Huu upagazi kwa wanawake utakoma lini?

Huu upagazi kwa wanawake utakoma lini?

tpaul

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2008
Posts
27,765
Reaction score
29,209
Siku hizi imekuwa kama desturi kwa wanawake na wasichana kubeba mikoba au mabegi kila mahali waendapo. Ukubwa wa vipochi, mikoba au mabegi haya hotofautiana ukubwa na ubora kutoka kwa mwanamke/msichana mmoja hadi mwingine. Kuna baadhi ya mabegi haya ni makubwa sana hata kufika uzito kilo 10 au zaidi yakiwa yamejazwa 'vitu' pomoni.

Kila siku nimekuwa nikijiuliza ni kwanini hasa kina mama wanajibebesha 'mizigo' hii kila wanapotoka nyumbani kwao kwenda kazini, matembezini, harusini, sokoni, saluni au mahali popote pale. Utamkuta mmama kabeba bonge ya begi lililosheheni makorokoro lukuki, hadi bega limekaa upande. Ukipanda kwenye daladala ukakosa kiti na ukabahatika kusimama mkabala na kinamama, utabanwa na hii mibegi yao mpaka utakoma. Yaani karibu nusu ya nafasi ndani ya gari inakuwa occupied na mibegi hii. Na usiombe ukapakana na wamama wa uswahilini--ambao hubeba mikoba mikubwa kupindukia!

Ni nini hasa siri ya mafanikio ya hawa viumbe hai mpaka wakahiari kujibebesha mizigo hii mizito kila mahali wawapo? Na nini hasa kinachobebwa kwenye mikoba hii ambacho ni lazima wawe nacho wakati wote? Wanafanya hivi kama fasheni tu ama kwa kuigana? Maana kina mama kwa kuiga hata vitu visivyokuwa na tija, hawajambo!
Nawaza tu.
 
mimi sioni tatizo. ni brain balansing tu. Wamasai nao hawawe wakiume hawawezi kutembe bila fimbo hata kama yupo mjini. hata wewe jaribu kuhau warreti yako utona unpwaya.
 
Siku hizi imekuwa kama desturi kwa wanawake na wasichana kubeba mikoba au mabegi kila mahali waendapo. Ukubwa wa vipochi, mikoba au mabegi haya hotofautiana ukubwa na ubora kutoka kwa mwanamke/msichana mmoja hadi mwingine. Kuna baadhi ya mabegi haya ni makubwa sana hata kufika uzito kilo 10 au zaidi yakiwa yamejazwa 'vitu' pomoni.

Kila siku nimekuwa nikijiuliza ni kwanini hasa kina mama wanajibebesha 'mizigo' hii kila wanapotoka nyumbani kwao kwenda kazini, matembezini, harusini, sokoni, saluni au mahali popote pale. Utamkuta mmama kabeba bonge ya begi lililosheheni makorokoro lukuki, hadi bega limekaa upande. Ukipanda kwenye daladala ukakosa kiti na ukabahatika kusimama mkabala na kinamama, utabanwa na hii mibegi yao mpaka utakoma. Yaani karibu nusu ya nafasi ndani ya gari inakuwa occupied na mibegi hii. Na usiombe ukapakana na wamama wa uswahilini--ambao hubeba mikoba mikubwa kupindukia!

Ni nini hasa siri ya mafanikio ya hawa viumbe hai mpaka wakahiari kujibebesha mizigo hii mizito kila mahali wawapo? Na nini hasa kinachobebwa kwenye mikoba hii ambacho ni lazima wawe nacho wakati wote? Wanafanya hivi kama fasheni tu ama kwa kuigana? Maana kina mama kwa kuiga hata vitu visivyokuwa na tija, hawajambo!
Nawaza tu.

Haaa haaa, unawaza na kuandika. Sio kuwaza tu.
 
mimi niliwahi kufanya nao kazi kwa kweli hiyo mikoba ilikuwa inatumika kuficha vitu mbalimbali kama maziwa,sukaru, toilet paper vitu ambavyo ofisi walikuwa wanatoa ili staff watumie
 
wanabeba vitendea kazi,na vitu vyengine vya dharura.
Nalog off
 
kilo kumi??????????? Hapo umezidisha chumvi kbsaaaa cz ni ngumu hata mkoba uwe mkubwa vipi ukafika kilo hata mbili otherwise awe anabeba magendo. Then pilipili usiyoila yakuwashia nini?? Mabega yao ndo yanaumia so waache.
 
Ni ishu ya kisaikolojia zaidi,me nahisi wengi wao wanaona bila mkoba hawajakamilika,na pia hyo mikoba huwapa kampani
 
mh ndugu yangu hiyo mikoba inaweka vitu vingi kutaja vichache huwa tunaweka

vipodozi,
kanga au kitenge wengine mtandio incase of msiba au kujisitiri wakati wa lolote,
viatu vya ziada vya chini ukichoka viatu virefu,
mwamvuli wa ziada mdogo wa kwenye pochi kama mvua itanyesha,
kiadiary kidogo
laptop ndogo,
pedi wengine wanaweka mbili tatu wengine wanaweka bunda zima.
dawa za kutuliza maumivu ya tumbo la hedhi la ghafla au kichwa kama panadol,hedex,etc
wengine wataongezea....

kwa list hii lazima uwe na jikoba.

kuna wadada au wanawake wao hawapendi kubeba vitu hivi wao wanabeba kipima joto kipochi kidogo ukiweka simu ya mkononi tu na kitambaa cha jasho kimejaa. akipata dharura anahaha.
kila mtu na mtazamo wake.
 
Siku hizi imekuwa kama desturi kwa wanawake na wasichana kubeba mikoba au mabegi kila mahali waendapo. Ukubwa wa vipochi, mikoba au mabegi haya hotofautiana ukubwa na ubora kutoka kwa mwanamke/msichana mmoja hadi mwingine. Kuna baadhi ya mabegi haya ni makubwa sana hata kufika uzito kilo 10 au zaidi yakiwa yamejazwa 'vitu' pomoni.

Kila siku nimekuwa nikijiuliza ni kwanini hasa kina mama wanajibebesha 'mizigo' hii kila wanapotoka nyumbani kwao kwenda kazini, matembezini, harusini, sokoni, saluni au mahali popote pale. Utamkuta mmama kabeba bonge ya begi lililosheheni makorokoro lukuki, hadi bega limekaa upande. Ukipanda kwenye daladala ukakosa kiti na ukabahatika kusimama mkabala na kinamama, utabanwa na hii mibegi yao mpaka utakoma. Yaani karibu nusu ya nafasi ndani ya gari inakuwa occupied na mibegi hii. Na usiombe ukapakana na wamama wa uswahilini--ambao hubeba mikoba mikubwa kupindukia!

Ni nini hasa siri ya mafanikio ya hawa viumbe hai mpaka wakahiari kujibebesha mizigo hii mizito kila mahali wawapo? Na nini hasa kinachobebwa kwenye mikoba hii ambacho ni lazima wawe nacho wakati wote? Wanafanya hivi kama fasheni tu ama kwa kuigana? Maana kina mama kwa kuiga hata vitu visivyokuwa na tija, hawajambo!
Nawaza tu.

mh ndugu yangu hiyo mikoba inaweka vitu vingi kutaja vichache huwa tunaweka

vipodozi,
kanga au kitenge wengine mtandio incase of msiba au kujisitiri wakati wa lolote,
viatu vya ziada vya chini ukichoka viatu virefu,
mwamvuli wa ziada mdogo wa kwenye pochi kama mvua itanyesha,
kiadiary kidogo
laptop ndogo,
pedi wengine wanaweka mbili tatu wengine wanaweka bunda zima.
dawa za kutuliza maumivu ya tumbo la hedhi la ghafla au kichwa kama panadol,hedex,etc
wengine wataongezea....

kwa list hii lazima uwe na jikoba.

kuna wadada au wanawake wao hawapendi kubeba vitu hivi wao wanabeba kipima joto kipochi kidogo ukiweka simu ya mkononi tu na kitambaa cha jasho kimejaa. akipata dharura anahaha.
kila mtu na mtazamo wake.

mkuu nafikiri umepata picha.
 
Umenikumbusha kuna mdada mmoja hospitali Muhimbili, alikuwa ameenda kwenye issue za uzazi, kumbe siku zilikuwa za mwishoni hivyo manesi wakalazimika kumbakisha. Nesi mmoja akamuuliza..begi lako liko wapi? Akasema sijaja nalo...nesi akamuambia aah, cha maana ulichoona ni hiyo pimajoto, basi leo utabeba mtoto humo humo....

Ila mtoa mada amezidisha jamani, begi la kilo kumi tena? Au anachanganya na mtu aliyebeba biashara?
 
Siku hizi wanawake wengi wanafanya bisahara na kutokana na maendeleo ni nadra kumuona mtu kabeba Rambo kuja mjini. Wafanyakazi wengine asubuhi anabeba vitafunwa vya kuuza ofisini kwake, anabeba lunch box yake, wax, mitumba, vipodozi, wengine viungo, hivyo hiyo mikobo usishangae ina siri nyingi mjini hapa kama ulitaka kuniibia mkono waweza donolewa na kuku au kulowa mayai ndani ya mkoba wangu lol
 
Umenikumbusha kuna mdada mmoja hospitali Muhimbili, alikuwa ameenda kwenye issue za uzazi, kumbe siku zilikuwa za mwishoni hivyo manesi wakalazimika kumbakisha. Nesi mmoja akamuuliza..begi lako liko wapi? Akasema sijaja nalo...nesi akamuambia aah, cha maana ulichoona ni hiyo pimajoto, basi leo utabeba mtoto humo humo....

Ila mtoa mada amezidisha jamani, begi la kilo kumi tena? Au anachanganya na mtu aliyebeba biashara?

kilo kumi hata mimi nimechoka lo nimechekaje
 
Umenikumbusha kuna mdada mmoja hospitali Muhimbili, alikuwa ameenda kwenye issue za uzazi, kumbe siku zilikuwa za mwishoni hivyo manesi wakalazimika kumbakisha. Nesi mmoja akamuuliza..begi lako liko wapi? Akasema sijaja nalo...nesi akamuambia aah, cha maana ulichoona ni hiyo pimajoto, basi leo utabeba mtoto humo humo....

Ila mtoa mada amezidisha jamani, begi la kilo kumi tena? Au anachanganya na mtu aliyebeba biashara?

kua siku kituo cha mwenge mvua inanyesha ya haja, dada moja alivaa gauni refu ila la vitambaa hivi vya kung'ang'ania na nguo kalowa nguo yote imemnasa mwilini chupi yaonekana matiti yanaonekana mkononi kashika kiwaleti kidogo cha kuwekea simu. watu wakaanza kumzonga kwa kelele na kumzomea mama mmoja akamwendea na kufungua jikoba lake na kumtolea kanga akamwambia mwanamke ni vema kutembea na mkowa mwenye vitu vya kukusitiri ona sasa mwanangu unaaibika kisa fashion.
labda uwe harusini utabeba kipochi kidogo lakini kama unausafiri ndani ya gari unakuwa na pochi yenye vya ziada ukumbuni ndio unaingia na kile kidogo kinachoendana na gauni lako au vazi lako.
 
hao hata ukiwanunulia bia nyingi hawanywi zote wanabadili za kopo wanatia kwenye jikoba inakuwa take away mkobani
 
umevaa suruali si inamifuko unaweka sim,warret,leso n.k basi na wao wanamikopa swali jepesi mnaigirizia
 
Au ndo "gym" za kiaina! Manake kuzunguka na mkoba kwa siku nzima ni zoezi tosha!
 
Back
Top Bottom