Mwanabalagha
Senior Member
- Nov 11, 2015
- 196
- 235
Habari za saa hii wananzengo...?
Kiufupi ni kwamba, miaka miwili nyuma kuna msichana mgeni nilimuona mtaani kwangu.Sasa baada ya kupeleleza nikaambiwa amekuja kumtembelea dada yake hapo mtaani, kwasababu aliyavuta macho yangu moyo nao ukataka kutoka kumfuata lakini bahati mbaya ukakwama kwenye kifua hivyo ikabidi urudi tu ndani ukaendelee kuugulia maumivu polepole.
Kiukweli ni msichana ambaye kama wewe ni mwanaume halafu ukakutana nae njiani,usipogeuka kumuangalia tena lazima utakuwa mchawi tu.Nilitokea kumpenda kiukweli...nikaanza kumchombeza taratibu huku nikizingatia vigezo na masharti nisije kuharibu.
Kwa bahati mbaya kabla hatujaelewana vizuri akawa amerudi kwao Babati.Sasa tukaanza kuwasiliana akiwa mbali, na bahati nzuri dada yake alikuwa anajua kinachoendelea hivyo nae akawa anasaidia kumchombeza mdogo wake anikubali arudi huku bongo.
Baadae nikakata tamaa kabisa manake yule msichana alikuwa akiniambia nakuja tarehe fulani....lakini tarehe ikifika haji aliniahidi zaidi ya mara nane kwamba anakuja ila hakufanya hivyo.
Ndipo siku moja nikiwa sina hili wala lile huku nikiwa nimekata mawasiliano nae kabisa, siku hiyo dada mtu alikuja ofisini kwangu na kuniambia kwamba yule binti atakuja kusherehekea sikukuu ya xmass huku hivyo nikae tayari.
Na kweli baada ya siku kama tatu mbele yule msichana akaja....alipofika tu akanitafuta tukaonana na mambo yakaanzia hapo na yakaendelea na mpaka sasa bado yanaendelea.
Kiufupi nimeshamtolea barua bado mahari, sasa dada mtu alimwambia aje tu kwangu aishi wakati anasubiria mahari...kweli binti akaja kwangu tukaanza kuishi huku dada mtu akiwa anakuja siku mojamoja kututembelea hapo nyumbani, cha ajabu sasa huyo dada mtu kabadilika kawa kama anayeona wivu vile mi kuwa na mdogo wake ,mara anamwambia hivyo vihela vya mmeo vitaisha tu we jifanye kuringa kwanza rudi nyumbani mpaka utolewe mahari... bint akaja akanieleza nikamwambia ok! mwambie dada mahari nitaleta baada ya wiki mbili....na umuombe uendelee kukaa huku siku mahari ikikaribia unarudi nyumbani.
Alivyomueleza hivyo akakubali na akamruhusu kuja kukaa nami, cha kushangaza baada ya siku mbili kabadilika tena amempigia simu mpaka baba akamueleza kuwa mdogo wake hayupo pale nyumbani kwake na hajui alipo na kaka yao akamwambie vivyo hivyo wakati anajua yupo kwangu...baba kapiga cm kamwambia afungashe vilago arudi nyumbani....sasa nashindwa kumuelewa huyu dada mtu anataka nini!!!