishi tofauti tofauti wakiamin nimelogwa kumbe G ndio ameniloga juhudi zote azikua na mafanikio mtaji uliyumba nikaanza kukopa kwenye taasisi na pesa izo akuna nilicho fanyia zaidi ya pombe mambo yakawa Magumu heshima yang nyumbani ikaisha nikabakia kuitwa mlevi sababu ya G ata marafiki nilio kua nao wakawa wananikwepa maana nilitoka kunywa henken,castle lite mpka kwenye pombe za karatasi au viroba,
Mambo yakawa magumu madeni kila kona na huku mikoan tunajuana Sana nikageuka story of the town watu wasijue kitu gan kimenipata,.
Ndani ya miez 8 nilikua nimetoka kwenye ujana mpka uzee ata ile sura yang ya ujana imepotea kila kitu ni kingine watu wanasema nimwlogwa,madeni yalinizidi nikakimbia mji ulikua mchungu nikaenda zang kwa bashite nikiwa sina hata nakumbika nauli ya kwenda huko niliuza laptop nilio kua naitumia chuo,.
Nilifika dar nikaanza maisha mapya kwa mkubwa Wang yeye ni mfanya biashara kko ivyo asubuh tukawa tunaenda nae na jion tunarudi lakin tayar nishakua teja maana mda wote nilikua alcohol na nikipotea kidogo tu nilikua naenda Ku charge betri.
Niliendelea ivyo ivyo na ayo maisha mpka siku Mungu alipo nirudishia akili zang Mimi mja wake nakumbuka iyo siku usiku sikunywa Sana ivyo ikapelekea usingizi kuisha mapema kwenye SAA8 iv ulikua umekata nikaanza kukumbuka mambo ya nyuma ikiwa ni mwaka umepita nikaangalia nilivyo kua na Sas NIKAAPA KUTOKUTUMIA POMBE TENA KWENYE MAISHA YANGU mwanzon nilipata shida maana nilikua nasikia kiu km mtu alieshinda kwenye jua siku tatu akifanya kazi ngumu bila kunywa maji ila hakika Mungu ni mwema alinisaidia nikaanza kwenda kanisan na kujitenga na marafiki walevi ambao ata dar nilikua nishakuaa nao,
Baada ya miezi mitatu nishakua na tabia njema wazazi na ndugu wakanichangia pesa nikafungua duka LA Viatu kkoo na maisha yakaanza upya,
UYU IBILISI WA KIKE sijui nan ! Alimwambia Niko sawa saaaiv akaanza kunitafta kuniomba msamah mi nikamuambia ujanikosea Kila mtu anachagua mtu sahii wa maisha yake ndio akaanza kunisimulia Analia jamaa yake alimdanganya anafanya kazi ofsi ya rais atamtaftia kazi BOT au wizara ya fedha kumbe jamaa ni mwalimu tena shule ya private alikua anaazima magar kwenda kwao G basi akaniomba nimsamehe na kwa kipindi icho G alivyo jua jamaa amemudanganya akavunja ndoa akarudi kwao ,tukawa tunasalimiana tu kawaida mpka mwaka huu Mwezi wa 1 alikuja dar kwenye harus ya ndugu yake akasema anataman afike kwangu maana nishatoka kwa bro najitegemea,
Ilikua siku ya jumamos nilienda kkoo. kwenye mishe zangu akanipigia simu mida ya saa8 anataka kuja home basi nikamwacha mshikaji makufuli jion atafunga mi nikaenda home Nikamuelekeza akafika nilikua nataman nimuone maana ni. siku nyingi na nilikua nampenda shida nijeraha moyoni alifika akashangaa kukuta Niko poa tu maana wanaume Kurudia khali yetu ni simple tofaauti na wanawake tulipiga story 2,3 mpka usiku ukaingia nasubr mtu aage sioni mtu km anadalili za kuondoka nikamwambia usiku unazidi kua mrefu naomba nikusindikize nashangaa MTU anaanza kulia nimsamehe kumbembeleza kujikuta tuko kitandani tunatinduana,
Akaa siku 2 lakini nishasema sito kaaa nirudiane nae uyo mwanamke alivyo toka tu nika mbolck akasafr kurudi mkoan na baada ya miezi mitatu Ananiambi anaujauzito Wang na awezi kuutoa ata km simpendi lakini atoi mimba Mimi nae nimemkaushia na nimebadili na namba Za simu maaana nikikumbuka aliko nipitisha naumia Sana aibu aliyo nipatia alafu Leo nimuoe apana acha tu abaki na mtoto wa makumbusho ameshaniaribia moyo wang iman sina tena tamani kuoa Ila yale matukio nikiyakumbuka moyo unasita na umri unasonga na Nimekua na tabia ya kuanzisha uhusiano na ghafla naanza kumchukia tena munisaidie nitafanyeje niweze kurudi hali ya mwanzo niweze kumuamin tena mchumba nitakae mpta MaanA km moyo wa kupenda sina tena