Mr Attorney
JF-Expert Member
- Mar 30, 2020
- 25,536
- 34,676
Wakuu tukiwa tunaendelea na michakato ya kunadi wagombea wetu kutoka vyama mbalimbali wa ngazi mbalimbali katika maeneo mbalimbali nchini. Naomba tuweke kituo na tujadili hili lililotokea siku ya jana.
Kwa wale ambao huwa mna wasaa wa kutazama kituo cha ITV majira ya saa 3 usiku, siku ya Alhamisi , ni siku ambayo kituo hiki hutuletea kipindi cha Malumbano ya hoja.
Lakini tofauti na ilivyo na utaratibu au mazoea au sheria ambayo ITV wameijenga kati ya sisi watazamaji na wao wazalisha vipindi, tulipatwa na mshtuko mkubwa sana kiasi cha kushindwa hata kupumua vizuri baada ya kuona wanatulisha kipindi cha tofauti na kile ambacho kipo kwenye sheria na taratibu zetu za utazamaji.
Badala ya kipindi cha MALUMBANO YA HOJA, ITV walituwekea kipindi cha DAKIKA 45 ambacho kwa kawaida, mazoea na sheria huwa kinarushwa siku ya Jumatatu. Kipindi cha DAKIKA 45 kwa siku ya jana kilichorushwa tofauti na taratibu zetu kilihusisha mtangazaji au kwa kisukuma wanamuita host ajulikanaye kama Farhia Middle pamoja na mgeni mashuhuri, mwanasheria nguli, mkongwe mwenye ushawishi mkubwa nchini na duniani na mgombea na Rais mteule wa jamhuri ya watu watulivu Ndugu Tundu Antipas Lissu a.k.a kiboko ya vichwa ngumu.
Sasa kwa namna moja au nyingine nilitegemea ITV watuombe radhi sisi watazamaji wao ambao tulikuwa tumeandaa muda, nguvu, masikio na mapoint ya kutosha kwa ajili ya kipindi cha MALUMBANO YA HOJA.
Nina uhakika yale mahojiano ya Farhia na Lissu yaliwasababishia baadhi ya watu wazito msongo wa mawazo + kukosa usingizi.
My take: Mjitahidi muwe mnafuata ratiba tulizozizoea, wengine hatujazoea kupigwa makonde muda wa kulala au kumpumzika.
Ila Lissu ukimuacha ajieleze una-enjoy sana ndio maana hata dada Farhia alikuwa anatikisa kichwa kwa jinsi madini aliyokuwa anayatema mwanasheria na mtoa shombo ndugu Lissu yalivyokuwa yanamuingia.