Huyu askari atachukuliwa hatua gani?

Huyu askari atachukuliwa hatua gani?

Hili si jambo lililowahi kufanywa na askari wetu yeyote siku za nyuma. Ni jambo la kushangaza kabisa kwa askari kujirekodi na kurusha maneno kama haya kwenye mitandao ya kijamii.

Nina wasiwasi inawezekana huyu kijana asiwe ni askari. Inawezekana ni kijana anayeishi kwenye nyumba ya askari magereza akaamua kuvaa magwanda na kufanya jambo hili. Jeshi letu la magereza itabidi lichunguze jambo hili kwa kina kwani si kila mtu ni msemaji wa jeshi hilo. Majeshi yetu kama zilivyo taasisi, idara za serikali na mashirika ya umma zinao wasemaji maalum ambao wanatambulika. Jeshi letu la wananchi linaye msemaji wake na kama ikibidi mkuu wa majeshi (CDF) mwenyewe hutoa taarifa kwa umma kulingana na uzito wa taarifa husika. Jeshi la polisi lina ye msemaji wake na pia makamanda wa polisi wa mikoa au kanda maalum ndio hutoa matamko na kama ni jambo lenye uzito mkubwa msemaji huwa mkuu wa jeshi hilo (IGP) mwenyewe. Vivo hivyo kwa idara nyingine kama za Uhamiaji n.k.
Na kama ikithibitika kuwa ni kweli huyo kijana ni askari magereza basi itabidi ahojiwe ili aeleze ni nini kimemsukuma atoe matamko hayo na kuyasambaza. Wananchi tunaweza kuanza kuamini kuwa labda ametumwa afanye hivyo kwa sababu maalum. Yaweza kuwa magereza yamejaa hivyo anatuma ujumbe kwetu kutuasa tuwe raia wema ili kupunguza mrundikano kule. Lakini vile vile kama pia ni askari wa jeshi la magereza basi itabidi jeshi litathmini mafunzo wanayowapa vijana wake. Mimi nimeona huyo kijana hajaiva kinidhamu binafsi (he is lacking self discipline). Askari aliyeiva si mropokaji kama huyo. Hasa anapozungumzia matumizi ya risasi na bunduki kuvunjia miguu na kutawanya ubongo! Hayo hayapaswi kuzungumzwa na askari aliyepewa silaha ili kulinda raia na kuhifadhi amani na utulivu. Matumizi ya silaha za moto ni jambo la mwisho kabisa ambalo askari hufanya kwa mhalifu na sio kama anavyojinasibu huyo kijana. Pia anapaswa afahamu kuwa sisi wananchi walipa kodi ndio baba zake na mama zake tunaomlipa mshahara na posho zake. Anasema risasi anapewa na serikali! Serikali ni ya wananchi. Risasi zinatengenezwa pale mzinga Morogoro lakini hiyo bunduki anayotutisha nayo kama ni SAR au ni SMG zinaagizwa nje ya nchi kwa kodi tunazolipa sisi wananchi. Hili jambo linapaswa kukomeshwa kwa kweli kwani kesho anaweza kutokea askari mwingine ambaye siye msemaji rasmi wa taasisi husika akatoa matamshi yanayoweza kuleta taharuki kubwa kwa jamii.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Conclusion.. case closed

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nikadhani ukisha kuwa kwenye sare ya serikali kuna baadhi ya maneno hayatakiwi kutoka kwenye kinywa chako, lakini dogo anadiriki kusema mmy..
 
Back
Top Bottom