Huu ni ugonjwa mbaya.

Malila

JF-Expert Member
Dec 22, 2007
5,149
4,674
Kwa wajasiriamali,

Hakuna hatari kubwa kama kusema jambo hili nitafanya kesho,kwa sababu kesho ina mambo yake. Hakuna ugonjwa mbaya kama kusema bila kutenda. Ili ufanikiwe ni muhimu sana nadharia na vitendo viende pamoja.

Nayachangia haya kwa sababu nimeyaona ktk jamii yetu na mimi yameniathiri kwa namna moja ama nyingine. Kwa ulimwengu tuliomo kwa sasa,kila kitu ni mapambano makubwa.
 
Ni kweli brother, nadhani pia hili limeniaffect for a long time. "kesho huwa haifiki"
 
Ni kweli brother, nadhani pia hili limeniaffect for a long time. "kesho huwa haifiki"

kesho haitakaa ifike,umri unafika. siku moja nikasema nikifika umri fulani naacha kazi ili nijiajiri,mwenzangu niliyempa wazo hili akafanya kweli na leo ana kampuni yake na mshahara tulikuwa karibu sawa. Ukiweza kufanya kitu fanya leo.
 
Ni kweli kabisa

Nilijipa ka-homework fulani,nikagundua kuwa ugonjwa huu unaambukiza. Angalia mtu anayefanya mambo yake vizuri anafuatana na nani au angalia mtu afanyaye vizuri/vibaya ktk mambo yake asili yake au familia yake au alikozaliwa. Kwa ufupi ni vema kuwa makini ktk tabia zetu hasa tukitaka kuwarithisha watoto wetu namna nzuri ya kujiongoza kuelekea mafanikio yao.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom