Huwezi kumuhusisha na rushwa hata kwa bahati mbaya!!!!!

NAFTAL DANIEL

Member
Nov 14, 2012
27
0
Kama CCM wanatumia nguvu nyingi kiasi hiki kumchafua DR, W.P.SLAA tena kwa propaganda ya kipuuzi kabisa, eti kuwa anakadi mbili basi ni wazi kuwa mzee huyu ni mwadilifu, mzalendo na mwenye uwezo mkubwa wa kuiongoza nchi hii. Kwani ni wazi hiyo ndo ajenda na karata muhimu ya sekretariat mpya ya ccm ikiongozwa na bwana Kinana na hii inatudhibitishia kuwa chama hiki hakina dhamira ya dhati ya kuwatumikia wananchi kwani tulitegemea watumie front page za magazeti kuonyesha na kuhusianisha miaka 52 ya uhuru na kiwango cha maendeleo tulichopiga sambamba na rasilimali zilizotumika, pia kutupa mustakabali wa siku 90 za kuondoa wezi na mafisadi ndani ya ccm '' kuvua magamba'' ajenda hii muhimu kwa maendeleo ya nchi yetu imefikia wapi, badala ya kuja na hoja ya umoja dhidi ya magamba na waliojiita wapambanaji wa ufisadi yani umoja kati ya wezi na wanaosemekana ni waadilifu. Wakati huo huo NAPE akitueleza anawezaje leo kuzunguka mikoani jukwaa moja na aliowaita wezi ,mafisadi wahujumu uchumi na kusimama kidete huku akitangaza kuwafukuza CCM ndani ya siku 90 . kwani ukweli ni kwamba pamoja na kuwa chama tawala ,kumiliki majeshi yote na usalama wa taifa lakini wameshindwa kubaini mapungufu ya kiamaadili,uzalendo na falsafa ya uongozi ya DR, W. P. SLAA NA WAKAISHIA KUPIGA MAYOWE eti anamiliki kadi 2.Na wakawekeza pesa nyingi kwa kununua front page za magazeti na kuitoa kama habari kubwa na muhimu sana wakidhani ndio majibu ya matatizo ya watanzania waliokata tamaa na kujiona wakimbizi ndani ya nchi yao . Hii inatufanya tuamini kuwa DR, SLAA HUWEZI KUMUHUSISHA NA RUSHWA HATA KWA BAHATI MBAYA!!! .Na sifa kubwa aliyo nayo DR,huyu wa ukweli ni kwamba moral authority yake iko juu sana kwa sababu anaongozwa na uadilifu,utaifa na uzalendo kuliko maslahi binafsi ,tunahitaji kiongozi kama huyu ambaye credibility yake haijawahi kuwa na shaka. Kwa kumalizia naomba kumnukuu DR, KITILA MKUMBO ktk moja ya makala zake ndani ya wiki hii anasema ''KIONGOZI YOYOTE WA UPINZANI ANAYESIFIWA NA CHAMA TAWALA HAFAI'' ,Hivyo basi kwa mujibu wa wa DR, KITILA MKUMBO tutegemee matusi,kashfa,na propaganda nyingi dhidi ya RAIS HUYU ANAYETAWALA MIOYO YA WATU TOKA KWA HAWA WEZI WA RASILIMALI ZETU KWA MDA MREFU SASA IKIWA KAMA KIPIMO CHA UIMARA WAKE NA UBORA WAKE KAMA KIONGOZI MZALENDO NA MWADILIFU ALIYETUKUKA ANAYEKOSA HATA WA KUMNYOSHEA KIDOLE KUTOKA KUNDI LA WEZI NA WAHUJUMU WA MAENDELEO YA NCHI YETU.
 

Kichuli

JF-Expert Member
Apr 23, 2012
320
0
Dr slaa amemuacha yule mama au bado anaye na je ile kesi ya mke wake halali imeishia wapi tunaomba mtuambie jamani maana huyu mzee tuna mheshimu sana!!!!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom