Tanesco huu utaratibu wenu wa wadaiwa kulipa madeni ni mzigo kwa masikini

imma_cafelatino

Senior Member
Dec 5, 2017
173
178
Leo nimefika tanesco kwa ajili ya kufatilia utaratibu waliouweka mpya wa kukusanya madeni kwa wadaiwa.Kifupi utaratibu huu ni gunia la misumari kwa watu wa kipato cha chini na hasa ukizingatia kwa sasa Hali ni mbaya mnoo kwa wananchi wengi.

Unakuta mtu anadaiwa let's say 10million na alikua anakatwa pindi awekapo umeme inakatwa automatically lakini Leo hii unamwambia awe analipa laki tatu na nusu kwa ushee ilhali huo umeme wenyewe kwa mwezi alikua ananunua kwa kudunduliza sasa hapo ni kukomoa watu wasiojiweza.

Tanesco mjitafakari Sana tena Sana ila ukiwauliza baadhi ya wahusika wanakwambia ni order imetoka juu wizara ya nishati.Inashangaza na kuumiza mnoo maana kila mtu unaemkuta tanesco anasema hawezi afford kulipa watu wanalalamika mnoo.

Uongozi wa tanesco pamoja na wizara husika mjitafakari upya kwenye huu utaratibu otherwise mmechemka Sana.
 
Back
Top Bottom