Huwa Rais anafikiria nini katika uteuzi wake?


labda wewe umenena ....
 
Kuna yule Mjeda mwingine wa Bukoba kule Aliyewachapa Walimu Bakora....baadae akatimuliwa na JK.....Asee hawa wajeda noma!!

hahaa 'kanali'? mnali!! mpaka wilaya sikuhizi inaitwa kwa mnali
 

Mkuu Hakuna lele mama katika mazingira gani ? Ya ukuu wa Wilaya au Ukuu wa Mikoa ? Hebu nifafanulie kidogo.
 
Mimi nionavyo, kwa Tanzania Jeshi lilikuwa politicised sana kiasi ambacho wanajeshi waliiva sana kisiasa hadi kuchukua siasa jeshini.Mf.JKT Mkuu wa kikosi alikuwa pia Mkuu wa chama au sijui ndio mwenyekiti.
Kwa msingi huu, na ili kuweka stability ya nchi vizuri imekuwa ni kawaida/utamaduni wetu kuwashirikisha hawa ndugu katika mambo mengi - siyo tu ukuu wa mkoa/wilaya bali hata kwenye balozi zetu kama livyopelekwa Meja jeneral Makame Rashid , miradi mbalimbali kama TACAIDS mtakumbuka alikuwepo Meja jenerali ( cheo sikikumbuki vizuri) Lupogo nk.
 
zipo kazi wapasazo kupewa wanajeshi pindi wanapostaafu,mfano kuwa attached katika projects za serikali kutokana na fani zao,kuwa kwenye mabaraza ya usuluhishi, kupewa mashamba wafanye kilimo bora,kutoa mafunzo kwa jamii kutokana na fani zao (hata vyuoni ikiwezekana).ujue wao issue ya maendeleo hawaijui,waweza hata angalia vifaa vyao jeshini no changes,amri ni amri tu no change,kupiga kupiga tu no change,so ukuu wa wilaya mikoa unahitaji multidimensinal thinking and experience,hii ni siasa,wajeshi sio sahihi hata kidogo.na hawa watu multdim wapo sana nchini mwetu raisi awatumie hao,tabu ni kuwa hivi vyeo vimekuwa vya kupoozana na kufadhiliana ndo tabu inapoanzia!kwa tz si rahisi kuorganise chaos i can see!!
 
tanzania kila kazi inatolewa kwa urafiki na ndio maana hatuendelei kwa vile tunaogopa kuwawajibisha marafiki zetu wanapo bolonga kazini.
 
Ni kinyume na KATIBA yetu ya JMT? Sio WATANZANIA? Hawajasoma fani nyingine zaidi ya huo UJESHI? Hatujapata MJESHI mzuri tu pale IKULU. Acha huo UDC na URC.
 
Nakumbuka Mkuchika alipo kuwa mkoa wa Tanga, Hahahaa!! Ilibidi asingizie watu wanamloga wakati madudu yalikuwa hayapandi kumkichwa..Mtumeeeeeh!!! Nchi yetu bana..Kila kitu kinawezekana..! Jamaa wamewajaza Makanali kuanzia kwa Mgosi Makamba hadi Newala...

Kungekuwa hakuna mpaka wa Msumbiji ungesikia hata huko kwa Zuru natali ni Makanali na Kepten John Komba wengi tu..!!!
 
 
Mimi nadhani hakuna tatizo lolote kwa Rais kuteua wanajeshi kushika madaraka yoyote katika nchi isipokuwa kama kufanya hivyo anakuwa amevunja sheria.

Wanajeshi (kama wananchi wengine wowote) wanayo haki ya kushiriki katika shughuli zozote ambazo wanaonekana kuweza kushiriki. Uwezo wao, nidhamu yao na hata mapenzi tu ya Rais yanatosha kuwa sababu ya kutosha kuhalalisha uteuzi wao.

Sioni sababu kwa kweli ya kufikiri wanajeshi hawana haki ya kuteuliwa kushika nafasi wanazoteuliwa kuzishika. Kwani kwa kuwabagua kwa namna hiyo, tunaweza kuanzisha matabaka ya wenye haki na wasio na haki ya kushika madaraka mbalimbali katika nchi.

Nadhani swali la muhimu ni kwanini wasiteuliwe kushika madaraka hayo, wakati wengine huteuliwa kwenye nafasi hizo?
 

na perfomance nayo tuiweke wapi?
 
may be pia naweza sema ndo kuiandaa nchi kuwaktk utawala wa kijeshi pale itapobidi kufanya hivyo,so may be mkuu wa kaya hatopata tabu kwani tayari watakuwa kila kona ya nchi ni kutoa amri basi! sasa tusemeje kwani?
 

ukweli ushaonyesha kuwa hawajui kitu inaitwa management an leadership especialy kwa civil activities,alizoea kupokea amri leo hii atakuwaje self starter? that means atapokea from above na kuimplement tuu basi!!
 

Ilikuwa wazi zaidi pale Nyerere alipomteua Meja Jenerali Sarakikya kuwa Balozi wetu Nigeria. Mtakaoweza kukumbuka kumbukeni ndipo mtaelewa huu utaratibu umetokea wapi na unaweza kutafsiriwa nambna gani.

Demokrasia ya kweli haitaki mambo haya. Labda mwanajeshi akijiuzulu akagombea ubunge hata Uraisi akachaguliwa hilo ni jambo mwafaka na si vinginevyo.
 
jishughulishe kidogo tu wa huhitaji kuchosha akili, anagalia mikoa/wilay azinazoongozwa na hao wageshi wastaafu afu ufanye tathmini...

Kwa Kanali Mstaafu aliyeamuru walimu watoto wacharazwe bakora? Au jimboni kwa Katibu Mwenezi mwenye kofia 3?
 

Nimeambiwa ukitaka kuwa mkuu wa mkoa ni lazima uwe ni mwanajeshi otherwise huupati afadhali hata ya ukuu wa wilaya unaweza kupata hata kama hujawa mjeshi.Labda wanafanya kazi ya kikachero
 
Mkuu Hakuna lele mama katika mazingira gani ? Ya ukuu wa Wilaya au Ukuu wa Mikoa ? Hebu nifafanulie kidogo.

Mimi mkuu wakti nipo Tanzania niliwahi kufanya kazi na kwa karibu sana katika level ya Mkoa na wanajeshi hawa Col Nsa Kaisi, Brig Mwakanjuki na vile vile nilipokuwa wizarani nilifanya kazi kwa karibu na Maj Gen Lupogo.

nakubali kabisa ukifanyakazi na hawa hakuna lele mama. maaagizo au maazimio yote yanawekwa katika time frame nao wanafatilia.

Sasa nikirudi kwenye ngazi ya wilaya. Nilikuwa nikiwa Mkoani unaona kabisa hao wanajeshi wa ngazi za wilaya wanafanya kazi zao kwa maelekezo toka juu.

Niliwapenda sana capt Nkoswe na wengine.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…