Huu utapeli manzese utaisha lini

Huu utapeli manzese utaisha lini

Makonda upo wapi?,wananchi wako wa Manzese wanaibiwa huko!,tupia jicho tafadhali..
 
Zamani walikuwa wanakamatwa sana hao wanaochezesha wamegundua njia baada ya kazi mgao polisi wanaambulia hawachezeshi bila ya kupata baraka za wakubwa.
 
Kuishi Dar kunahitaji akili ya ziada... hakuna cha bure hapa mjin , ukiona v2 kam ivo jiongeze vinginevyo utalia kila cku wengne ndo maisha yao hayo
 
Wanalazimishwa kucheza huo mchezo?
Deo Carleone, mtu awe amelazimishwa au amecheza kwa hiyari yake as far as kuna uhuni umejificha nyuma yake ni kazi ya serikali kuusitisha mara moja.

Kama serikali ina jukumu la kutulazimisha tusichukue 'FAO la kujitoa' ili kwamba tusipate shida uzeeni (which is unreasonable) kwa nini hapa isibebe jukumu hilo.

Wanaofanya huo uhuni wanajua kuna watu wa aina na ufahamu mbali mbali, si kila mmoja ana ufahamu km wako wewe.
 
Mm ndo nipo karibu nao zaidi wanachofanya Sio haki ila serikali inashirikiana nao hao wezi yaani mpaka kero unakuta mtu Kaja kununua bidhaa anaishia pale na pesa yote inaondoka yaani hadi kwetu biashara inakuwa ngumu
 
Mimi mwenzenu wakati nahamia Kigoma nilikutana na wale wazee wa karata 3 pale kwa bela walioko Kigoma wanapajua. Walitaka kinila pesa, ila sikua na za kutosha wakachukua sim yangu. Kilichotokea........
Nilienda kuwachukua vijana wenzangu kama 20 hivi, tulienda kuwachakaza na kuwapeleka central police.
Mbona sim ilirudisha siku ya pili. Hadi naondoka Mkoa ule wale vijana walikua marafiki zangu. Na mchezo ulisimama kwa mda wa wiki 2. Walikua wanauguza vidonda, police walitupa hongera kwa kazi nzuri.
 
Na hao hamjaanza kuwachakaza jipangeni vijana wenzangu wake kwa waume muwachakaze.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom