Huwezi fananisha Nyerere na Magufuli hata kidogo

man-eno

Member
Sep 20, 2015
13
62
HUWEZI MFANANISHA NYERERE NA MAGUFULI HATA KIDOGO.
Nyerere alijenga mabwawa ya kufua umeme Kidatu, Kihansi, Nyumba ya Mungu, Hale
Nyerere alinunua ndege na ATC ikafanya biashara katika soko la ndani/kimataifa
Nyerere alijenga UDSM, Mzumbe, NIT, Dar Tech, Arusha Tech, Mbeya Tech, IFM, CBE, TIA/DSA, DMI, ISW,
Nyerere alijenga madaraja makubwa kama Kirumi, Selander, Wami, Mara na mengine mengi.
Nyerere alijenga viwanda vya kuchakata mazao ya Pamba, Kahawa, Pareto, Chai, Ngozi, Nyama, Maziwa, Viatu,
Nyerere alinunua Meli na vivuko (Panton) katika maeneo kadhaa nchini
Nyerere alijenga viwanda vya kutengeneza Vifaa/Zana za kilimo, Mbolea, Madawa, Magurudumu, n.k
Mwl. Nyerere alijenga viwanda vya Korosho.
Nyerere aliwapenda Wananchi wake.
Nyerere aliwasomesha watoto wake Shule za Serikali
Nyerere hakudhulumu Wananchi wake.
Nyerere Alituunganisha Wananchi, hakuwa na Ubaguzi hata kidogo.
Nyerere hakutumia Dola kutesa Wananchi
Hakutumia mabavu kubomolea Wananchi makazi yao.
Nyerere Aliheshimu mihimili yote. Sio km huyu "Mahakama ilitoa Injunction ubomoaji wa makazi ya Wananchi lkn,aliikataa".
Nyerere aliwatafutia Wananchi wake Chakula waliposhikwa na njaa.
Wakati wa Nyerere wanafunzi walisoma na kusafiri kwenye usafiri wa umma bure.
pia baba wa taifa alifanya na mengineyo mengi kama watanzania kupelekwa nje kusoma aijalishi kabila wa dini gani.
alijenga uhusiano na mataifa yote bila mipaka.
alisaidia ukombozi wa bara la Africa.
wanafunzi wa mbali kama Mtwara tech,manghamba high school, bukoba na kwingineko walipelekwa na usafiri wa ndege ya serikali bure.
wanafunzi walikula kuku mara tatu kwa wiki zikisafirishwa na ndege kwa maeneo ya mbali.
alijenga viwanja vya michezo nchi nzima kama jamhuri stadium, dodoma,arusha,kirumba,tabora,shinyanga sokoine stadium mbeya n.K.
alijenga mashirika na taasisi kama sukita,national milling co.,rtc,ugavi ,twico, tanganyika packers,shirika la usagishaji la taifa, posta na simu ,bank za ujamaa, n.K.
pia alitoa vitabu bure mashuleni kama michezo na utamaduni.
mashirika na taasisi zilikuwa na timu zao.
Viwanja vilijaaa ila kwa sasa idadi ya watu imeongezeka na bado viwanja havijai.
alianzisha national festival kila mwaka ngoma za makabila kushindana.
aliendeleza vijiji na azimio la arusha.
alijenga chimwaga Dodoma ,ukumbi wa mikutano mikuu ya taifa Dodoma.
alitoa chakula cha msaada bure wakati wa njaa 1986's.
alitembelewa na kina fidel castro, keneth kaunda,dos santos ,malkia wa uingereza,n.K

Kuombwa ushauri

Je, kweli kuna zaidi yakee..?

na utofauti mkubwa kuliko wote:

Badara ya reli ya tazara kuelekea mara (butiama) kwa hekima zake aliipeleka kusini.

Alijua muhimu wa viwanja vya ndege ila akujenga mara (butiama).

Na kubwa zaidi yote aliyofanya nyerere alisema tumefanya. Badala ya nimefanya.

Huwezi kufananisha na nyerere

hakuwa feki alichosema ndicho anatekeleza pia alisaidia kulinda mipaka dhidi ya nduli idd amin dada huko kagera
Nyerere alijenga Reli ya TAZARA
Nyerere alijenga vijiji vya Ujamaa nyerere alijenga Umoja wa Kitaifa yaani lugha moja Nyerere hakuwa Mbaguzi wa Kisiasa Nyerere alikaa madarakan kwa faida
Pamoja na mambo mengine kede kede ambayo alifanya lakini bado aliamini kuwa wapo watakokuja kufanya zaidi ya yeye.!
Naichukia hii tabia ya kinafiki,kama Nyerere ambaye ndiyo baba wa Taifa hakuwai kusema eti akitoka nani atafanya kama yeye ,wewe ni nani hata useme hivyo??tuwe na staha na akiba ya maneno kuna watu wengi tu Tanzania wanaweza kuongoza Mungu akiwaongoza...
Lakini bado Nyerere aliondoka madarakani kwa hiari yake mwenyewe (kung'atuka) na hakuogopa ama kuhofia kwamba akiondoka madarakani ni nani atafanya kama yeye!
Vimbwanga mlotaaka kuaminisha Watanzania kwamba hakuna mwingine mwenye uwezo wa kufanya kama Magufuli yanatokea wapi?

Mjukuu.
 
HUWEZI MFANANISHA NYERERE NA MAGUFULI HATA KIDOGO.
Nyerere alijenga mabwawa ya kufua umeme Kidatu, Kihansi, Nyumba ya Mungu, Hale
Nyerere alinunua ndege na ATC ikafanya biashara katika soko la ndani/kimataifa
Nyerere alijenga UDSM, Mzumbe, NIT, Dar Tech, Arusha Tech, Mbeya Tech, IFM, CBE, TIA/DSA, DMI, ISW,..
Tatizo ni ushamba wa viongozi ambao hujiuna malaika na welevu kuliko wengine. Hata mawaziri wake wengi tu waliiga tabia ya kuponda watangulizi kitu ambacho si chakiugwana. Hakuna excuse rais au mawazili kutimiza wajibu wao. Lakini walitaka misifa ya hovyo ili kuficha mapungufu yao.

Ukiona kiongozi anatowesha transparency huyo ni muoga wakukusolewa na hafai kuongoza watu maana nchi itaongozwa kwa mawazo yake. Huu ni muda wakuwa pamoja tusahau maumivo tuliyopitia ya kuitwa wanyonge kwenye nchi yetu wenyewe ambayo babu zetu waliipigania kwa jasho na damu.
 
Nyerere alitawala kwa kipindi gani? Umesahau ya ujamaa? ya uhujumu uchumi? kifo cha sokoine? Umesahau zama za kuchapwa viboko hadharani?

Tanzania Rais Moja tu wa maana na huyo ni Mzee mwinyi. Hawa wengine wote hovyo tu.
 
Nyerere alitawala kwa kipindi gani? Umesahau ya ujamaa? ya uhujumu uchumi? kifo cha sokoine? Umesahau zama za kuchapwa viboko hadharani?

Tanzania Rais Moja tu wa maana na huyo ni Mzee mwinyi. Hawa wengine wote hovyo tu.
Mwinyi?😳😳😳😳 Acha masikhara. Wewe ulikuwa mdogo umekuja kumsikia sikia tu mwinyi. Huyu ndo alianzisha biashara ya kuuza wanyama wetu na mbuga zetu ...
 
Lilianza kujengwa awamu ya mwaka 1980 na kumalizika 1985 na tar 14 oct mwaka 1985 lilifunguliwa na kuanza kutumika sikumbuki lilifunguliwa na nani unaweza nisaidia
OK mwenyewe nilikuwa sielew. Labda mie nazungumzia lilipojengwa kwa awam ya pili.
 
Hadithi hizi zinachosha!

Nyerere alitawala kwa kipindi gani? Umesahau ya ujamaa? ya uhujumu uchumi? kifo cha sokoine? Umesahau zama za kuchapwa viboko hadharani?

Tanzania Rais Moja tu wa maana na huyo ni Mzee mwinyi. Hawa wengine wote hovyo tu.
Ni vigumu kumfananisha muasisi wataifa na viongozi wengine lakini pia ni vizuri kuwatambua viongozi wengine kwa utumishi na mchango kwa Taifa.

Kila zama na kitabu chake mwinyi alishasema rejea hutuba nyerere alikuwa hapondi wenzake ili alikemea maovu nanukuu 'tulikuwa wakali kukemea rushwa''.

Sasa nyie mnajiita wazalendo uchwara mnataka misifa na propaganda za hovyo wakati mnatimiza wajibu wenu. Kinaya zaidi mlitumia MEDiA BIAS kujifanya special kumbe mnaficha mapungufu yenu. Weka transparency tujue mbivu na mbichi
 
Nani anabisha nyerere hakufanya kazi? Muwege mnachangia kwa kutumia akili sio mihemiko.

Nyerere alitawala more than 20 + yrs kwa nini asifanye hayo yote uloyataja?

Magufuli miaka mitano, aliyoyafanya ndani ya muda mfupi nayo yanaonekana.

Kila mutu asifiwe kwa kazi wake.
 
HUWEZI MFANANISHA NYERERE NA MAGUFULI HATA KIDOGO.
Nyerere alijenga mabwawa ya kufua umeme Kidatu, Kihansi, Nyumba ya Mungu, Hale
Nyerere alinunua ndege na ATC ikafanya biashara katika soko la ndani/kimataifa..
Well said
 
Mtu wa pwani ukimsifia Nyerere ananuna wanamuita majina ya hivyo utasikia mchonga haambiliki nk
 
Back
Top Bottom