Huwezi kumshinda adui usiyemjua

Huwezi kumshinda adui usiyemjua

Right Marker

Senior Member
Joined
Apr 30, 2018
Posts
194
Reaction score
624
Itakupa shida kutibu maumivu ya miguu kwa kunywa dawa za malaria. Ni ngumu mno kumshinda adui usiyemjua.

Huenda ukawa unajiuliza maswali:- Nani anayevuruga mipango yako - Nani anayevuruga ndoa yako - Kwa nini bosi wako anakuchukia sana - Kwanini kazini kwako hupati fursa kama wenzako.

Jaribu kumjua adui yako ili umshinde. Mara nyingi adui huwa hatoki mbali, ikiwa atatoka mbali basi kibaraka wake ndo atakuwa karibu yako. Adui anaweza kuwa ni binadamu au hali iliyopo ndani ya nafsi yako.

1. ADUI BINADAMU - Unashauriwa kuwa macho na watu wa karibu yako (Never put too much trust in friends). Lakini pia katika kujitafuta kwako usipende sana kuwa mtu wa kusubiri kutafuniwa chakula na wenzako ili umeze, siku moja utatafuniwa chakula chenye sumu. Kama unajenga mji wako usiwaamini sana mafundi kwa kuwaachia uhuru, watakuibia...Kama unatafuta kazi nenda wewe mwenyewe kwa Afisa Mwajiri, usitume mtu...Kama unahitaji kuomba msamaha kwa bosi wako uliyemkosea; nenda mwenyewe, usitume mtu.

2. ADUI WA NDANI YA NAFSI YAKO - Mjue adui wa ndani ya nafsi yako unayemlea wewe mwenyewe ili uweze kumshinda. Wapo watu ambao wanakwamishwa na uvivu, kukata tamaa, kuahirisha mambo pasipo na sababu, hofu, wasiwasi, jeuri, majivuno, nidhamu mbovu kwa watu, n.k, ikiwa umegundua hao ni maadui wako chukua hatua.

HUWEZI KUMSHINDA ADUI USIYEMJUA;
By: RIGHT MARKER - TZ
Sept 16, 2024
 
Back
Top Bottom