Huu wivu wa hubby huu

Asprini na skay eclat msinifanye nicheke mpaka niji.....e nyie we haya. Najua skay ni mdogo kwangu ila Aspirin sijui. By the way wivu ni dalili nzuri ya kupendwa. Usipoonewa wivu ujue wewe ni kiti cha pembeni.
Wivu siyo mapenzi.

Watengeneza soda wangeweza kujaza chupa mpaka juu, ila space matters.

Tupeane space kwenye mapenzi ili kila mmoja aenjoy.
 
Mwanaume bila wivu hajakamilika.
Mwanzo 20
5 Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi, Bwana, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao,

Maneno niliyokoleza ni muhimu sana kumjua Mungu
 
Wivu siyo mapenzi.

Watengeneza soda wangeweza kujaza chupa mpaka juu, ila space matters.

Tupeane space kwenye mapenzi ili kila mmoja aenjoy.
Napinga hoja. Bila wivu hupendi babu na bibie???? Kuaminiana sawa lakini kachumvi ka wivu kakikosekana ujue mhu we basi tena. Lazima umjuze lahaziz wako unakoelekea na sehemu gani. Akupeleke, akushushe ule raha zako na shoga/rafiki yako na baadaye anaweza kuja kukufuata.
 
Mapenzi tunaweza kuyaonyesha bila kumbana na kumkosesha pumzi mwenza.

Mi naamini wivu ni hatua ya kwanza ya kutoaminiana. Kwa hoja ya huu uzi, ikiwa Sky alishaaga kulikua na haja ya kuuliza jinsia? Hata kama angekua ni mwanaume tuseme haamini kua Sky anaweza kujichunga?

Mi naona tutofautishe kati ya kumuonea wivu na kumjali mwenza.
 
πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…