bongo man
JF-Expert Member
- Dec 26, 2016
- 1,053
- 2,338
Habari za mchana wanajamvi, kuna jambo naliona na kulifananisha na wizi ambao tunafanyiwa waajiriwa huku waajiri na ma bank wakishilikiana kutuibia, kwa mfano si taasisi binafsi au serikalini kisheria mwajiri anatakiwa kumlipa mtumishi wake mshahara ndani ya siku 30 na si zaidi ya hapo na endapo itakuwa chini ya hapo basi kwa utashi W mwajiri. Kuna njamaa naziona kati ya waajiri kwa kutambua kuwa watumishi wengi wapo vijijini kusiko mbali na taasisi za fedha wameamua kuwa wanachelesha mshahara maksudi Ili watumishi waingie kwenye huduma ya kuulizia salio. Kumbuka kuna baadhi ya bank ukiuliza salio unakatwa 250 tsh. Sasa basi wasi wasi wangu waajiri watakuwa na % yao hapo ikumbukwe kuwa ikifika siku ya 30 watumishi wengi wanakuja wameishiwa hivyo wanakuwa na pressure ya kuulizia salio kwa wingi kumbe ndo wanaliwa kiaina. Huu ni utafiti wangu binafsi. Naomba kuwasilisha.