Huwa sibembelezi mtu

Huwa sibembelezi mtu

Maisha haya umenikumbusha mbali sana mimi nilikuwa nalala mbagala stand pale kila siku kwasababu nilikuwa nakaa kwa mshikaji wangu nilimaliza naye o level yeye alipomaliza 4m4 akaende chuo mimi nikaenda A level then chuo.

Sasa nilipata kazi ya shift yaani unaingia asubuh mpaka saa 9:30 then saa 10:00 jioni mpaka saa 5 usiku then usiku mpaka asubuh.

Sasa nilikuwa sijaajiriwa nafanya kazi kama kibarua kwenye hyo kampuni ila walikuwa wananilipa posho sasa nikaomba kujishikiza kwake yaani kulala tu basi.

Aisee nilikuwa nikiingia kazini saa 9:15 natoka saa 5 usiku nikifika kwake nikigonga hafungui wala simu nikipiga hapokei kwa hyo nikawa narudi mbagala stand kulala yeye alikuwa anakaa ule mtaa wa juma nature.

Kutokana na visa vyake nikapangisha geto la 20 mbagala sisimizi mchwa mende wote nalala nao dirisha mtu akapita nje anaona nikaanza maisha nikapunguza mazoea naye hatimaye nikampotezea kabisa hatuwasiliani mpaka leo.

Nikaoa bila kumwambia sasa hivi anasema naringa kwasababu nimepata kazi na simu simpigii nimemwachia mungu kwasababu mimi naujua ukweli na yeye anajua ukweli alhamdulilah mambo safi mungu si athumani.

Nimeoa nina mtoto mdogo wa kiume nikifikiria maisha niliyotokea na nikimuangalia mwanangu namuomba mwenyezi mungu anipe afya na umri nimlee mwanangu au wanangu maisha ya sasa hivi hakuna cha ndugu wala rafiki wengi wanafiki tunaishi nae kwa tahadhari tu mungu tusaidie.
 
Back
Top Bottom