Huu ubishi, nipeni maoni yenu. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Huu ubishi, nipeni maoni yenu.

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by Judgement, Jul 13, 2012.

 1. Judgement

  Judgement JF-Expert Member

  #1
  Jul 13, 2012
  Joined: Nov 13, 2011
  Messages: 10,361
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 145
  Ninasibishe misemo hii miwili na ninachokisemea hapa.
  "Tembea uyaone" na
  "Hujafa hujaumbika"
  Hii ni kauli iliyobeba malalamiko lukuki kutoka kwa Baba (mzazi) kwenda kwa kijana wake wa kiume :-

  "Huyu mtoto nimemsomesha kwa gharama zangu , nikijinyima mambo kadha wa kadha , nikijua nawekeza kwa mwanangu.
  Matarajio ni aje kunilea pale mie nitakapofikia kuchoka.

  Umefika wakati sasa nimechoka nahitaji nipate mafao yalionifanya niwekeze kwake hali imekua kinyume na matarajio.
  Mwanangu ana kazi nzuri ni Boss Pale TRA , lakini sina faida nae! .
  Wanaonufaika na pesa zake ni wanawake malaya na wenye ma'Bar, yeye ni pombe , pombe na yeye.

  Hivi majuzi tumetoleana nae maneno , tumebishana sana akiwa kalewa ananiambia mimi sikumsomesha, bali kasomeshwa na walimu shuleni, namnukuu "kwani pesa zako ulizokua unalipa bila walimu ningesoma?" mwisho nukuu.

  Wadau ubishi wa nani kamsomesha kijana baina ya Baba na Mwalimu tuusemeeje ?
  Kijana ndiyo yuko sahihi au Baba?
  Kwa maana ya kusema kila mmoja kati yao apaswa aishi kivyakevyake?
  Nawasilisha.
   
 2. platozoom

  platozoom JF-Expert Member

  #2
  Jul 13, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 7,320
  Likes Received: 2,291
  Trophy Points: 280
  Kijana ni chizi........! sema tu hajafikia hatua ya kupelekwa mirembe
   
 3. CUTE

  CUTE JF-Expert Member

  #3
  Jul 13, 2012
  Joined: Mar 5, 2012
  Messages: 1,237
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  kijana yuko sahihi walimu ndio waliosomesha baba kalipa ada
   
 4. Judgement

  Judgement JF-Expert Member

  #4
  Jul 13, 2012
  Joined: Nov 13, 2011
  Messages: 10,361
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 145
  Nitamke kuutambua uwepo wako hapa Mhe. Platozoom, napokea changio lako.
   
 5. Ruhazwe JR

  Ruhazwe JR JF-Expert Member

  #5
  Jul 13, 2012
  Joined: Jan 31, 2011
  Messages: 3,414
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  kwa deni mpaka baba anze kudai hivyo,nadhani huyo baba mtu apimwe akili
   
 6. Judgement

  Judgement JF-Expert Member

  #6
  Jul 13, 2012
  Joined: Nov 13, 2011
  Messages: 10,361
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 145
  Na bila Baba kulipa fees, hapo TRA angekuwepo?
   
 7. platozoom

  platozoom JF-Expert Member

  #7
  Jul 13, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 7,320
  Likes Received: 2,291
  Trophy Points: 280
  Kijana hana adabu, haikuwa busara kumjibu hivyo baba yake..........Ndio mwalimu alimpa maarifa lakini kusomesha ni zaidi ya mwalimu kunahitajika jitihada ya mzazi kuhakikisha mwanafunzi amekwenda shule, amepata chakula, sare, na maneno ya kumtia moyo mwanafunzi.......isingekuwa haya angeweza kumsikiliza mwalimu?
   
 8. CUTE

  CUTE JF-Expert Member

  #8
  Jul 14, 2012
  Joined: Mar 5, 2012
  Messages: 1,237
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  sasa naona kijana unataka kuleta mambo ya yai na kuku nani alianza mweh!
   
 9. Bishanga

  Bishanga JF-Expert Member

  #9
  Jul 14, 2012
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 15,347
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 0
  Judgement,are you serious? How dare you?
  Ambao hamjazaa,inshalah mola awajalie uoe,mzae,mlee na kisha ndo mrudi uzi huu.
  Kuzaa na kulea ni jukumu kubwa sana,omba Mungu akupe mzazi mwenzio mlee pamoja.
   
 10. Judgement

  Judgement JF-Expert Member

  #10
  Jul 14, 2012
  Joined: Nov 13, 2011
  Messages: 10,361
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 145
  Hee! Mukubwa hujalala mpaka mida hizi ? Pamoja na mapilika yako ya majukwaani mchana kutwa!
  Nway nasaha zako zina mashiko.
   
 11. Judgement

  Judgement JF-Expert Member

  #11
  Jul 14, 2012
  Joined: Nov 13, 2011
  Messages: 10,361
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 145
  Uyasemayo yana sense.
   
 12. matumbo

  matumbo JF-Expert Member

  #12
  Jul 14, 2012
  Joined: Jul 9, 2011
  Messages: 7,199
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 145
  Kijana ni mpunga mpya wa Ileje.
   
 13. K

  Kenyi New Member

  #13
  Jul 14, 2012
  Joined: Jul 10, 2012
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hichi ndicho kizaz cha karne 21.
   
 14. Judgement

  Judgement JF-Expert Member

  #14
  Jul 14, 2012
  Joined: Nov 13, 2011
  Messages: 10,361
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 145
  Angekua mpunga wa Kyela afadhali?
   
 15. Judgement

  Judgement JF-Expert Member

  #15
  Jul 14, 2012
  Joined: Nov 13, 2011
  Messages: 10,361
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 145
  Kiongozi , hebu tufanye research isijekua hawa Kuku na Mayai ya broiler, Chips zikaangwazo kwa mafuta ya Transfoma, Industries food products , generally vikawa vinachangia kuharibu mentality ya vijana wa 21 century ?
  Si inasemwa tusiangalie tulipoangukia tuangalie kilichocoz anguko!
   
 16. Mkwai

  Mkwai JF-Expert Member

  #16
  Jul 14, 2012
  Joined: Feb 29, 2012
  Messages: 308
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Katika mabishano yao nadhani wote huenda hawakutendeana sawa, naamini katika mazungumzo staha ya maneno inapaswa kutumiwa na rika zote iwe wazee au vijana, baba au mwana ili kuweka utangamano au uelewano wa kile wanacholiongea na wanachokusudia kukiongea na kieleweke.
  Pili ningependa Wazazi tuelewe na tubadilike, kumsomesha mtoto ni wajibu wetu. Haya mawazo ya kumsomesha mtoto kwa minajili ya kuwekeza ili baadae aje akutunze nadhani hatuko sahihi. Cha msingi tusomeshe na tuwajengee misingi ya kuweza kusimama wao kama wao na kuendesha maisha yao kwa namna tunavotaka wawe.
  Hii habari ya kuwekeza kwa watoto ili baadae waje watufae kiuchumi kwa maoni yangu wengi hatuko sahihi. Tuna wajibu wa kuwawezesha ili waje wawe na maisha mazuri, na pia tusijisahau kuwekeza sehemu stahiki kwa ajili ya mafao yetu sisi wenyewe kama wazazi.

  Itokee tu mtoto aamue kukuongezea nguvu kiuchumi, lakini isiwe lazima. HAYA NI MAWAZO YANGU.
   
 17. Blaine

  Blaine JF-Expert Member

  #17
  Jul 14, 2012
  Joined: Jan 11, 2012
  Messages: 2,285
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  pole kwa mahasibu, ila epuka kubishana na mtu aliyelewa hamtapata muafaka. Ongea nae akiwa sober na uone atajibu nini.

  nini kilianza: yai vs kuku
  kipi bora: pesa vs elimu
  nani zaidi: ndugu vs rafiki nk
  epuka argument kama hizi, hazina tija
   
 18. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #18
  Jul 14, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,227
  Trophy Points: 280
  hivi bila mzazi kujinyima na kutafuta shule, plus kulipa ada, hao walimu huyo kijana angewaonea wapi?
   
 19. Mphamvu

  Mphamvu JF-Expert Member

  #19
  Jul 14, 2012
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 10,708
  Likes Received: 934
  Trophy Points: 280
  Roho inauma kwakweli, ukiona kichanga kikiumwa wazazi wanavyopata stress na hata kushindwa kula. Majamaa, spend time zenu na wamama wanaolea vichanga, inasaidia kurudisha heshima kwa wazazi wako. You know what am I saying...
   
 20. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #20
  Jul 14, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,091
  Likes Received: 6,557
  Trophy Points: 280
  Liliwahi kutokea katika familia inayonihusu kabisa,
  hali iliendelea baba akaugua kwa kuwa hakuwa na nyumba nzuri ilibidi augulie kwenye zizi la ng'ombe
  japo kijana alishajenga nyumba pembeni (akiwa anafunga milango kuacha mlinzi kwenda zake town kazini)
  baba akatwaliwa (RIP Mzee S).

  Baada ya muda mfupi sana toka atwaliwe baba yake, kila yule kijana akirudi zake wikiend akifungua mlango anamkuta baba yake kakaa sebuleni kwake, baada ya hapo alihangaika sana kwa kuwa ana imani za kishirikina, ila hata sasa bado siyo swari.

  Hapo mnaweza kupata majibu nyie wenyewe kuwa mzazi ni nani.

   
Loading...