texaz mc
JF-Expert Member
- Jan 15, 2016
- 371
- 205
Habari za asubuhi wadau wote wa Jf.
Jana niliangalia kipindi cha "MWANAZUONI WETU" kinachorushwa TBC 1.
Jana walirusha kipindi hiko wakiwa chuo kikuu cha UDSM, Mada kuu ilikua ni umuhimu wa utafiti kwa maendeleo ya viwanda. Lakini kabla ya kuanza kulikua na maonesho ya bidhaa za kiutafiti zilizotengenezwa na wanavyuo wa hapo UDSM. Cha ajabu kuna kijana mmoja mimi nilidhani atajinadi kuwa ametengeneza mashine ya kuandalia juice kumbe la!!! Eti alijinadi bila aibu kuwa mimi ni mwanafunzi wa engineering hapa UDSM nimetengeneza "JUICE YA MABIBO" aiseee nilimshangaa sana huyu kijana.
Ujue kuna vijana kama hawa wanaingia katika fani hii ya uhandisi kwa infuences kutoka kwa marafiki zao nasi kwa wishes zao na ndio maana wanabuni vitu ambavyo havimtofautishi na mamantilie anaetengeneza juice ya maembe. Na hawa ndio huja kulalamikia ajira kwa sababu hawana ujuzi wa kiuhandisi.
Kwa ninavyojua mimi mhandisi ni wa kuzaliwa na si wa kusomea akiwa ukubwani, bali mhandisi aliejulikana tangu akiwa mtoto akisomea anaongeza maarofa na kua na uelewa mpana zaidi, na ndio maana kuna vijana hata hawajasoma hata elimu ya msingi lakini ni mafundi wazuri sana mitaani sasa mtu kama huyo akisomea si ndio balaa!!!.
UHANDISI NI FANI INAYOHUSISHA UBUNIFU WA HALI YA JUU KUUNDA KITU KITAKACHO ONDOA TATIZO KATIKA JAMII. Kwa mfano ukibuni taa ya kuongozea magari then ikawa automatic labda kila baada ya dk 10 inastop upande huu na kuruhusu upande mwingine hii itaondoa ttzo la foleni au hata kuwapunguzia matraffick adha ya kukaa juani lkn wanafunzi wetu wa TZ ndio kwanza eti wanatengeneza JUICE eti huyo nae ni engineer aisee kweli hii ndio TANZANIA.
Nawakaribisha wale ma engineer wote muitetee fani yenu maana si kwa kudhalilishwa huku.