Shebbydo
JF-Expert Member
- Feb 12, 2015
- 1,174
- 1,937
Habari wana JF,
Baada ya serikali kuagiza sukari na jana kiasi fulani kuwa kimeingia katika mikoa mbalimbali kwa bei elekezi kama ilivyoelekezwa, nilijua sasa tatizo limekwisha. Tatizo ambalo linaleta taharuki kubwa kwa Watanzania.
Niliyoyaona jana kwenye duka moja la jumla la Mhindi yamenivunja moyo kabisa juu ya mafanikio ambayo niliyatarajia kwa utawala huu usiyokuwa na simile kwa maovu. Nilienda dukani hapo na rafiki yangu alienda kununua sukari kwa ajili ya duka lake. Sukari kilo 50 imeuzwa kwa Tsh.135000/=, inamaana rejareja iuzwe sh.3000/=.
Mchezo ulivyokuwa unafanyika ni "urushaji"(neno hili lilitumika miaka ya nyuma wakati bidhaa kama sukari, sigara na nyinginezo zilipokuwa adimu. Wavuta sigara walikuwa wanauziana kwa "pafu"). Risiti ilikuwa inaandikwa elfu 95 halafu Mhindi anapokea 135000, anakuambia wewe ni mfanyabiashara utajua mwenyewe utauza je.
Sukari hiyo kufikia saa 12 ilikuwa imeisha, wafanyabiashara wa jiji la Mwanza bado wanahaha kutafuta sukari. Mimi nikajiuliza maswali ambayo sikupata majibu. Serikali ilisema sukari hiyo itauzwa rejareja sh. 1800, ambapo kilo 50 isingezidi sh. elfu 70, Sasa bei ya risiti ilikuwa elfu 95, rejareja kilo moja iuzwe 2000, je ni nani anayewasaliti Watanzania? Jumlisha cha juu Mhindi alichokuwa anaweka, utake ununue usitake uwache, mtaani ikiuzwa kilo 3000 Wananchi wataielewa je serikali? Utaratibu wa kuipata hiyo sukari iliyoletwa na serikali upo je?
Wakuu na nyinyi mnaweza toa mawazo yenu, mimi kwangu naona nchi hii ilishaharibika labda zitungwe sheria za kunyonga, kutumbua majipu tu haitoshi.