Tongue blister
JF-Expert Member
- Jun 19, 2009
- 362
- 11
- Thread starter
- #41
Mimi mkuu wakti nipo Tanzania niliwahi kufanya kazi na kwa karibu sana katika level ya Mkoa na wanajeshi hawa Col Nsa Kaisi, Brig Mwakanjuki na vile vile nilipokuwa wizarani nilifanya kazi kwa karibu na Maj Gen Lupogo.
nakubali kabisa ukifanyakazi na hawa hakuna lele mama. maaagizo au maazimio yote yanawekwa katika time frame nao wanafatilia.
Sasa nikirudi kwenye ngazi ya wilaya. Nilikuwa nikiwa Mkoani unaona kabisa hao wanajeshi wa ngazi za wilaya wanafanya kazi zao kwa maelekezo toka juu.
Niliwapenda sana capt Nkoswe na wengine.
Mkuu nadhani hizo time frame hata utakapokuwa nazo kwenye mafile 1,000 kama utendaji wako ni mbovu huwezi kwenda kokote. Kazi za mezani kwa kalamu ni wengi wanaziweza hata wewe au hata mama yangu mzazi kule kijijini anaweza hizo.
Wakuu wa Mikoa na Wilaya wanajeshi walio wengi hawajishughulishi zaidi ya kushughulikia maagizo wanayopata kutoka Serikalini. Hilo kubali au kataa lakini lipo wazi.
Kipindi ulipokuwa Tanzania ni tofauti na jana, Kama ulikaa na hawa waheshimiwa basi una bahati sana, Na huenda hata kutumia Bunduki unaweza.
Unaweza kuwa mkali sana kwa mwanao wakike lakini kama ukali ule hauna tija yoyote waweza shangaa mwanao huyo akapata ujauzito na akajifungulia nyumbani kwako...
Unapo kuwa Kiongozi usisubiri tu kupangiwa au kupewa maelekezo kutoka juu, Bali jaribu kubuni jinsi ya kuwaongoza wale walio chini yako kutokana na hali ya mazingira ya uongozi uliyopangiwa..Unapo boronga anaye laumiwa si boss wako bali ni wewe..!