kiss ov love
JF-Expert Member
- Jan 21, 2025
- 9,388
- 16,188
Za jumapili wakuu moja kwa moja kwenye mada, hivi huwa mnadili vipi na ndugu wa namna hii yeye akikutafuta ni kukuomba hela tu,, na hakuna chochote anachokusaidia kwenye maisha yako.
Ni dada yangu mtoto wa mama angu mkubwa, kuna kipindi waliuza eneo lao kama milioni 30 hivi, wakapewa mamilioni yao na mama yao, sikuwa napigiwa simu nilitumiwaga elf30 tu, na kipindi hicho nilikuwa nahihitaji support ya pesa ya ada ila walijikausha, wakaenda kununua eneo huko maporini hatimaye kumewashinda huko wamerudi huku Dar wamepanga.
Ndiyo huyu dada sasa ni mara nyingi sana ananitumiaga meseji za mara nimkopeshe hela mara nimsaidie mimi, anadhani nimesahau walichonifanyia, naombeni ushauri wenu huwa mnafanyaje kwa ndugu kama hawa.