Watanzania wengi ni wapenzi wa michezo haswa Soka, lakini pia ni washabiki wa timu za taifa na vilabu vilevile haswa Simba, Yanga na Azam.
Watanzania hupenda burudani ya mpira kwa kutazama uwanjani, kwenye Tv au kusikiliza redioni.
Leo Novemba 23, Timu ya Taifa ya mpira wa miguu kwa upande wa wanawake inacheza nusu fainali na timu ya Taifa ya Uganda baada ya kuzifunga Burundi, Zanzibar na Ethiopia.
Wakati huo huo, Azam ipo Mwanza inachuana na Mbao FC wakati Simba inachuana na Ruvu Shooting katika Uwanja wa Taifa.
Mechi zote tatu kubwa zinachezwa saa kumi kamili hivyo Watanzania watagawanyika katika kutazama. Ama utazame timu ya taifa, Simba vs Ruvu Shooting au Azam vs Mbao. Kama TFF wangekuwa makini, hizi mechi zingetenganishwa muda.
Hii ingetupatia mashabiki fursa ya kupata burudani zote. Pia mapato yangeongezeka maana wapo ambao wangependa kutazama mechi mbili au zote.
Afisa Mipango wa TFF ajitathmini.