Huu ni ugonjwa gani?

shafii77

Member
Mar 18, 2019
49
77
Habarini za usiku ndugu na rafiki zangu? Bila kusita niende moja kwa moja kwenye mada tajwa hapo juu. Mimi ni kijana mwenye umri miaka 26 nina mchumba wangu anasumbuliwa na tatizo, maumivu ya mara kwa mara chini na pembeni ya kitovu na maumivu hayo huvuta mpaka shingoni na mwili mzima, maumivu makali wakati wa tendo la ndoa hivyo kupelekea kukosa hamu kabisa ya kushiriki tendo.

Dalili zimeanza mpaka sasa takribani miezi minne, japokua mwanzo nilimpeleka zahanati kwa ajili ya vipimo vya awali majibu yakaja kwamba ana fungusi katika sehemu za siri hivyo kupewa dawa mpaka akapona lakini maumivu yameendelea mpaka leo hii kila akitaka kushiriki tendo la ndoa hayo maumivu hujitokeza kwa nguvu na kupata maumivu makali.

Amefanyiwa vipimo vya UTI, ugonjwa hana, hivyo nimekuja hapa ndgu nipate ushauri na mwongozo pia katika tatizo hili, je nikachukue vipimo gani tena ili kujua tatizo, ama huenda ni magonjwa ya STI,s na STDs yanamnyemelea, naombeni ushauri ndugu.
 
Back
Top Bottom