Huu upuuzi wa wazanzibari usisikilizwe kabisa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Huu upuuzi wa wazanzibari usisikilizwe kabisa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pdidy, Jan 9, 2010.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Jan 9, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,109
  Likes Received: 5,565
  Trophy Points: 280
  AFP waunga mkono Karume aongezewe muda

  Nora Damian

  CHAMA cha Alliance for Tanzania Farmers (AFP), kimetaka Rais wa Zanzibar, Amani Abeid Karume, aongezewe muda, ili awe katika nafasi mzuri ya kuunda serikali ya mseto.


  Kauli hiyo imekuja huku kukiwa na hoja zinazokinzana, kuhusu kiongozi huyo ama kuongezewa au kutoongezewa muda wa kuongoza serikali ya Zanzibar.


  Mapema wiki hii, Msaidizi wa Katibu Mkuu wa CUF, Ismail Jussa, alikaririwa na gazeti dada la The Citizen, akitaka Rais Karume, aongezewe muda wa kuwa madarakani, lakini baadaye Mwenyekiti wa chama hicho, Profesa Ibrahimu Lipumba, alisema huo si msimamo wa chama chake.


  Pia Chama Cha Mapinduzi

  (CCM), kilichomweka madarakani Rais huyo kimesema hakina mpango wa kumuongezea kwa sababu utaratibu hauruhusu.


  Hoja ya kutaka Rais Karume aongezewe muda wa kuwa madarakani, imeibuka katika majuma ya hivi karibuni baada ya kiongozi huyo na Katibu Mkuu wa CUF, Seif Sharrif Hamad, kukutana na kukubaliana kuzika tofauti za kisiasa, jambo ambalo limewaletea sifa viongozi hao.


  Akizungumzia hoja hiyo jana jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa AFP, Said Soud Said, alisema si dhambi Rais Karume,kuongezewa muda wa kuwa madarakani na kwamba dhambi ni kutoa wakimbizi wanaotokana na machafuko yanayoweza kutokea baada ya uchaguzi


  Alisema Wanzanzibari, wanahitaji mno kuwepo kwa serikali ya mseto, ili hatimaye waweze kuishi kwa amani na utulivu huku wakiwa wamoja.


  Sais alisema Zanzibar inaongozwa na katiba ya nchi na kwamba kwa kupitia katiba hiyo, Rais Karume ana uwezo wa kuunda serikali ya mseto akivishirikisha vyama vyote vya siasa, hatua ambayo alisema italeta utulivu katika visiwa hivyo.


  "Kuundwa kwa serikali ya mseto visiwani Zanzibar, kutasaidia kuindoa nchi hiyo katika mitafaruku ya mara kwa mara ya kisasa inayotokana na msimamo wa viongozi walioko madarakani, kukataa serikali ya mseto," alisema Said.


  Hivi karibuni, CCM kupitia Makamu Mwenyekiti wake (Bara), Pius Msekwa, ilisema haiwezi kumuongezea muda Rais Karume, muda wa kuwa madarakani kwa sababu ni kinyume cha katiba.


  Msekwa alisema katiba ya chama hicho, inataka marais wa pande zote mbili za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kushika nyadhifa hizo kwa mihula miwili ya miaka mitano, kwa kila muhula.


  Katika hatua nyingine, chama cha AFP kimeiomba serikali kutoa msamaha wa kodi kwa vyama vya siasa ili waweze kuingiza nchini vifaa vya kampeni ambavyo alidai kuwa ni rahisi kuvinunua nje kuliko hapa nchini.


  Chama hicho ambacho kimeanzisha operesheni ijulikanayo kama 'pomboo' kuhamasisha wananchi kujiunga nacho pia kimemtaka rais Jakaya Kikwete akutane na viongozi wakuu wa vyama vya upinzani kabla ya muda wake wa uongozi kumalizika ili waweze kumweleza mambo mbalimbali
   
 2. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #2
  Jan 9, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,109
  Likes Received: 5,565
  Trophy Points: 280
  Hivi vyama vinavyoanza kumchanganya rais karume vikome kabisa
  wiki iliopita vilianza vyama vya wamama
  mara vyama vya watoa mikopo
  mara vyama vya wauza vifaa vya kilimo
  hawa tena

  ccm kwa hili tutakufa na nyie daima;msiruhu ujinga kama huu
   
 3. October

  October JF-Expert Member

  #3
  Jan 9, 2010
  Joined: Oct 5, 2009
  Messages: 2,147
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Kwani yeye tu ndio anaejua kuunda serikali ya Mseto?
  Hii kwa nini watu wengine wanapenda kujifanya wao ni Oxygen?
   
 4. Z

  Zion Train JF-Expert Member

  #4
  Jan 9, 2010
  Joined: Jun 5, 2008
  Messages: 503
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  karume ataongezewa miaka miwili hawe pamoja na seif(mseto), uchaguzi zenjibar hakuna mwaka huu, habari ndiyo hiyo.
   
 5. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #5
  Jan 9, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Kwa Katiba ipi Rais huyo ataendelea kuwa madarakani hata baada ya muda kwisha? Kwani huo ni mchezo wa soka mpaka kuwe na muda wa majeruhi ambaye anayeuongeza ni refa tu? Oh, use your brain, at least once please!
   
 6. Che Kalizozele

  Che Kalizozele JF-Expert Member

  #6
  Jan 9, 2010
  Joined: Jul 20, 2008
  Messages: 778
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Kaka naona huyu jamaa leo unae tuu,akila kona una yeye with the same statement,"Use your brain atleast once please"
   
 7. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #7
  Jan 9, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Ninapojibu mara nyingine huwa siangalii nimemjibu nani, ninachoangalia ni hoja yenyewe tu ndugu, sorry kama inaonekana namtarget mtu yule yule! Ni katika kuweka msisitizo wa jambo! Thanks for your observation!
   
 8. Z

  Zion Train JF-Expert Member

  #8
  Jan 17, 2010
  Joined: Jun 5, 2008
  Messages: 503
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  sijaelewa ni nini unakusudia? yuko na mimi kivipi?
   
 9. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #9
  Jan 17, 2010
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...CCM 'inaogopa' nini kumpa KARUME muda wa nyongeza kuunda hiyo serikali ya mpito iwapo wapinzani wameridhia? Katiba sio msahafu au biblia kusema 'hauguswi'!

  Hata kama CCM itang'ang'ania kuweka mgombea wake, nchi ya Zanzibar itakuja ongozwa na serikali ya Upinzani, kama sio 2010 basi 2015.

   
 10. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #10
  Jan 17, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,547
  Likes Received: 18,204
  Trophy Points: 280
  Kwa vile katiba siyo Msahafu, inabadilishika na itabadilishwa!.

  CCM bara lazima wajifunze kusoma alama za nyakati, Karume keshafungua macho, hawaweza kumfanya zezeta kama walivyomfanza Jumbe. Yeye na Seif wameshakubaliana, uchaguzi mwaka huu, Zanzibar mikononi mwa Seif, hiyo CCM bara itatafuta pa kushikia na pa kushikia.
   
 11. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #11
  Jan 17, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  waachani wenye zanzibari yao waamue mambo yao wenyewe kwani nyie inawahusu nini?hata wakitaka karume awe rais wa milele si sawa tu
   
 12. Monsignor

  Monsignor JF-Expert Member

  #12
  Jan 18, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 523
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mimi naamini hatima iko mikononi mwa Karume kwana Seif ameshatamka lakini Karume kwa sababu anazojua ameshatamka hadharani kuwa hataki sasa kama anayetakiwa ameshasema hapana nani tena atendeleza huo uchuro? Labda Seif ataomba apewe amalizie miaka miwili akidai ni kumalizia kipindi cha Karume.
  Sisi kina tuhusu kwa sababu watakuja kutusumbua hawa. Huu ushirikiano wao ni wa wachawi hauwezi kudumu.
   
Loading...