Huu utaratibu mpya wa TANESCO wakulipa deni ni kiashiria tosha kuwa hawataki sisi wenye hali ya chini tutumie umeme

Mkuu wanatafuta pesa za kujenga jengo jipya!! Hizo lawama zako ungezipeleka kwa alietoa amri ya kuwabomolea pale
Kama ndo wanatafuta pesa kwa nguvu basi hawatozipata maana kqa hali ilivyo ni bora hizo pesa tujichange tununue Solar walau tipate mwanga maana hatuna matumizi makubwa.
 
ungekuwa unajua jinsi hayo madeni yalivyotokea kwa wateja wengi usingemlaumu mleta mada,zamani wakati mfumo wa mita za LUKU,haujawa kwa kila mteja kulikuwa na zile mita ambazo tanesco wanatakiwa waje kusoma kila mwezi ,wengi wao walikuwa hawaji kusoma mita bali wana kadilia tu matumizi yako ya kila mwezi na kukuletea bill,balaa lililowakumba wateja wengi walikuwa wanakadiliwa makadilio ya chini kuliko matumizi halisi,sasa hizo units zinazoachwa kila mwezi baada ya mwaka unazani itakuwaje??balaa lilianza pale walipoanza kuzibadilisha hizo conversion meter na kuweka luku,kwani lazima wasome actual readings,ndio unakuta mtu anadaiwa milioni kadhaa!!!na baadaye tanesco waliliona hilo kuwa kwa kiasi. Fulani walichangia ndio maana wakaweka utaratibu huo wa malipo kidogo kidogo!!kama wameutoa watu Mwafaaaa
Mkuu umeongea points
 
Mkuu wanadai watu wengi,sio wewe tu.Wakikusanya madeni yote Tanzania nzima, ni hela nyingi.Nenda kalipe tu mkuu, ili wakuuzie umeme.The choice is yours.
Hawatopata kitu mkuu,hiyo pesa wanayotudai ni bora tuitunze walau iongezeke tukanunue solar
 
Ila nyie TANESCO si mpo humu mbona mnashindwa kuja kutoa ufafanuz au hili tangazo lenu la hapo chini mlimaanisha nin?
Tanesco.PNG
 
Hawatopata kitu mkuu,hiyo pesa wanayotudai ni bora tuitunze walau iongezeke tukanunue solar
Sawa,ila muombe Mungu wasiamue kuwapeleka mahakamani.Na hata hivyoo, solar nayo ina limitations zake,labda kama matumizi yenu ni madogo, kwa hiyo you only need a small capital investment.Pigeni mahesabu yenu vizuri.
 
Nakushauri kaonane na meneja wa eneo husika au kwa Public relation wa eneo ulilopo hao wote wanaweza kukusaidia
 
Juzi ulileta mada kama hii, tukakusaidia kuelezea scenario kama hizo za watu wa Tanesco.

Kuna taratibu nyingi za kulipia madeni Tanesco, kuna madeni ya aina mbili, moja ni madeni yanayotokana na malimbikizo ya ankara za nyuma kutoka mita za zamani za kuzunguka na deni la pili linatokana na wizi wa umeme.

Kama deni lako linatokana na malimbikizo ya ankara za nyuma basi utaratibu ni kulipia nusu ya muamala wako, ukinunua umeme wa 10,000 unakatwa 5,000 kwa ajili ya deni la zamani na unapewa umeme wa 5,000 iliyobaki.

Kama deni linatokana na wizi wa umeme, hilo ndilo unalazimishwa kulipia kiasi flani kwa mwezi ili uruhusiwe kununua umeme, hili unaweza kuonana na meneja wa eneo husika ukamuomba akusaidie kama kiwango walichokuwekea kiko juu sana.

Wewe una deni la wizi wa umeme, nenda ofisi ya tanesco iliyo karibu na wewe watakusaidia. Usiwalaum bila kuwasilikiza.

Awali nilikua najua naamini Tanesco ni watu wa ajabu sana ila baada ya kuwasikiliza nikawaona ni watu tofauti na nilivyokua nawachukulia.
 
Habar wakuu,

Kwa masikitiko makubwa napenda niwaombe TANESCO waje watoe kila kilicho chao majumbani mwetu ili tujue moja.

Wameanzisha utaratibu wa ajabu kwa wateja wanaodaiwa madeni. Mwanzo walikuwa wanatukata madeni kupitia mfumo wa Luku, yaani tunanunua umeme tunapewa nusu ya pesa tulionunua umeme. Tukinunua umeme wa 10000 tunakatwa 5000 tunapewa umeme wa 5000

Chaajabu hivi sasa hawataki tena tulipe kwa mfumo huo! Yaani wanataka ulipe kiasi kikubwa cha pesa, mfano nyumbani wametuambia tunatakiwa kulipa Tsh. 85000 kila mwezi halafu ndo turuhusiwe kununua umeme! Tusipotoa hiyo hela hatupati umeme!


Hili haliwezekani hata kidogo, umeme tunaotumia kwa mwezi ni wa 10000. Je tutawezaje kumudu hiyo 85000 kila mwezi?


TANESCO Tuoneeni huruma jamanii vyuma vimekaza. Leo ni siku ya NNE tupo kizani.
Nyie ndio mlikuwa mnaiibia Tanesko mnafaa kusekwa rumande
 
Hilo deni limekujaje?.. naomba kujua.
zamani wakati mfumo wa mita za LUKU,haujawa kwa kila mteja kulikuwa na zile mita ambazo tanesco wanatakiwa waje kusoma kila mwezi ,wengi wao walikuwa hawaji kusoma mita bali wana kadilia tu matumizi yako ya kila mwezi na kukuletea bill,balaa lililowakumba wateja wengi walikuwa wanakadiliwa makadilio ya chini kuliko matumizi halisi,sasa hizo units zinazoachwa kila mwezi baada ya mwaka unazani itakuwaje??balaa lilianza pale walipoanza kuzibadilisha hizo conversion meter na kuweka luku,kwani lazima wasome actual readings,ndio unakuta mtu anadaiwa milioni kadhaa!!!na baadaye tanesco waliliona hilo kuwa kwa kiasi. Fulani walichangia ndio maana wakaweka utaratibu huo wa malipo kidogo kidogo!!kama wameutoa watu Mwafaaaa
 
Sawa,ila muombe Mungu wasiamue kuwapeleka mahakamani.Na hata hivyoo, solar nayo ina limitations zake,labda kama matumizi yenu ni madogo, kwa hiyo you only need a small capital investment.Pigeni mahesabu yenu vizuri.
Hatuna matumiz makubwa
 
Back
Top Bottom