Huwa unasolve vipi hii tabia ya wapangaji wenzako?

kingkongtz

JF-Expert Member
Dec 28, 2019
1,023
3,458
Wakuu salama?

Katika maisha yote ya upangaji hamna kitu kinanikera kama baadhi ya wapangaji kufungulia subwoofer kwa sauti kubwa.

Hii kiukwel huwa inanikata stimu, inafikia ile time ya kurud magethon huna hamu kwa sbb ukiingia tuu utafikir umetoka kanisan unaingia disco.

Kuna mwanamke mmoja amepanga chumba kinachokaribia na chumba changu, anafujo huyo mama kwa upande wa mizik alaf kibaya zaid n taraabu mwanzo mwisho na nyimbo zote za kusutana

Juz mzee wangu alipita kwangu akiwa ametokea mkoa fulan akaona aweke kambi kwangu kwa siku moja, usiku tumelala yule mwanamke kafungulia subwoofer volume 52+, mzee wangu akaniuliza kijana wangu zile simu za usiku tunazowasiliana nakuuliza upo club kumbe ndo hivi, nilijiskia vibaya sana.

Asubuh yake tumeamka ding akaendelea na safar nikamfata yule mwanamke nikamchana akaenda kupunguza, lakn nilirud mchana nikakuta vile vile yaan.

Nilishajaribu kuongea na baba mwenye nyumba akanijibu hat yy ameshapiga kelele kuhusu wapangaji kupiga miziki kwa fujo lakn huyo mwanmke hasikii.

Hapo nyuma kabla hajaja huyo mwanamke kulikuw shwari kabsaa.

Niliwaza sijui niwe naacha nimefungulia SEA PEANO yangu niweke full bass volume 60(simnaijua sea peano inaweza angusha ukuta)

Nawaza niwe nafanya ivo nafungulia SEA PEANO nafunga chumba natimkia job af niwe narud night sana.

Wajuba nyie huwa mnaikabili vipi hii situation.
 
Mkuu na wewe ni kuweka volume mwisho, mi apa ninao wawili wana vimichina wanafungulia vinabaki vinakoroma ko mimi na SEA PEANO (nadhani ni mchina pia) nikikiwasha lazima wasikilize ngoma zangu.. Sema nini mm nawawekeaga ngoma kali kali tu latest ko wanainjoy:)
 
Kwanza huo ni ushamba, kuna siku nimewah kuzima main switch (kwa wahenga zile main switch za zaman mtakua mnazipata. Zile za kuchomoa). Kam ni usiku nachomoa alf nalala, kama ni mchana nachomoa alaf naondoka

Badae wale majamaa wakachoka ile tabia ya umeme kukatik hovyo wakaondoka. Siku hizi najifunza kukata umeme chumba cha muhusika mwenyew bila kutesa wengine
 
Nlivokua chuo hilo tatizo lilikuepo sana Download app inaitwa sleep sounds, inasauti mbalimbali. Me nlikua naweka sauti ya mvua alaf nacoonect na bluetooth speaker alaf unaweka volume adi mwisho. Usiku unalala usingizi mzuri tu.
 
Kwanza huo ni ushamba, kuna siku nimewah kuzima main switch (kwa wahenga zile main switch za zaman mtakua mnazipata. Zile za kuchomoa). Kam ni usiku nachomoa alf nalala, kama ni mchana nachomoa alaf naondoka

Badae wale majamaa wakachoka ile tabia ya umeme kukatik hovyo wakaondoka. Siku hizi najifunza kukata umeme chumba cha muhusika mwenyew bila kutesa wengine
Kwa hiyo awaja wai kujua kama una wafanyia huuni?
 
Mimi kuna jirani zangu wana hiyo tabia yani asubuhi mapema iwe ni weekdays au weekends asubuhi wanaanza na bongo flavor na huo muda watoto wanakua wamelala, na ni wadogo kwahiyo wanaamshwa na makerere yani ni lazima watoto waamke, kwa kweli ni kero, na ni wadada walio bleach nywele i think unaelewa hawa wadada wa mithili hii walivyo ila ni ulimbukeni tu
 
Back
Top Bottom