Huyu binti kanikera naomba ushauri

mapenzi ya small house yana wivu mkali kuliko yale ya nyumba kubwa au ulikwa hujui hilo..

Ni kweli si unajuwa tena vigharama vyake. kodi ya nyumba, transport, simu, outing, pocket money etc
 
Kadiri siku zinvyokwenda usaliti wa ndoa unazidi kuwa jambo la kawaida sana. Dhamira za wengi wetu hazipo hai tena, hata roho haziumi tunavyofanya vitu vya kiovu namna hii kwa ndoa zetu, bila aibu tunaomba na ushauri kabisa namna ya kumiliki nyumba ndogo vizuri.

Mwili si wa kuuamini sana mahitaji yake na tamaa zake. lazima tujifunze ku-argue na tamaa za miili yetu. Wengi wetu tumekuwa shuleni kwa miaka takribani 20 tukinoa bongo zetu, nini faida yake kama tunatekwa na tamaa za miili teyu kirahisi rahisi? tumekua watumwa sana wa miili yetu, akili tumepewa za nini? kufikiri tumepewa kwa nini?
Usipokuwa mwaminifu kwa KIAPO cha ndoa yako, utawezaje kuwa mwaminfu kwa mengine?
 
mwache binti wa watu apate wake wa kumuoa. wewe nenda katulizane na mkeo.kwanza utkuwaje na wivu kwa vitu vya kuiba.

Mimi sina shida ila kumsaidia ni lazima, yeye angekuwa na mchumba m1 sawa. sasa wachumba wa2 na mimi wa3
 
Kwa mtazamo wako,kuna hoja jadilifu kweli hapa? Kuwa serious hata kidogo...
 

TIZED asante sana kwa ushauri na unayosema yote ni kweli lakini sisi binadamu ni wazaifu sana ninadhani unanielewa
 
Mimi sina shida ila kumsaidia ni lazima, yeye angekuwa na mchumba m1 sawa. sasa wachumba wa2 na mimi wa3
umsaidie nini?unashindwa kusaidia ndugu zako na familia yako?wewe ni king'amuzi chake kwasasa hamna zaidi.ukilikwaa gonjwa utatia akili
 
tuko wangapi?chukua hatua,ndugu yangu ilinde familia yako achana na huyu binti ili utulie na mkeo na umuepushe na UKIMWI.
 
TIZED asante sana kwa ushauri na unayosema yote ni kweli lakini sisi binadamu ni wazaifu sana ninadhani unanielewa
evelyne salt,Lara1,gfswin,kaunga mko wapi mujadili hii kitu hapa? allllah mukimya tu.....jamaahataki stress za mama watoto wake ndo maana kajichagulia kadumu ingawa kanataka kumzingua,anasema pia vijana anawaonea huruma kama wataoa kwani wao wazee wanatunza vyema halafu ndo wanakimbiliwa na hawa bi dada....akina bujibuji,Rutashobolwa,wadau watu 8,Mtambuzi kumbe hii kitu inasaidie kupunguza stress za ndanieeeee.mama akikunyima mzigoeeee
 
Nashukuru kwa ushauri niliopewa na JF and I have made up my mind huyu binti ni MALAYA na simtaki tena, ngoja aendelee na umalaya wake na mimi nimeamua kutulia na mke wangu. Nitaungama dhambi zangu na najuwa Mungu atanisamehe.

Ushauri wazee wenzangu tusihangaike na hivi vibinti ni pressure tu na kutafuta magonjwa.
 

Kama mtu vile!na iwe kweli

Mkuu,sasa nduka original ndio huyu yule mwingine ni nduka babu mzinZi!!!!
 
Karibu sana Mkuu, Ila kukiri udhaifu ndio udhaifu wenyewe kaka. ukikiri udhaifu inakupa kitu cha kujitetea nacho kuhalalisha uovu flani ambao mwili utakutuma kuufanya. Then utasema tu sisi ni wadhaifu, na utakuwa umeridhika rohoni.

Mimi ni muumini wa kila kitu kinawezekana ukiweka nia thabiti. na huwezi weka nia mahali ukakosa njia hata mara moja.(nina expeience nayo sana) wengi tunashindwa kwa sababu ya woga wa vitu visivyojulikana na vitu vyenyewe havipo. kabla ya kuanza mtu anashindwa. Pia naamini maisha ambayo hayana changamoto (pamoja na za kimwili) ambazo napambana nazo na kuzishinda hamna cha kujivunia na kufurahia. lazima kuwe tofati kubwa sana kati ya kitu kinachofikiri na kisichofikiri.

TIZED asante sana kwa ushauri na unayosema yote ni kweli lakini sisi binadamu ni wazaifu sana ninadhani unanielewa
 

we endelea kutia tu hata wew c umawako mke bado unataka vya nnje basi nayeye pia mwache apate nje anatafuta wa kumuoa bado akipata hopefuly atapunguza list
 

Ni kweli kaka na nina uhakika nitamshinda shetani, ni mambo ya kishenzi sana na ninadhani Mungu kaamua kunionyesha kinyume na hapo ningekuwa naona kawaida tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…