Huyu dada nampenda sana.

Nina rafki yangu wa kike nampenda sana ila yeye kanipita miaka 2 ana miaka 28 sasa hv, kila cku huwa ananiuliza nitamuoa lini? Me najaribu kumpa sound cause ya umri wake, isingekua umri ungekuta nishamuoa, nataka kumtambulisha home ila najishtukia kuhusu age yake hiyo

Jamani miaka miwili si kama agemate tu? nilidhani amekupita 5-6 years?!!..hebu fanya kweli kama unampenda, age ain't nothing but a number..
 
Jamani miaka miwili si kama agemate tu? nilidhani amekupita 5-6 years?!!..hebu fanya kweli kama unampenda, age ain't nothing but a number..

Nafurahi bint anapokuwa na mtazamo huu kwani sasa inaonekana dhana hii huenda ikaisha,thanx Belinda!
 
Mi sidhani kama unampenda kweli, by the way miaka miwili ni michache mno, acha mbwembwe, endelea kushangaashangaa mwisho wa siku atakuja mwingine atasepeshwa, utalia ngelingeli.
 
Nina rafki yangu wa kike nampenda sana ila yeye kanipita miaka 2 ana miaka 28 sasa hv, kila cku huwa ananiuliza nitamuoa lini? Me najaribu kumpa sound cause ya umri wake, isingekua umri ungekuta nishamuoa, nataka kumtambulisha home ila najishtukia kuhusu age yake hiyo

Kama kweli unampenda age is just a number!!
 
Vuta mzigo huo! Cha msingi ni kama maeneo mengine yupo freshi. Tofauti ya miaka miwili siyo tatizo, suala kubwa ni tabia.
 
Unaoa umri au? mbona wengi tu wameoa wake waliowazidi umri, wewe unaonyesha hujaamua, better umuache binti wa watu kuliko baadae umsumbue kwa maneno ya kashfa, oh kwanza wewe ni dada yangu, oh oh, mwache aolewe na mwingine nawe tafuta unayemzidi kama unadhani ndio utakuwa salama!!!!
 
age matters jamani, wakati mshikaji anafika 40s mkewe atakuwa amefikia au anakaribia menopause na wanawake wakifikia umri huo mengi hutokea jamani.
lakini mm nna mke wangu mtarajiwa na tumezaa mtoto na kanizidi 5years na sijaona kama ni ishu coz i love her!
 
Fikiria tena kama unampenda. Unajua kama hakuna penzi la dhati utaona mengi si umri tu. Kuna wanaosingizia kabila, kazi, familia atokayo mwanamke etc. Lakini wakikaa chini waka dig deeper jibu ni kuwa there is no love bali mazoea. Sikushauri umuoe huyo dada kwani ndoa ni uamuzi unaotakiwa uwe bila shinikizo lolote; otherwise ndio hapo watu wanaanza kusema ooh ndoa za siku hizi, ooh ndoa ndoano. Listean to your heart. I think it is telling you she is not the one!
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Kma ungekua unampenda usingeona umri wake kama tatizo....bora utafute ambae hutasema ''asingekua hivi au vile ningemuoa''.
 
kwanini ulipokutana naye mara ya kwanza hukuona km umri is an issue to u?ss umefika wakati wa kumwoa ndo unaona age kubwa inaonekana ww hujatulia!
 
Nina rafki yangu wa kike nampenda sana ila yeye kanipita miaka 2 ana miaka 28 sasa hv, kila cku huwa ananiuliza nitamuoa lini? Me najaribu kumpa sound cause ya umri wake, isingekua umri ungekuta nishamuoa, nataka kumtambulisha home ila najishtukia kuhusu age yake hiyo

mpotezee,mkubwa sana kwako huyo,utamuoaje bibi chalii angu!? We wa kishumundu nini?
 
Nina rafki yangu wa kike nampenda sana ila yeye kanipita miaka 2 ana miaka 28 sasa hv, kila cku huwa ananiuliza nitamuoa lini? Me najaribu kumpa sound cause ya umri wake, isingekua umri ungekuta nishamuoa, nataka kumtambulisha home ila najishtukia kuhusu age yake hiyo

Unajua unachokitaka? Mwache dada wa watu atafute atakeyemfaa. If you love her, then do so without any reservation au mwache tafuta unaoyeona anakufaa kiumri. Otherwise, huko baadae umri utaweza kuja kuleta matatizo.
 
Kwani ulipoanza kumtongoza ulikuwa hujui umri wake?acha kuchezea wasichana,unajua kuna watu kama wewe wanawapa girls wakati mgumu,halafu unampa muda wa kukusubiria then anakusubiri na bado humwoi unampotezea tu mda wake wa nini?acha kuchezea feelings za watu kutimiza haja zako,nye ndo wale mnasababisha mimba halafu mnaacha girls njia panda
 
Usituchanganye hapa,inaonyesha wewe ni msanii tu,na wala si mpendaji.ungempenda usingejali hilo.
 
Back
Top Bottom