Musoma Yetu
JF-Expert Member
- Mar 11, 2016
- 2,633
- 2,297
Ni kwa nini kwenye hili sakata la mchanga kuna watu (wana siasa) wanameanza kutaka kuonekana wenye nia njema,na wengine hawana nia njema. Lakini hawa wanasiasa wenye nia njema na wasio na nia njema ni wapi?
Siasa zetu kwa muda mrefu zimekuwa siasa za maji taka ( za kuchafuana na kuonyeshana ubabe hata mahala ambapo kuna nia njema au hakuna nia njema). Natoa mifano michache tu.
i) Kuna kundi la wanasiasa Fulani kwa muda mrefu wamepiga kelele kuhusu mikataba iliyopo ya madini enzi za utawala wa Mkapa, Kikwete. Hati za dharura zimepitishwa kuhusu madini utafikiri nchi ilikuwa inaelekea kufa. Tulikuwa na nia njema...!
ii) Mara nyingi mikataba mikubwa ya nchi hii na kwenye rasilimali zetu ni siri, kwa nini iwe siri? Tuna nia njema na Taifa...!
iii) Ni mara ngapi wananchi tumepiga kelele ili mikataba isiwe siri na mpaka leo hakuna lolote? Jamii forum kuna nyuzi zaidi ya 100 zinahoji kuhusu rasilimali za nchi. Wananchi, tulieni kelele za nini mitandaoni? Tuna nia njema kabisa....!
iv) Mchakato wa katiba mpya ulianzishwa, kazi ilifanyika na wananchi tukatoa maoni yetu vizuri tu. Rasimu ikasomwa bungeni, ikajadiliwa na ghafla ikatupwa kwenye makabati na hatujui ni lini itajadiliwa tena. Wananchi tulieni hivyo hivyo....Tuna nia njema..!
v) Wengine tulipiga kelele, tukapewa madaraka, tulipopewa madaraka tulikuwa hatusikii kelele wala minong’ono kipindi tuna madaraka. Tumetoka, tumeanza kupiga kelele..! Tuna nia njema.!
vi) Leo hii limeibuka suala la mchanga kusafirishwa nje, tumeanza kunyoosheana vidole kuwa kundi fulani halina nia njema, au watu baadhi (C.C.M) na baadhi upinzani; hawana nia njema. Hivi hawa wenye nia njema wapo kweli? Na wanaendelea kuwa na nia njema na nchi hii?
vii) Sisi watanzania tuwe wakweli na dhamira zetu zituongoze. Nchi itaendelea kuwepo, watu tutaishi na wengine tutakufa! Iko wapi nia njema ambayo wananchi tunaaminishwa leo na wanasiasa wetu ?
Tusilaumiane wala kunyoesheana vidole! Siasa zetu ndo tatizo. Tubadili mfumo wa siasa zetu na kweli tuonyeshe tuna nia njema kweli.... hata kwa mola tutasamehewa dhambi zetu.
Nawasilisha.