Huu ni uzembe wa viongozi MSD | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Huu ni uzembe wa viongozi MSD

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mpandafarasi, Jun 5, 2011.

 1. Mpandafarasi

  Mpandafarasi Member

  #1
  Jun 5, 2011
  Joined: Dec 7, 2008
  Messages: 57
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  MOJA kati ya habari zilizopewa uzito Juma hili ni ile inayoigusa bohari ya madawa (MSD) kusababisha hasara ya dawa zenye thamani ya sh bilioni 5.2 ambazo ziliharibika baada ya kuhifadhiwa kwa muda mrefu.

  Hayo yalibainika katika kikao cha Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC), baada ya makamu mwenyekiti wa kamati hiyo, Deo Filikunjombe, kumbana kaimu mwenyekiti wa MSD, Tekla Shangali, na mkurugenzi mkuu, Joseph Mgaya, ambao walishindwa kutoa ufafanuzi mbele ya kamati na kutakiwa kutoka nje ya kikao.

  Fikunjombe, alikuwa akirejea ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), ambayo ilibaini hasara hiyo baada ya mamlaka hiyo kuweka dawa katika hifadhi zake bila kuzisambaza na kusababisha kuharibika.
  Tanzania Daima tunaamini kuwa hasara hiyo ingeweza kuepukwa kama kungekuwa na ufuatiliaji na uwajibikaji wa viongozi husika kama wangejali ama kufikiri juu ya uhai wa watu walioko katika hospitali mbalimbali nchini ambao baadhi yao wamekuwa wakikosa fedha za kununulia dawa.
  Lakini viongozi hao hawakufanya hivyo, hawakutimiza wajibu wao.

  Ikumbukwe kuwa kuna maelfu ya Watanzania wanakufa kwa kukosa dawa hospitalini, huku serikali ikishutumiwa kila wakati.

  Tunasema hatuwezi kuvumilia hali hii kwa sababu suala la dawa ni suala nyeti linalogusa maisha ya kila Mtanzania hasa wale wenye kipato cha chini wasio na uwezo wa kupata huduma hiyo kwa kuhimili bei.

  Ikumbukwe hii si mara ya kwanza kwa MSD kuharibikiwa na dawa na kusababisha hasara kubwa tumeelezwa kuwa katika kipindi cha miaka minne iliyopita kuna dawa nyingine zenye thamani ya sh bilioni nane ziliharibika kutokana na uzembe wa watendaji wa bohari na hivyo kuisababishia hasara serikali.

  Tuna kila sababu ya kutamka kwamba hii ni aibu na fedheha kubwa kwa nchi maskini kama Tanzania ambapo kila wakati tumekuwa tukilia na hata kuwapigia magoti wahisani watusaidie katika suala zima la afya.

  Tunatoa wito kwa serikali, kuhakikisha inawachukulia hatua ikiwa ni pamoja na kuwafukuza kazi viongozi wa MSD ambao wamekuwa wakilegalega katika nafasi zao na hata kuisababishia hasara kila wakati.

  Kamwe hatutakubali kudanganywa kwa kuambiwa kwamba kilichotokea ni ajali iliyokosa kinga; la hasha, tunasema kilichotokea ni uzembe wa baadhi ya viongozi ambao mwisho wa siku huisababishia hasara serikali na Watanzania kwa ujumla.

  Source: Tanzania Daima, Jumamosi 04,06 2011 Huu ni uzembe wa viongozi MSD

  Nawasilisha
   
 2. MKWECHE

  MKWECHE JF-Expert Member

  #2
  Jun 5, 2011
  Joined: Apr 8, 2011
  Messages: 299
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Utendaji mbovu wa Bohari kuu la Madawa Tanzania(MSD) ndio chanzo kikukwa cha Uzorotaji wa Huduma za Afya katika Mahospitali,Vituo vya Afya na Zahanati zote za Serikali Tanzania.Hii ni kwa sababu Kisheria wao(MSD) ndio waliopewa jukumu la Kusambaza Dawa na Vifaa tiba ktk Hospitali Zote za Serikali!
  Ili Kupewa Nguvu Kifedha hawa MSD Hupewa fedha yote ya Iliyotengwa ktk bajeti ya dawa ya Serikali katika mwaka husika moja kwa moja toka hazina kuu ya Taifa,tena hupewa kwa mtindo wa malipo kabla(Pre-Paid),Juu ya hapo wakijitokeza wahisani wa nje wakitoa Grant ya Mabilioni ya Shilingi kwa ajili ya Madawa kwa ajili ya Hospitali zetu serikali nayo pia Hutumbukizwa MSD!
  Wana JF embu tutengeneze taswira juu ya MSD,Kwa kuchukua Mabilioni yote ya Budget ya Madawa na Vifaa tiba jumlisha fedha za Wahisani kila mwaka tangu MSD ianzishwe!Kuna sababu ya Kukosa Dawa na Vifaa Tiba!(Tunapozungumzia Vifaa tiba ni kama Gloves,Mabandeji na Mazagazaga tofauti na Dawa!)
  Maajabu ni Kwamba MSD wakati wote haina madawa ya Kutosha!Wimbo wao ni OS(out of stock) ndio kisingizio chao.Matokeo yake hospitali za serikali nazo wimbo wa dawa hakuna ndio uliozoeleka na Watanzania wenzetu wamepoteza na wataendelea kupoteza maisha kwa Kukosa Madawa na fedha ya Kununulia Madawa kwenye Maduka Binafsi ambayo mengi yake yanamilikiwa wa Waajiriwa wa Wizara ya Afya katika ngazi mbalimbali kuanzia wauguzi hadi Madakitari wanafanya kazi kwenye Hospitali zisizo na Dawa!Swala la kuambiwa nenda kanunue dawa duka flani hapa hospitalini hazipo nalo tulishaga lizoea muda,Lakini hili jipya la Dawa za 8bilioni kuoza MSD wakati ndugu zetu wanaangamia kwa kukosa dawa Mahospitalini Katu Halikubaliki,Halizoeleki,Halivumiliki na ni Ngumu "Kumeza"
  Hizi 8Bilioni zilipwe na Uongozi mzima wa MSD na Na Wizara ya Afya Imulikwe katika hili kwani MSD ipo chini yao na Dawa Zinapokosekana huku zinaozea Walikuwa Wapi?!Tupige Siasa kwenye IPTL,Richmond,Dowans na Symbion Lakini si kwa Afya za Watanzania!
  Malalamiko ya Kukosa Dawa na Vifaa tiba ni zao la Kuubeba Uongazi Hafifu wa MSD na Kuendekeza Ukuritimba kwenye Madawa!
  Swali,Je Ni nani kati yetu akipewa fursa na Upendeleo wa kupewa Budget yote ya Madawa na Vifaa tiba ya Serikali kwa mwaka mzima wa fedha na hapa Tunazungumzia Zaidi yaShilingi 45Bilioni za KiTanzania plus Michango ya Wahisani afu ufungue duka la madawa uuze Kibiashara na Faida apatayo abaki nayo kwa Sharti Moja Dawa zisikauke Mahospitalini atashindwa!Labda wengine si MSD!Hili nalo Janga La Kitaifa
  Nawasilisha
   
 3. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #3
  Jun 5, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  ..........YOU ARE DEAD WRONG, YOU DONT NEED KUVUNJA MSD UNLESS WEEWE NI MHINDI UNATAKA KUWANEEMESHA MA DMO, DT NA WAFAMASIA MATUMBO YAO

  I wish you knew how much MSD has contributed to safeguard at least most of the health supply system ya nchi hii

  NINGEKUELEWA KAMA UNGESEMA UONGOZI ULIOPO UKIANZIA NA BODI UBADILISHWE
   
 4. B

  Bijou JF-Expert Member

  #4
  Jun 5, 2011
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 1,177
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145


  umesema vizuri sana mkuu
   
 5. kipindupindu

  kipindupindu JF-Expert Member

  #5
  Jun 5, 2011
  Joined: Dec 16, 2010
  Messages: 1,051
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  MSD isivunje lakini ipate mshindani,ukiritimba umezidi.hospitali za serikali zinakosa gauze kwa zaidi ya mwezi!gloves zinaisha ?!
   
 6. MKWECHE

  MKWECHE JF-Expert Member

  #6
  Jun 5, 2011
  Joined: Apr 8, 2011
  Messages: 299
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Na-Kifikiria Kwa Kiwango cha Tumbo Ni Hatari Zaidi!Sijawahi kuona MSD imefanya Vizuri na Lengo la Kuwa na Mfumo wa Central Medical Store Ume-Fail na Ndo mana siipendi MSD!Hao wahindi na Ma-DOMs,DTs na Wafamasia na Matumbo yao ni Majungu yako!Cha Uhakika Vituoni Dawa Hazipo Ilhali Zinaharibikia Bohari ambayo Lugha ya OS imezoeleka!
  Hao Wahindi wanapata wapi dawa na MSD wanazikosa!Mie sifikiirii kiwango cha Tumbo!Ila Ukubwa wa Tatizo Nafahamu na nimehangaika nao ndio mana nimeshangaa Dawa hatupati Wakati Zinaharibika!
  Kama nawe ni Nishemu ya Sisi Kukosa Dawa Uvuliwe gamba na Kingereza chako cha Ugoko!
   
 7. TabletFellow

  TabletFellow JF-Expert Member

  #7
  Jun 5, 2011
  Joined: May 17, 2011
  Messages: 928
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  MSD ina washindani tayari... wilaya zina fungu about 30% za kununua mitaani dawa zao ndio maana unaona counterfeit products zinashamiri baadhi ya maeneo

  cha kusema ni kwamba MSD ipate mshindani wa level yake.... lile shirika haliko efficient kabisa, kila kitu wanafanya wageni kama technical assistance

  hawana hata kitengo cha operational research sasa jiulize how can they lead products development, supply chain management strategies au purchasing environment

  LILE CHAKA LA WATU MAZEE
   
 8. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #8
  Jun 5, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  KWELI KABISA MKWECHE... YAWEZEKANA MIMI NI MKWECHE WA MAWAZO NA KIINGEREZA CHANGU

  Hujui mfumo, huelewi wahindi wanatoa wapi dawa, hujui documents za kuonyesha product sources kama zikihitajika kwa government facilities zilizosource dawa kwenye private sources zinatengenezwaje, hujui main actors wa tanzania supply system, unajaribu kuwa emotional na kiingereza changu cha ugoko

  MSD is not a central medical store, it is a medical store department... in a decetralised health system, players ni wengi sana kuanzia mtumiaji, famasi, doctor, administrators, stock managers, transporter, community funds, suppliers (MSD ni major), wizara ya afya na hazina.

  MSD is a strategic organization; tatizo si MSD kama shirika, tatizo ni waliopewa dhamana ya kuongoza na kuintegrate roles za MSD na clients wake ambao kwa upande mmoja ni suppliers, na upande mwingine ni serikali, vituo vya afya na wagonjwa

  kuna siku utaelewa hasara za kuvunja MSD, ila kupata mshindani wa MSD hakuna hasara

  BTW, umeshawahi kujua price variation ya paracetamol tu?? basi ni zaidi ya asilimia 1000

  ....ugoko unawasha
   
 9. N

  Ngonini JF-Expert Member

  #9
  Jun 5, 2011
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 2,024
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Tusicheze na afya zetu, msd lazima ibaki ila tatizo ni uendeshaji tu ambao ni janga la kitaifa kwa Tanzania ya leo toka Rais hadi mtendaji wa kijiji.
   
 10. MKWECHE

  MKWECHE JF-Expert Member

  #10
  Jun 5, 2011
  Joined: Apr 8, 2011
  Messages: 299
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Ugoko Ukiwasha Piga Kidochi cha Budi la JESHI!
  Fikra Kiwango Cha Tumbo Basi!
  Mie Mkweche nachotaka nikitaka dawa nipate!
  Mambo hayo ya Systems na Strategies sijui Chain Supply zote Polotiki!
  Lugha yenu Ya OS na wakati Midawa Imeozeo store wakati Mahospitalini tunakosa Dawa za Kutibu wagonjwa ndo niSioutaka!
  Matumbo yajae yasijae Soluu ni aliekwamisha na Kuasisi Lugha ya Kuna Dawa,Atupiwe Virago pamoja na wewe!Mzee wa Ugoko!
   
 11. MANAMBA

  MANAMBA Senior Member

  #11
  Jun 5, 2011
  Joined: Jan 16, 2011
  Messages: 169
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nchi hii ina nini? watu wanapoteza maisha huko vijijini kwa kukosa dawa wakati dawa zinaachwa ziharibike kiasi hicho. Shame on them
   
 12. kipindupindu

  kipindupindu JF-Expert Member

  #12
  Jun 5, 2011
  Joined: Dec 16, 2010
  Messages: 1,051
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  sio vijijini hapo mwananyamala na ilala watu wanakufa kukosa dawa!
   
 13. S

  Sakane Member

  #13
  Jun 5, 2011
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 18
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  tusilalamikie MSD kwakuwa na wao wana mipango yao ya kazi ya mwaka mzima, sasa wameandaa budget wamenunua dawa kutokana na mahitaji na wakati huo huo Serikali imepokea msaada wa dawa toka kwa wafadhili na labda zinazokaribia kutumika (mambo ya misaada!) Wanasema peleka Bohari Kuu zikatunzwe, sasa hapa nani mwenye makosa. Hiyo kamati ya bunge ingetakiwa ifahamu kwa undani tatizo lipo wapi tusije wahukumu na wao wanatafuta cheap popularity,tena ni iaongozwa na wabunge wa CCM ambao wanatakiwa wasupport mkuu wao alivyokua anatoa ahadi kwenye uchaguzi uliopita
   
 14. MKWECHE

  MKWECHE JF-Expert Member

  #14
  Jun 5, 2011
  Joined: Apr 8, 2011
  Messages: 299
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Kilichabainisha Si Wabunge ni Riport ya CAG Kaka!
   
 15. S

  Sakane Member

  #15
  Jun 5, 2011
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 18
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Sawa ripoti ya Mkaguzi inasema hivyo ila alichambua kiini cha tatizo? Wenyewe MSD wanasema hizo zilizoharibika ni zile zilizotolewa msaada na wafadhili zikaja changanywa na stock za kwao walizokwisha nunua unategemea nini? Ilitakiwa serikali kuwasiliana na MSD kuitaarifu jamani kuna msaada na mbaya zaidi unakuta mara nyingi zinakuwa zinazokaribia kwa matumizi yas binadamu labda bado miezi minne mpaka sita unategemea nini? Sio nawatetea MSD ila mfumo wenyewe ungetakiwa kurekebishwa na huyo CAG angetakiwa ashauri both to Serikali na MSD ukiangalia kwa undani siku hizi ni kutafutana tu, hivi mbona hatusikii Budget ya Idara ya Bunge wametumiaje? Na wamepangiwa kiasi gani kwa Mwaka,hata hizo Tume za Bunge kwa maoin zina misuse Govt fund, what is their role kama walishapitisha budget then wanakwenda kukagua? Na CAG? Je wao wanakaguliwa na nani?
   
 16. I

  IPECACUANHA JF-Expert Member

  #16
  Jun 6, 2011
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 2,127
  Likes Received: 291
  Trophy Points: 180
  MSD kama taasisi iliyonajukumu la kuhifadhi dawa inategemewa kwamba kiasi fulani cha dawa zitafikia mwisho wa matumizi zikiwa bado hazijasambazwa. Dawa ambazo nazizungumzia ni zile ambazo pamoja na kuwa na matumizi madogo lakini ni muhimu kuwepo kwenye hifadhi. Pia zipo dawa ambazo muda wake wa matumizi (shelf life) ni mfupi mfano (miezi 24). Dawa hizi pia zinaingia kwenye kundi la dawa ambazo uwezekano wa kuharibika zikiwa kwenye hifadhi ni mkubwa.
  Thamani kubwa ya dawa iliyotajwa si kiashiria kizuri cha ufanisi wa MSD pamoja na sababu nilizozitaja na nyingine za msingi NI VYEMA TUKACHUKUA ANGALIZO KATIKA YAFUATAYO
  • MSD imefuta dawa za thamani iliyotajwa baada ya MUDA GANI? Baadhi ya vyombo vimeripoti kwamba ni dawa za miaka 9(kuanzia 2002)
  • Dawa zilizoisha muda wake zikiwa kwenye hifadhi ni asilimia gani ya dawa zilizonunuliwa na kuhifadhiwa kwa kipindi hicho?
  • Mabadiliko ya Miongozo ya Matibabu Nchini mfano kuondoa Klorokwini katika utaratibu wa tiba ya malaria yamechangia kiasi gani katika thamani ya dawa hizo???(zilizoisha muda wake)
   
 17. I

  IPECACUANHA JF-Expert Member

  #17
  Jun 6, 2011
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 2,127
  Likes Received: 291
  Trophy Points: 180
  Kwa kuongezea hivi unaweza kuifanya taasisi ambayo lengo lake ni kutoa huduma bila kutengeneza faida(service oriented) kufanya kazi nzuri kwa kuipa mshindani ambaye ni mfanyabiashara? Hivi muhimbili hospitali imemsaidia vipi mlalahoi kwa sababu Aga Khan hospital ipo ikitoa huduma hiyo hiyo ya tiba? Sidhani kama ni busara kufumua mfumo wa maji uliopo(mabomba) kwasababu maji hayatoki kama hatua ya kutatua tatizo la maji.
   
 18. t

  tambarare Senior Member

  #18
  Jun 6, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 148
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  yaaani huu ni uzembe ambao hauvumiliki hivi kwa nini rais asipunguziwe madaraka ili wakurugenzi wawajibike kwa mtu mwingine na sio rais?????????? kibaha hosp. hawana huduma ya xray kwa zaidi ya miezi minne tatizo MSD hawana vifaa vinavyotakiwa kutolea huduma hiyo......nani ambaye hajui umuhimu wa huduma hiii ? ukizingatia kibaha hosp. ipo zone ambayo kila kukicha kuna ajari nyiiingi zinatokea zikiacha majeruhi kibao wanaohitaji huduma ya xray ili wapate matibabu mie nadhani huyu jamaa aondolewe mara moja hawezi kazi
   
 19. S

  SURUMA JF-Expert Member

  #19
  Jun 6, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 2,908
  Likes Received: 124
  Trophy Points: 160
  MSD kama taasisi zetu nyingine nchini inatagubikwa na URASIMU na UHABA umakini katika utendaji kazi wake!!!! Kama umepewa dawa za massada; unapooagiza stock mpya mwakani si unaangalia kwanza ULIZOPEWA BURE ZITATUMIKA WAPI KABLA HUJAAGIZA NYINGINE??Hiyo haihitaji uwe umesomea procurement kuijua maana hata home huwezi b=nunua nyanya wakati zilizo kwenye friji zinakaribia kupitiliza kuiva!!!!

  Ubangaizajio na WIZI vinachangia haya yote!!!!! KUna wakati nahisi hii hali ya confusion/sintokujua na kuchanganya mambo katika Taasisi zetu inafanywa makusudi kuwanufaisha waliokatika nafasi za maamuzi kwenye taasisi husika!!!
   
 20. Glue

  Glue Senior Member

  #20
  Jun 6, 2011
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 123
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  MSD imeshindwa kazi. Viongozi wawajibishe pamoja na kurasimisha bohari binafsi. Kila mwaka MSD inafanya stock taking tena kwa mwezi mzimaa! Iweje washindwe kugundua dawa za gharama kubwa kiasi hiki kuharibikia ghalani. Hii haivumiliki kwakweli.
   
Loading...