Huu ni Ufisadi katika Ajira au ndo kawaida | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Huu ni Ufisadi katika Ajira au ndo kawaida

Discussion in 'Nafasi za Kazi na Tenda' started by kabila01, Sep 1, 2009.

 1. kabila01

  kabila01 JF-Expert Member

  #1
  Sep 1, 2009
  Joined: Apr 21, 2009
  Messages: 3,012
  Likes Received: 1,821
  Trophy Points: 280
  habari wana Jamiiforums
  nimejitokeza niweze kupata mawazo na kueleweshwa kutoka kwa ndugu zangu wana Jamii.
  Kuna shirika moja lilitangaza nafasi za kazi ya Uhasibu na wakasema sifa za muombaji awe na shahada ya Uhasibu au utawala na Biashara.
  Kilichoniacha hoi ni pale tulipoitwa kwenye Interview kati ya watu 30 tulioitwa tuliosomea uhasibu pamoja na utawala wa biashara tulikua jumla wanne tu na post zilikua saba. wengine walikua wamesoma kilimo, Sheria na uchumi. cha kushangaza ni kwamba waliopita kwenye ile interview ni wale waliosoma kilimo na sisi wote tuliosoma Uhasibu, Uchumi na Biashara tukapigwa chini.
  sasa hapo nashindwa kuelewa kwamba kwa sababu waliosoma kilimo ndani yake eti walisoma somo la uhasibu ndo wakapata nafasi na sisi tuliosoma Uhasibu kwa miaka mitatu pamoja na mazoezi ya vitendo ya uhasibu tukapigwa chini ni kwamba tulishindwa kujieleza kwenye usail au ndo Ufisadi ndani ya ajira.
  Naomba mnisaidie wana jamii kunielewesha hapo
   
 2. Muota Ndoto

  Muota Ndoto Member

  #2
  Sep 1, 2009
  Joined: Dec 4, 2007
  Messages: 79
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Pole sana jamaa yangu. Ninachojua interview inahusisha mambo mengi ikiwa ni pamoja na staha, uelewa wa current issues kitaifa na kimataifa, siasa, utamaduni na pia kuhusu masomo ya darasani. Wakati mwingine kutokana na suala la wizi wa mitihani na vyeti ambalo kwa bahati mbaya sasa limafikia hadi vyuo vikuu, waajiri hawaamini tena vyeti na hata vilivyoandikwa humo. Hivyo wanatoa mitihani yao kupata picha ya uelewa wako na kulinganisha na cheti. Sasa kama wewe una BA Economics and Management na unashindwa kuelezea chanzo cha anguko la uchumi duniani na kuna mtu ana BSc Agriculture General anauelezea kwa ufasaha, hapa nani aajiriwe? Nina mfano wa Kijana mmoja aliitwa kwenye usaili katika taasisi moja ya elimu ya juu inayochipukia kwa kasi katikati ya nchi. Huyu alikuwa na shahada ya kwanza ya mambo ya ICT toka chuo kimoja mkoani Morogoro. Pamoja na kuwa na daraja la kwanza GPA 4.8 alishindwa kujibu hata swali moja kwa ufasaha. Liwe la kifani au mambo mengine. WITO WANGU KWA WATANZANIA HASA WANAFUNZI. mUACHE KUIBIA MITIHANI NA KUZEMBEA MASOMO. FAINALI ZAKE NI KATIKA KUTAFUTA KAZI!!!
   
 3. m

  mkulu Member

  #3
  Sep 1, 2009
  Joined: Mar 27, 2009
  Messages: 47
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  @Muota Ndoto ...... Well said!!
   
 4. kabila01

  kabila01 JF-Expert Member

  #4
  Sep 2, 2009
  Joined: Apr 21, 2009
  Messages: 3,012
  Likes Received: 1,821
  Trophy Points: 280
  Badohaijaniingia Akilini kwanza tuliofanya application watu wa uhasibu tulikua zaid ya 40 lakini kwenye short list tukachukuliwa wanne tu. na ile taasisi ni ya fedha
   
 5. The Farmer

  The Farmer JF-Expert Member

  #5
  Sep 2, 2009
  Joined: Jan 7, 2009
  Messages: 1,581
  Likes Received: 433
  Trophy Points: 180
  Kuna uwezekano hiyo taasisi ilikuwa inadili zaidi na mambo kilimo zaidi ndio maana wakawachukua hao waliosoma kilimo. Kwani wewe hufahamu kuwa kuna degree za AgroBusiness na AgroEcomomics!!

  Tupe maelezo zaidi ili tuweze kuchambua zaidi.
   
 6. Ramthods

  Ramthods JF-Expert Member

  #6
  Sep 2, 2009
  Joined: Jun 2, 2009
  Messages: 494
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  Pole sana kabila01.

  Ingawa hujatoa maelezo kamili kuhusiana na hiyo wizara na qualification za watu zilizokuwa zinahitajika, mambo kama haya hapa Bongo ni ya kawaida sana.

  Inawezekana pia nyie wanne hamkufanya vizuri kwenye interview - ila nalitilia shaka hilo pia kama kweli hiyo ndio ilikuwa sababu. Pengine labda utupe undani zaidi interview ilikuaje.

  Naweza kusema 60% - 80% ya ajira zinazotangazwa hapa Bongo tayari zinajulikana nani na nani wataajiriwa - wengine inakuwa ni kuzuga tu kama ushahidi kuonyesha utaratibu husika ulifuatwa.

  Hamna tofauti sana na tenda zinazotangazwa kwenye media - wengi wanashinda hizo tenda kwa kutumia vi-memo au kutoa hela kwa wahusika - We utaandika proposal ilioenda shule lakini tenda utazisikia tu kwa wenzio - ndio mambo ya serikali hayo.

  Mdogo wangu alifanya interview - wao walikua 18. Mchujo ukaenda hadi wakabaki 2, na alikua anahitajika mtu 1 tu - so ungedhania ni lazima angechukuliwa yeye au mwenzake.

  Cha kushangaza ni kwamba kuna jamaa alionekana kwenye interview ya mwisho na ndio aliyepata ile nafasi - huko mwanzoni kote alikua hayupo na sio miongoni mwa wale 18 walioitwa.

  Wakati wanaendelea kufuatilia majibu, kwa bahati nzuri mdogo akakutana na msichana mmoja "family-friend" wetu - mdogo wangu hakujua kuwa alikua anafanya kazi kwenye zile ofisi.

  Yule dada akasema "Ungejua ungeniambia mapema ningekuambia tu usipoteze muda wako. Huyu aliyepata hii nafasi mbona alishaanza kazi tayari hata kabla ya interview!"

  So kumbe kwenda kwenye interview ilikua ni kama alikua anapoteza muda wake tu!

  Ndio ajira zetu hizo ndugu yangu!
   
 7. kabila01

  kabila01 JF-Expert Member

  #7
  Sep 3, 2009
  Joined: Apr 21, 2009
  Messages: 3,012
  Likes Received: 1,821
  Trophy Points: 280
  Post ilikua ni ya Accountant na Qualification ni bachelor of Busines Administation, Bachelor of commerce plus CPA na experience in related field iwe ya miaka 2 and above
   
 8. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #8
  Sep 3, 2009
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,356
  Likes Received: 3,122
  Trophy Points: 280
  kuwa muwazi mjomba ni kampuni gani hiyo isije ikawa hata sie wengine tuliisha tuma mara kibao bila mafanikio tuijue tujue chakufanya zaidi.Hii nchi tusipokuwa wawazi hatufiki popote.Sehemu kibao kuna ukabila japo hausemwi waziwazi.Ukicheki vyombo vya fedha vyote kwamfano unakuta wachaga tu.......
   
Loading...