Huu ni ushauri wangu kwa Young Killer baada ya kutoa sinaga swaga

Mr Suprize

JF-Expert Member
Dec 18, 2014
858
937
Nimekuwa mshabiki na mfuatiliaji wa muziki wako kwa muda mrefu sana sijawahi kuchoka kusikiliza nyimbo zako hata siku.

Ulivyotoa huu wimbo wa sinaga swaga nimeusikiliza kama mara 10 hivi umeutendea haki ila umefika kuharibu sehemu ndogo sana baada ya kuingiza huu mstari unaosema "...WAAMBIENI SIMBA, YANGA NDO MABINGWA..."

Ukiwa maarufu au jina lako ni kubwa sana katika jamii ni vyema kulinda heshima yako ili jamii iweze kukuona unaheshimika,kuna vitu vingi vinaweza kukushushia heshima uliyojiwekea katika jamii, mojawapo ni kujiweka wazi kuwa umeegemea upande flani kwenye mambo yanayoigawa jamii. mfano Timu, Chama, kikundi n.k

Hatuzuii usiwe na timu au chama ila ni vizuri usipende kuweka wazi sana haya mambo yanayoigawa jamii, ni bora ungesema ..."WAMBIENI SIMBA YANGA, TOTO NDO MABINGWA.." hapo ungekuwa umebalance pande zote mbili ziko sawa. sababu tunajua wewe ni mzaliwa wa mwanza na unaipenda timu yako ya nyumbani toto africa tusingehoji hata sekunde..

Kwa mstari huu .."waambieni simba yanga ndo mabingwa".. naamini mashabiki wengi wa simba wataanzakupunguza kasi ya kukufwatilia kwenye muziki wako.

Ila sina sio mbaya yote mema tunaamini SINAGA SWAGA itafika sehemu nzuri. Mungu aibariki.
 
Afiche fiche ya nini,ye ni shabiki wa Yanga,au kuna kosa kuongea ukweli? Chamsingi aendelee kufanya mziki mzuri tu atasapotiwa,maisha yake binafsi ni maamuz yake.
 
Afiche fiche ya nini,ye ni shabiki wa Yanga,au kuna kosa kuongea ukweli? Chamsingi aendelee kufanya mziki mzuri tu atasapotiwa,maisha yake binafsi ni maamuz yake.
afanye muziki ila asitumie muziki kuwachosha watu! yeye kama anataka kujulikana kama ni shabiki wa yangu angetamka hata kwenye interview inatosha, but asiwe anayaingiza kwenye muziki, atumie muziki kuwaunganisha watu ila sio kuwagawa watu kwa mapenzi yake binafsi..
 
Dogo mkali wewe hakuna kitu alichoharibu ,,yaan mech tu je wale waliokuwa CCM mbona bado mnawasapoti na mmeshasahau kabisa ,,, kuwa msanii hakumfanyi asiweze kuchagua anachokipenda
 
Mponde kwa mengine sio hilo, wakina Snoop Doggy, Drake, Usain Bolt ni mashabiki wa wazi kabisa wa Manchester United na sijawahi kusikia wakipoteza mashabiki kwa hilo, mtu ambaye hapaswi kuonyesha ushabiki wa wazi labda watu wenye mamlaka makubwa kama Rais, maana akionesha ushabiki siku akitoa msaada wa kawaida itaonekana kawapendelea, au marefa,wachambuzi,na viongozi wa TFF. Lakini msanii wala haathiri chochote ndio maana huwa kuna mechi za wasanii washabiki wa Simba vs wa Yanga na tunaenjoy hata kama msanii hayuko timu yako
 
Yap alichokiongea mleta mada ni kitu sahihi madhara yake hayawezi kuonekana kwenye redio ila kwenye shows atakazofanya. Kwenye official song hakutakiwa kusema hivyo.
 
Mbona hawa wasanii wenu pendwa Diamond na Kiba walikata viuno jukwaa la chama chakavu na bado mnawashabikia alafu Kiba mbona nae hajifichi ni shabiki wa kutupwa wa Yanga na usisahau mzee JK ni Yanga pia ila aliongoza nchi ngoja nivunge ila list ni ndefu muacheni Young Killer
 
Ila kweli unapokuwa star hutakiwi kuweka persona preference zako hasa zile zihusizo pande mbili zinazohitilafiana
 
Me amenikera aliposena wakimjibu ni madem zake

Angeacha watu wa reply asee ili vita iendelee na hapo tungepata mziki mtam sana
 
ndo maana mnaambiwa hiphop ni ngumu kuielewa hamsikii, kwa taarifa yako hilo ni fumbo kwa diamond(simba) na kiba (yanga), HIPHOP yahitaji umakini kuielewa.
... sawa mkuu kwa uchambuzi
 
Back
Top Bottom