Kusini kuchele
Senior Member
- May 21, 2023
- 121
- 687
Nimesikiliza sana ila sijaelewa, nikasema pia na machapisho bado sijaelewa... means waendelee kuandamana au kudai vipi? Wapi? Tuseme Leo askofu amekuwa disappointed kwa watu kutoandamana? 🤔Tuendelee kutafakari lengo lao, huku papa anasema msitumie dini.... 🙌
ASKOFU AWAHIMIZA WAKRISTO KUDAI HAKI
Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mhashamu Jude Thaddeus Ruwa’ichi, amewahimiza Wakristo kuwa wadau wa haki akisisitiza kuwa “hakuna amani ya kudumu bila haki.”
Akihubiri wakati wa mkesha wa Krismasi, Askofu Ruwa’ichi alisema, “Sisi sote kwa nguvu ya ubatizo wetu tunaitwa tuwe watu wa haki… haki ni kutambua mastahili ya wengine na kuyaheshimu.”
Aliwakumbusha waumini kujitathmini kwa kuuliza, “Ewe mwana wa Dar es Salaam, ewe Mtanzania, je wewe ni mtu wa haki?”
#MerryChristmasEveryone