Huyu dada nimfanyeje niko njia panda

Huyu dada nimfanyeje niko njia panda

kamituga

JF-Expert Member
Joined
May 31, 2019
Posts
1,195
Reaction score
1,937
Nakumbuka ilikuwa mwaka 2015 ndio nakutana na huyu Dada kwenye moja ya mikoa kanda ya ziwa alikuja kwa mjomba wake na mimi nilikuwa zangu nishaanza mapambano ya kusaka $ .

Alikuwa amemaliza Kati ya moja ya vyuo jijini Mwanza na kwa wakati huo alikuwa yupo yupo hivyo mjomba wake akaona ni vema aje kwake kipindi anasubri mambo yake amsaidie kuuza duka la vifaa vya ujenzi mjini hapo ambapo mjomba wake ana maduka kadhaa.

Katika pitapita zangu mtaani maana mimi pia nilikuwa nafanya hiyo biashara mtaa wa pili na kilichonikutanisha na huyo binti ni mteja wangu alikosa item aliyoitaka dukani kwangu akaomba nikamtaftie kwa wenzangu kwa kigezo cha mimi ndio najua ubora wa item kufika pale ndio nikakuta MTOTO amesimama sio sura sio rangi sio umbo mrefu km mtusi mate yakanitoka mdomoni mithiri ya muathirika wa dawa za kulevya wa muda mrefu hapo ndio mwanzo wa kujuana na huyu mrembo aliyegeuka badae sumu katika maisha yangu.

Sikuwa na papala siku ya kwanza na maadam nilijua anapopatikana nilijiapiza kufanya kila ninachoweza ili awe wangu nikaona sio vema kwenda nae kwa speed nikapanga mikakati kama ya Michael Scolfied kwenye prison break.

Zilipita siku tatu na siku ya nne nilirejea tena pale dukani kwa mjomba wake nikamsalimia kwa bashasha na ukarimu wa hali ya juu huku nikiwa nimetupia pamba mpya kwanzia juu mpaka chini na nimetoka barbar shop muda sio mrefu kabla sijamtokea pale.

Alinisalim pia lakini hakuonesha kunijali ikawa km hanikumbuki hivyo ilinilazimu kumkumbusha akanikumbuka na sikuwa na mambo mengi nilimwambia kilichonipeleka pale nilihitaji kujua anaitwa nan? Nilimwambia sio vema tunafanya biashara mtaa mmoja na biashara ya aina moja tusijuane,hilo alikumsumbua kichwa akanieleza jina lake anaitwa G na Mimi nikamwambia la kwangu.

Siku hiyo ilikuwa ya furaha sana kwangu kwakuwa mission yangu ya siku iyo ilitimia,Niliondoka dukani pale huku mission inayofuatia ni ya kuchukua namba yake ya simu ya kiganjani.

Baada ya siku mbili kupita niliamka asubuhi na mapema nikajiandaa kwenda dukani kwangu huku nikijiapiza moyoni kuchukua namba ya simu. Siku hiyo nilifika dukani kama kawaida nikafungiu kisha nikamsubiri dogo kuna dogo nilikuwa nae pale alivyofika nikaondoka kwenda kuzunguka madukani kutafuta simu mpya maana ile yangu niliona kama haifai na imeshakaa mwaka mmoja hivyo nilifanikiwa kununua simu nyingine akili nyingine ya kiwenda wazimu ikanituma ninunue nguo mpya tena kwa kigezo zangu hazifai sijui yule mwanamke nilimuonaje kwa kipindi hicho tofauti na sasa.

Nilirejea dukani kwa mtoto mzuri nikamkuta anaendelea na biashara safari hii ikawa tofauti akanisalimu kwa ukalimu na pia akanambia nimependeza sana hapo moyo unafurahi kwa ndani na kichwa kinavimba. Alivyomaliza tukapiga story mbili tatu za kibiashara mwisho wa siku nikamuomba namba kwa kigezo cha kibiashara kwamba kuna vitu vingine unakuta sina dukani kwangu hivyo kujua kama anavyo endapo wateja wangu watahitaji tunapaswa kuwasiliana. Hiyo technique alikuwa hawezi kuruka akaniomba simu aandike kumbuka nimenunua simu latest kwa wakati huo kwa watu wenye uchumi wa kawaida lakini unaweza kujiuliza nilikuwa naweza kuyamudu haya yote ukumbuke miaka miwili nyuma nilikuwa nimetoka chuo na sikuamini kuajiriwa hivyo mzazi alinibariki pesa za kuanzisha biashara na kwa kipindi hicho chote nilikuwa niko home pesa yangu ilikuwa ya matumizi yangu tuu sikuhusishwa kwa lolote na chochote.

Baada ya Ku-win biko km sio tatu mzuka ya kupata no mission yangu kwa 75%ilikuwa imekamilika nilianza kuangalia madhaifu na mapungufu yake nikagundua kwenye suala la chakula na usafiri ni changamoto maana unakuwa busy kiasi kwamba anakosa nafasi ya kwenda sehemu nzuri kuagiza chakula hivyo inamlazimu kula chakula kwa mamantilie wanaouza mabarabarani na kwenye usafiri nikagundua asubuhi anakuja na mjomba wake na jioni anapanda pikipiki nikawa nimepata sehemu ya kuchukulia point3 kavu.

Tushakuwa na mawasiliano na kila mtu anamjua mwenzie katika kuchat chat nikamuomba nimpe lunch siku hiyo akanambia hawezi kutoka nikamjulisha itamfata hapo hapo akakubali ofa yangu nikafurahi sana nikatafuta mgahawa unaouza chakula kizuri mkoani hapo haikuwa kazi ngumu kuna wasomali ni mabingwa wa kupika nikaomba kuweka bili wakakukubali nikawaelekeza duka la huyo mrembo lilipo kwa makubaliano ya kuanza bili siku inayofuatia Ila siku hiyo nililipia cash na nikamuagizia pilau na kuku wakampelekea

Alifurahi sana na kukisifu chakula na sikumwambia kama nimemuwekea bila siku iliofuata nilienda kulipia pesa na kuwambia wampelekea chakula cha tofauti na siku iliopita na pia wampe taarifa kuwa amewekewa bili ya msosi hivyo awe anatoa taarifa ya siku inayofuata chakula atakachopenda kutumia.

Alinishukuru kwa ajiribya hilo na ukaribu wetu ukaongezeka tukawa tunawasiliana mara kwa mara bila kuonesha dalili za kutakana, sikutaka kuwa na speed maana nilijua jinsi ninavyompenda angenikataa ningeumia sana.

Ilikuwa weekend moja tulivu nakumbuka siku hiyo mvua ilinyesha nikamuomba tukutane kwenye moja ya hotel nzuri hapo mkoani kwa ajiri ya kupiga story za kirafiki na chakula pia kama hatojali alinikubalia ombi langu na hakua na mashaka na mimi tena.

Hiyo ndio siku niliyofungua moyo na kutoa kilichokuwa ndani alinisikiliza kwa makini na nilimuomba tuwe Wapenzi Ila tukiwa na mpango wa kuoana maana nilimueleza ni jinsi gani moyo Wangu unamuhitaj awe Wang na nikala kiapo kwamba ikitokea ananikubalia sito kuja kumsaliti au kutoka na mtu mwingine kamwe maana nilimuona yeye ndio Mwanzo na mwisho, Kiukweli alikua jambo gumu kwake akanijibu nimpe mda nimemshitukiza hakua amejiandaa kwa hilo nikamuelewa tukaendelea kutumia vinywaji alipendelelea red bull na Mimi nikawa natumia vitamalt nachanganya na coke nilikua Natumi Bia lakin sikupenda kujiweka wazi maana sikujua angenichukulia vp kpz Wang uyo,

Siku kadhaa zilipita tukiendelea kuwasilaana kawaida na mimi sikua na presha maana tayar mzigo nilio kua nimebeba moyoni tayar nisha utua ghafla text msg ikangia kwenye siku yangu ilikua km ifuatavyo (E nakupenda kuliko kitu chochote nakupa moyo Wang tafadhali usije ukanitoa machozi) Hapo ndio dunia mpya ikawa imefunguka baina yang na G sio siri kwa mtu yoyote alie tuona kipindi hicho alipendezwa na namna tulivyokuwa mda baada ya kazi nilimpeleka mpaka nyumbani sio siri alionesha kunipenda na mimi nikampenda Sana tena Sana na tulifanya mambo mazur km sio yote ambayo watu wanao pendana wanapswa kufanyiana.

GHAFLA ibilisi akaingilia penzi letu ndio kilicho pelekea Leo naandika yote haya G akaanza kubadilika taratibu akaanza kufunga biashara anaenda nyumban bila kuniarifu nikawaza ni bahati mbaya kumbe alikusudia na mimi mshale ukaanza kunigota kutaka kujua ni nni? Kinachotaka kudhulumu penzi langu nikaanza kufatilia kuna baadhi ya ndugu zake nilikuwa nafamiana nao ndio mmoja akanambia G amepata mchumba anataka kumuoa na nyumbani amekuja ameleta vitu mahari ni mwezi ujao ,Sio siri nilipokuwa sijui mwanamke ananikwepa kwepa kumbe anayake.ITAENDELEA BADADAE KIDOGO
 
Sasa kama amepata mchumba na ameshapeleka vitu nyumbani kwao binti, wewe unataka tukusaidieje Sheikh.
Nasubiria nikue, ili mikasa ya kipuuzi kama hii nione kama itanisumbua.
Huyu mwandishu wa story mzur...yan anakutamanisha uyajue yanayofuata...utasema riwaya
 
Nimeisoma story yoote, ukirudi uni tag mapema ili nitoe ushauri wangu.
 
Season 1 yote hadi imeisha unatongoza tu.
Watu tunatonatongiza episode ya kwanza tu tunapiga.

Kujichelewesha kutongoza huko ni kujichelewesha kukubaliwa upige au kujicheleweshwa kupigwa chini(kujipotezea mida).

Kama anaolewa na wewe upo ujue wewe ni fala maana yule mwamba ndo anaoa.

Ukija season 2 ujitahidi iwe nzuri maana season 1 umekuwa fala huyo.
 
SASA TUENDELEEEEE

Baada ya kutoka kuzungumza na uyo binti nilikua km plug azichomi ivi maana nilihisi moyo tu ndio unafanya kazi viungo vyote na akili vimesimama kwa kutokuamin yanayo tokea katika maisha yang ukumbuke tang tufahamiane na G ni miezi8 ilikua imepita ayo ndio yanaanza kutokea iyo siku ndio siku ya kwanza natumia pombe Kali konyagi maana sikutaka kukumbuka kitu usiku nakumbuka nililewa Sana na sikuweza kwenda nyumbani nilijikuata Niko kwenye chumba cha lodge Niko peke yang na kila kitu chang kiko salama na ni SAA4 asubuh wafanya usafi ndio wananiamsha nilijimwagia maji nikaenda home Ku change nikaenda shop nikafungua kisha nikaenda kwa G Niki taka kupata uthibitisho wa yale nilio yasikia kutoka kwa ndugu yake ,
Alinikaribisha huku km ajiamin ivi nilamsalimu baada ya salaam nikamuuliza kwanin? Amebadilika ukumbuke kipindi icho na simu na text zimepungua Mara apokee Mara asipokee ndivyo ilivyo kua basi tuendelee akasema amuna kitu ni u busy tu namimi sikumficha nikamueleza kila kitu nilicho elezwa kuhusu yeye mpka tarehe ya mahar na kunithibitishia alinyamaza kimya akanambia aliona Mimi nampotezea mda na sikua na mpango nae na tayar tulikua tushapanga mwaka unaofuata yaan 2017 ndio ndoa yetu akuwa na cha kusema ni aibu tu kwa hasira nikaondoka huku kichwa kikiwa na msongo mwingi wa mawazo nikiwaza nishamtbulisha kwa watu Wang wa karbu watanielewaje na alimanusura nmpeleke nyumbani nishaanza kuingia kwenye kamati za harusi mbali mbali nikijua yangu aiko mbali ivyo nianze kuchanga maana nitahtaji kuchangiwa na mimi ayo mambo yote yalinivuruga kichwa nikaona bora nilewe tu pengine Niko ndotoni nitazindika kutoka usingizini lakini aikua ivyo ,

Mipango ya harus iliendelea na wakafunga ndoa ya kihalali kanisa katoliki huku Mimi familia na jamaa wasijue kitu gan kimenipata duka nilimuachia yule dogo walevi ndio wakawa rafiki zang nakumbuka Mara kadhaa nilipelekwa na mama kuombewa kwa watumishi tofauti tofauti wakiamin nimelogwa kumbe G ndio ameniloga juhudi zote azikua na mafanikio mtaji uliyumba nikaanza kukopa kwenye taasisi na pesa izo akuna nilicho fanyia zaidi ya pombe mambo yakawa Magumu heshima yang nyumbani ikaisha nikabakia kuitwa mlevi sababu ya G ata marafiki nilio kua nao wakawa wananikwepa maana nilitoka kunywa henken,castle lite mpka kwenye pombe za karatasi au viroba,
Mambo yakawa magumu madeni kila kona na huku mikoan tunajuana Sana nikageuka story of the town watu wasijue kitu gan kimenipata,.

Ndani ya miez 8 nilikua nimetoka kwenye ujana mpka uzee ata ile sura yang ya ujana imepotea kila kitu ni kingine watu wanasema nimwlogwa,madeni yalinizidi nikakimbia mji ulikua mchungu nikaenda zang kwa bashite nikiwa sina hata nakumbika nauli ya kwenda huko niliuza laptop nilio kua naitumia chuo,.

Nilifika dar nikaanza maisha mapya kwa mkubwa Wang yeye ni mfanya biashara kko ivyo asubuh tukawa tunaenda nae na jion tunarudi lakin tayar nishakua teja maana mda wote nilikua alcohol na nikipotea kidogo tu nilikua naenda Ku charge betri.
Niliendelea ivyo ivyo na ayo maisha mpka siku Mungu alipo nirudishia akili zang Mimi mja wake nakumbuka iyo siku usiku sikunywa Sana ivyo ikapelekea usingizi kuisha mapema kwenye SAA8 iv ulikua umekata nikaanza kukumbuka mambo ya nyuma ikiwa ni mwaka umepita nikaangalia nilivyo kua na Sas NIKAAPA KUTOKUTUMIA POMBE TENA KWENYE MAISHA YANGU mwanzon nilipata shida maana nilikua nasikia kiu km mtu alieshinda kwenye jua siku tatu akifanya kazi ngumu bila kunywa maji ila hakika Mungu ni mwema alinisaidia nikaanza kwenda kanisan na kujitenga na marafiki walevi ambao ata dar nilikua nishakuaa nao,

Baada ya miezi mitatu nishakua na tabia njema wazazi na ndugu wakanichangia pesa nikafungua duka LA Viatu kkoo na maisha yakaanza upya,

UYU IBILISI WA KIKE sijui nan ! Alimwambia Niko sawa saaaiv akaanza kunitafta kuniomba msamah mi nikamuambia ujanikosea Kila mtu anachagua mtu sahii wa maisha yake ndio akaanza kunisimulia Analia jamaa yake alimdanganya anafanya kazi ofsi ya rais atamtaftia kazi BOT au wizara ya fedha kumbe jamaa ni mwalimu tena shule ya private alikua anaazima magar kwenda kwao G basi akaniomba nimsamehe na kwa kipindi icho G alivyo jua jamaa amemudanganya akavunja ndoa akarudi kwao ,tukawa tunasalimiana tu kawaida mpka mwaka huu Mwezi wa 1 alikuja dar kwenye harus ya ndugu yake akasema anataman afike kwangu maana nishatoka kwa bro najitegemea,

Ilikua siku ya jumamos nilienda kkoo. kwenye mishe zangu akanipigia simu mida ya saa8 anataka kuja home basi nikamwacha mshikaji makufuli jion atafunga mi nikaenda home Nikamuelekeza akafika nilikua nataman nimuone maana ni. siku nyingi na nilikua nampenda shida nijeraha moyoni alifika akashangaa kukuta Niko poa tu maana wanaume Kurudia khali yetu ni simple tofaauti na wanawake tulipiga story 2,3 mpka usiku ukaingia nasubr mtu aage sioni mtu km anadalili za kuondoka nikamwambia usiku unazidi kua mrefu naomba nikusindikize nashangaa MTU anaanza kulia nimsamehe kumbembeleza kujikuta tuko kitandani tunatinduana,

Akaa siku 2 lakini nishasema sito kaaa nirudiane nae uyo mwanamke alivyo toka tu nika mbolck akasafr kurudi mkoan na baada ya miezi mitatu Ananiambi anaujauzito Wang na awezi kuutoa ata km simpendi lakini atoi mimba Mimi nae nimemkaushia na nimebadili na namba Za simu maaana nikikumbuka aliko nipitisha naumia Sana aibu aliyo nipatia alafu Leo nimuoe apana acha tu abaki na mtoto wa makumbusho ameshaniaribia moyo wang iman sina tena tamani kuoa Ila yale matukio nikiyakumbuka moyo unasita na umri unasonga na Nimekua na tabia ya kuanzisha uhusiano na ghafla naanza kumchukia tena munisaidie nitafanyeje niweze kurudi hali ya mwanzo niweze kumuamin tena mchumba nitakae mpta MaanA km moyo wa kupenda sina tena
 
Aisee. Haya maisha haya. Anyway pole sana mkuu. Sina ushauri wa ziada aisee
 
Back
Top Bottom