mh ndugu yangu hiyo mikoba inaweka vitu vingi kutaja vichache huwa tunaweka
vipodozi,
kanga au kitenge wengine mtandio incase of msiba au kujisitiri wakati wa lolote,
viatu vya ziada vya chini ukichoka viatu virefu,
mwamvuli wa ziada mdogo wa kwenye pochi kama mvua itanyesha,
kiadiary kidogo
laptop ndogo,
pedi wengine wanaweka mbili tatu wengine wanaweka bunda zima.
dawa za kutuliza maumivu ya tumbo la hedhi la ghafla au kichwa kama panadol,hedex,etc
wengine wataongezea....
kwa list hii lazima uwe na jikoba.
kuna wadada au wanawake wao hawapendi kubeba vitu hivi wao wanabeba kipima joto kipochi kidogo ukiweka simu ya mkononi tu na kitambaa cha jasho kimejaa. akipata dharura anahaha.
kila mtu na mtazamo wake.