Huyu Cloudflare Ni nani?

Determinantor

Platinum Member
Joined
Mar 17, 2008
Posts
61,488
Reaction score
100,883
Yaani kila niki-browse JF naletewa error 400 na kuna hayo maandishi ya Cloudflare (sp) hadi naboreka, inapatikana zaidi nikitumia simu. natumia HTC-HD7 ndio tatizo au kuna la zaidi? Nisaidieni wadau
 
ntajinyonga jamani, kha nakosa uhondo mioe, nawezaje kuondoa hii error 400 jamani? haya wanasayansi naombeni mkuje kwa huku mnisaidie
 
Hebu waheshimiwa nisaidieni na natumia line ya Vodacom, seems hili tatizo nalipata zaidi nikifungua JF, ni mimi tu au kuna wengine pia? je dawa yake ninini?
 
pole sana mpwa, ngoja wataalamu wa IT waje wakusaidie.
 
Hiyo imewekwa na haohao wataalamu wa JF. Inawasaidia kupambana na hackers au watu wabaya wanaotaka kuharibu system zao. Kwenye maelezo yanayokuja angalia kuna option ya kuingia na utaendelea ku browse JF kama kawaida ila hautakuwa kwenye desktop mode kama simu yako ni smart phone. Mimi huwa inatokea ni kiwa natumia smartphone lakini nikiingia kwenye hiyo option tu mambo yanaenda poa. Ufafanuzi hapo juu niliuona google. Kama kuna ufafanuzi zaidi tuongezeane ujuzi.
 
Huwa inatokea website inapokuwa down, hivyo unaweza kuendelea kubrowse pages za jf ambazo zipo stored na cloudflare, pindi site inapokuwa stable hilo lazima lisitokee. Ikikutokea hivyo siku nzima wafahamishe jf kwa njia ya facebook au twitter.
 
wakati mwingine huwa napata message 'the web site is unreachable.
 
inanitesa sana hii kitu,nilifikiri ni browser ninayotumia opera classic kumbe ni wengi. aaaaaah mods toa hii kitu bana inatuzinguaaaaaaaaaaa!over
 
Huyo ni Mwigulu Nchemba anaficha aibu ya kushindwa Arusha licha ya kutumia mahela mingi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…