Huu ni ulemavu au makusudi

Pdidy, aitwe huu uzi unamuhusu sana, ila sometimes ni lafudhi ya kabila. Mfano sisi Wanyiramba tuna matatizo ya kuweka L kwenye R
 
kwani ni fashion kuandika hivyo?sikuwa nafahamu
 
Wengine hata uwachape bakora hawawezi kuacha kwa sababu ni lafudhi ya kikwao, eg wakurya hawana L wana R

Ni kujiendekeza tu na kutokuwa na nidhamu. Mbona Nyerere alijifundisha na akaelewa na alikiri kuwa alipopokelewa na wazee wa Dar hata Kiswahili alikuwa hajui vizuri.
 
Tusiwalaumu sana bali tuendelee kuwasaidia kuwauonesha kosa kila linapotokea, kwa "experience" yangu humu jamvini nimekuwa kila nnapoliona kosa la R na L huwa najaribu kulionesha, na wengi sana wanajirekebisha. Mmoja wao ni Yericko Nyerere, anajaribu sana siku hizi kuweka sawa.

Tukumbuke kuwa wengi ya Watanzania lugha yao ya kwanza (mama) si Kiswahili na Kiswahili wanachokumbana nacho walipo toka wakiwa wadogo ndio hicho kisichokuwa na nidhamu ya matamshi.

Tuendelee kueleimishina tusikate tamaa hakuna aliye kamilika.

Kingine kinachokera ni ile yakuongea "ga" kwenye maneno, mfano, "tunakwendaga", "hakunaga", "wanasemaga"

hizo "ga" hazina maana yoyote kwenye Kiswahili na hazipaswi kuwepo, lakini ndio hivyo tena.

Tukienzi na tukilinde Kiswahili chetu, ni lugha tamu sana ikiwa itatunzwa lafdhi yake.
 
Last edited by a moderator:

Jamani mimi nimeshashindwa kabisa, R na L zinanitesa sana mpaka nakuwa nashindwa kuandika naona nitakosea, yaani sijui ni aje tu ila wanasema sisi wasukuma wengi zinatupa taabu sio mimi tu.
 
Last edited by a moderator:

Uliowah- uliyowahi
Kiswahili hukijui ila unataka kukosoa wenzio? Nenda kalale wewe
 
Acha utani mkuu. Wahehe hatuna r na v.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…