Huu ni ugonjwa gani? Msaidieni mama yangu madocta

Jul 19, 2013
16
8
Mama mmkubwa wangu anawatoto 10 ila baadaya kujifungua mtoto wake huyu wa mwisho alianza kubadilika ghafla akaanza tabia ya kuongea mwenyewe yaani kama anajibizana na watu na mara nyingine anafoka na huwa hatoki tena nyumbani na anaweza kuongea hivyo kwa siku nzima -ila mgeni akija humpokea vizuri na huweza kuongea nae vizuri kabisa bila hata mgeni kujua kuwa anatatizo lolote
-naombeni nisaidiwe kujua hili ni tatizo gani? Wengine husema nguvu za giza, wengine husema karukwa na akili sababu ya kuzaa watoto wengi ukweli hasa uko wapi? ., nini madhara yake lisipotibiwa mapema?
- nini matibabu yake?
 
Duh huyo ana psychosis au ugonjwa unaoitwa SCHIZOFERNIA anahitaji antipsychotics(typical or a-typical)....Samahani mpeleke kwa daktari wa magonjwa ya akili...
 
Mama mmkubwa wangu anawatoto 10 ila baadaya kujifungua mtoto wake huyu wa mwisho alianza kubadilika ghafla akaanza tabia ya kuongea mwenyewe yaani kama anajibizana na watu na mara nyingine anafoka na huwa hatoki tena nyumbani na anaweza kuongea hivyo kwa siku nzima -ila mgeni akija humpokea vizuri na huweza kuongea nae vizuri kabisa bila hata mgeni kujua kuwa anatatizo lolote
-naombeni nisaidiwe kujua hili ni tatizo gani? Wengine husema nguvu za giza, wengine husema karukwa na akili sababu ya kuzaa watoto wengi ukweli hasa uko wapi? ., nini madhara yake lisipotibiwa mapema?
- nini matibabu yake?

Pole sana mkuu, kama mama amepata tatizo la kiakili baada ya kujifungua mtoto hiyo inaitwa PUPERIAL PSYCHOSIS... Ni vyema mama huyu akafika hospitali na kuonwa kwani mwishowe anaweza kuwa anapata HALLUCINATION kusikia sauti zinazomwelekeza afanye nini kama kumdhuru mtoto, kuchoma nyumba na pia anaweza kupata kitu kinaitwa DELUSIONS... Hizi ni false fixed beliefs kama mtu kuamini kuwa yeye anaitwa na Obama na anataka kusafiri, n.k hivyo mpeleke hospitali ndugu
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Yaani kajifungua 'mtoto huyu wa mwisho' ambae ni wa 10 hivi karibuni? Lazma adate aisee. She is shutting down her mind, m0elekeni hospitali.
 
Tatizo lake halikusababishwa na uzazi wa wtt 10 hata siku moja!

Kuna maradhi ya stress! Ambayo yanakuja kwa mitindo tofauti!

Wako wengi huongea peke yao! Wengi huwakosesha mpaka hamu ya kula na hawatoki vyumbani mwao!

Kuna wengi hula chakula kupita kiasi na huamua kwenda popote saa yyt bila kujali matokeo!

Na kuna wengi kila ukifanyacho kwao ni balaa tu! Hata ujaribu kuwafurahisha vipi!
Maradhi hayo ni very common hapa England! Na yanatibika kirahisi tu!

Kikubwa ni kufuata masharti yote atakayopewa na daktari!

Nakushauri umpeleke kwa psychiatric doctor (daktari wa magonjwa ya akili)
Huenda akipewa anti depression tablets tu atapona kwa uwezo wa Mungu!
Na hizo dawa za antidepressants zina side effects nyingi lkn ukiwa na subira zinasaidia sana!

Yuko brother wangu alikutwa na matatizo kama hayo akapewa hizo dawa!
Siku 4 za kwanza hatukuona dalili zozote tofauti! Lkn baada ya wiki alikuja nyumbani kwangu kama saa nane usiku akaniambia kuwa anahisi kama mji mzima unapigwa mdundiko! Kwa hiyo kashindwa kulala kabisa!
Na hiyo ni moja ya side effect!

Mungu amfanyie wepesi inshallah.
 
mama yangu mzazi aliwahi kuupata huo ugonjwa baada ya kujifungua mdogo wetu wa mwisho,na sisi tupo watatu, tena alikua kama kichaa kabisa anapiga watu,anaongea mwenyewe,anaondoka nyumbani anakoenda hapajulikani,for sure tuliteseka sana ila tulimpeleka kwa daktari bingwa wa magonjwa ya akili anaitwa dokta ringo yupo pale mawezi kitengo cha magonjwa ya akili,ndani yamiezi miwili tu alitumia dawa na amapona mpaka sasa huwezi kujua kama aliwahi kupata magonjwa ya namna hiyo
nakushauri waone wataalamu wa magonjwa ya akili,hilo tatizo linatokana na mazingira ya kujifungua
 
Back
Top Bottom