HUU UJANJA AJANJA MAKAMPUNI YA SIMU, JE NI UTAPELI?

Simpompo

Member
Dec 22, 2016
66
21
Makampuni ya simu za kiganjani yamekuwa kero kwa wateja wake kwa kutowatendea haki, ni kwa kutoa huduma duni. Kuna kampuni inaongoza kwa usumbufu kwa wateja wake, imekuwa dhaifu sana kwa utendaji wake, itakapobidi tutaitaja kwa jina. Mtu akipata tatizo la kupoteza kadi akitoa taarifa, anaambiwa nenda kwenye duka kubwa la kampuni ya simu, mengi ambayo yapo makao makuu ya Mikoa. Ukifika unatoa vielelezo kwa maelekezo ya mhudumu. Pamoja na kutekeleza vigezo unambiwa nenda utapigiwa simu toka makao makuu ya simu Dar es salaam. Umesafiri labda zaidi hata zaidi ya kilomita 100, umelipa ghalama za kulejesha hiyo namba, unasubiri wki moja, wiki ya pili, unaingia wiki ya tatu, ujjapewa mrejesho ukipiga namba ulizopewa hazipatikani, zikipatikana hakuna msaada wo wote. Je wakurugenzi wa makampuni mnayajua haya? Kwa nini mtese wateja wenu? Makampuni ninayoyataja Airtel, TiGO, Halotel na Vodacom wachunguzeni wafanyakazi wenu, wanatesa wateja wenu. Mjue wana ajenda gani? Je nyie wamiliki mnajua adha sisi tunavyosumbuka, wengine kadi zimekuwa zinapitisha pesa za biashara iwe ni ndogo au ni kubwa zote ni pesa. Watendeeni haki wateja wenu.
 
TIGO, TAARIFA IWAFIKIE MKITOA TU BANDO LA CHUO NAHAMIA HALOTELI

NB: Nimeandika kwa herufi kubwa kuonyesha msisitizo
 
Back
Top Bottom